Pure_sapiens
JF-Expert Member
- Dec 25, 2016
- 2,202
- 2,035
Habari Ndugu zangu wa JF natumaini nyote ni wazima kabisa,wote tunaendelee kujenga taifa la Tanzania kwani tutakumbukwa daima hata wakati tutakapo tangulia mbele za haki.
Pia namshukuru Mungu Kwa uzima huu, na shukrani zangu ziende kwa mh makonda kwa kujitokeza mafichoni na kutufuta tongotongo pia nawapongeza star tive kwa kujitoa katika kifungo.Niende kwenye maada~
Utangulizi~
Tanzania ilipata Uhuru 9 December 1961 tukio hili liliambatana na kuwashwa kwa mwenge na kuwekwa katika mlima Kilimanjaro, mwenge wa Uhuru ulikuwa na matumaini mapya kwa Watanzania wengi baada ya kutoka mikononi mwa waingereza.
Mwenge ulileta amani,furaha na matumaini kwa watanzania walio wengi,Mara baada ya Azimio la Arusha(1977) mwenge ukawa kama chachu ya maendeleo na kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo na kutungua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mwenge ulimgusa moja kwa moja mwananchi wa kawaida pia wananchi walishiriki kikamilifu katika sherehe za Mwenge.Nazani wote tunakumbuka kipindi cha nyuma tulivyokuwa tunajipanga barabarani kuupokea mwenge huku tukiimba nyimbo za kumsifu Mwl Nyerere.
SHEREHE ZA MWENGE MWAKA HUU
Jana mwenge ulikuwa mkoani Lindi katika wilaya ya Lindi v.Lakini cha kilichonishangaza ni hamasa ndogo kwa wananchi.Yaani wananchi hawakuwa na habari na Mwenge hii haikunifurahisha hata kidogo,Licha ya kuwa na msanii Snura aliyeimba wimbo pendwa wa chura alikuwa mburudishaji katika sherehe hizi.
Uwepo wa snura katika shughuli za mwenge Lakini pia wananchi wa Lindi hawakuja.Yaani nimethibitisha kuwa miaka hii hakuna uzalendo kabisa.
Ombi langu naomba serikali itumie nguvu ya ziada kuwalazimisha wananchi waende kwenye sherehe za mwenge Kwa lazima.
Je kwa Upande wako unadhani nini kifanyike kurudisha heshima ya mwenge kama miaka ya zamani.....Karibu kwa mjadala