Nini kifanyike kuokoa hali ya mazingira Tanzania?

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Amani iwe kwenu wadau,

Kama kawaida natumai wote mpo salama na mnaendelea vyema na mapumziko ya mwisho wa wiki.

Kama kawaida Nipo kwenye mfululizo wa kuleta mada mbalimbali ambazo naamini kama Taifa tukizifanyia kazi tunaweza kupata matokeo chanya katika uchumi na ukuaji kama Taifa.

Nilishawai kusema mwanzo kuwa kati ya vitu ambavyo Chama Kikuu hapa Tanzania walifeli ilikuwa ni kushindwa kupanga miji vizuri ivyo kupelekea ujenzi holela katika maeneo mengi nchini Tanzania.

Nilipendekeza kuwa njia sahihi ya kuondoa Tatizo hilo ni kutosubiria upimaji wa Serikali au kampuni binafsi ila tuanze kwa kuzipa Serikali za mitaa mamlaka ya kupanga maeneo yake na kuwaelekeza wananchi wake kujenga kimpangilio.

Hili hadi sasa niamini ni jambo litakaloleta mapinduzi makubwa sana katika mitaa yetu na miji yetu kupendeza na kupangika vizuri na Kikubwa ni pia halihitaji bajeti wala fedha.

Nilileta pia mapendekezo ya kuanzishwa kwa mabalaza ya kiuchumi, amani na mazingira kuwa kama vyombo vikuu vya juu vya kumshauri Mh Raisi katika mambo yanayohusu uchumi, amani na mazingira.

Nilipendeleza yaundwe kisheria kama lilivyoundwa baraza la usalama la taifa na ndo yawe vyombo vya mwisho vya kumshauri Mh Rais kwa maendeleo ya nchi na Taifa kwa ujumla.

Jana nilileta mada kuhusu nini kifanyike ili kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi na
Leo napenda kuzungumzia juu ya hatari ninayoiona inaweza kulikumba Taifa siku chache zijazo za usoni na hatari iyo ni nchi kugeuka jangwa na kupelekea kupata shida ya chakula na uzalishaji wa Nishati na kuongezeka kwa magonjwa kama kansa.

Naiona hii shida kulikumba Taifa kwa sababu dalili tayari ziko wazi. Kama una fuatilia Habari za ndani utakuwa uliona wakati Mh Rais ametembelea mbuga ya katavi alikuta kuna shida kubwa ya Maji iliyopelekea mto kukauka na kuamuru hifadhi ichimbe mabwawa na kuweka Maji kwa ajili ya wanyama.

Kama unatembea maeneo ya Tanzania utakuwa umeona pia maeneo ya Dodoma, Singida, Tabora, shinyanga na mwanza yalivyoathilika na ukame unaoenda kutishia uhai wa taifa siku si nyingi.

Sio hivyo tu utagundua kuwa hata mradi wa umeme wa rufiji pia una hatari wa kutozalisha umeme wa kutosha huko mbeleni kwa sababu mto Ruaha hali yake si Nzuri kabisa, ukame unaitisha sana mikoa ya Iringa na Morogoro ivyo kupelekea hatari kubwa kulala kutokea huko mbeleni.

Hata mikoa ya Kilimanjaro na Arusha nayo inaonekana kuwa na shida ya ukame unaopelekea kuanza kutokea shida ya maji

Kama Taifa lazima tushtushwe na hali hii na lazima kama watu tunaoona dunia inaenda wapi tutoe mchango katika kushauri nini kifanyike ili kuliokoa Taifa huko mbeleni.

Katika kupambana na Changamoto hizi za kimazingira napendekeza kama Taifa tufanye mambo yafuatayo

1. Ianzishwe kampeni maalum ya upandaji miti itakayoongozwa na jeshi la kujenga Taifa nchi nzima. Ipande Miti Mingi nchi nzima na msisitizo uwe kwenye vyanzo vya Maji na mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Iringa, Shinyanga, Simiyu, Mwanza, Kigoma na Kilimanjaro. Then mikoa mingine ifuate.

2. Serikali iache utaratibu wa kugawa maeneo ya hifadhi kwa wananchi kwa kiasi vizuri tu eti watu wanaongezeka. Maeneo ya hifadhi yalindwe na kuongezwa zaidi kwa faida za vizazi vijavyo.

3. Serikali ije na mkakati maalumu kwa kubadirisha aina ya ufugaji nchini. Inunue na kuingiza nchini teknolojia ya kufuga mifugo michache katika eneo dogo kibiashara. Teknolojia hii wapewe wafugaji kwa lazima na isiwe na majadala. Mambo ya kufuga ng’ombe 1000-5000 yasiwepo tena.

4. Mamlaka za vijiji na mitaa zisimamiwe ipasavyo kuhakikisha kunakuwa na miti ya kutosha kwenye vijini/ mitaa yao na hili lisimamiwe na kamati za ulinzi za wilaya.

5. Serikali iangalie kutumia njia za kilimo kama za Israel katika kuleta mapinduzi ya Kilimo. Watu wapewe pembejeo nzuri na njia za asili za kupambana na majanga ya kilimo kama kutumia wanyama na ndege mfano bundi kwa maeneo yenye panya wengi zitumike.

Hili litasababisha tusitumie Madata ambayo yanaharibu rutuba ya Ardhi na kupelekea kilimo kuwa kigumu na watu kuhitaji maeneo makubwa zaidi kwa ajili ya kilimo.

Naomba kuwasilisha.
 
Moshi where Im from is even worse!
Sio Moshi tu ndugu, maeneo mengi ya Tanzania hali inasikitisha. Hatua za haraka lazima zichukuliwe kama wanavochukua duniani huko.

Kuna picha juzi niliona ilipigwa kwenye mradi mmoja wilayani Bahi. Nilitamani hadi kulia. Natembea mikoa mingi hali inasikitisha sana. Kama Serikali inatakiwa kuwa mbele kifikra na kuyaona haya na kuyaletea majibu ya uhakika.
 
Walao nilichojaribu kufanya,ni kuotesha miti kwa hali na mali shambani kwangu!

Walao wanakijiji wanaiga!

Hii kitu serikali iingilie kwa makusudi kama ulivyo suggest!

Wanasiasa wetu wenye madaraka sasa,hovyo kabisa!
 
Serikali ina vpaumbele vyake kwa sasa!au ww ni mgeni hapa nchini mkuu?mbona vipaumbele vyetu hawa watoto wanajua???
 
Walao nilichojaribu kufanya,ni kuotesha miti kwa hali na mali shambani kwangu!

Walao wanakijiji wanaiga!

Hii kitu serikali iingilie kwa makusudi kama ulivyo suggest!

Wanasiasa wetu wenye madaraka sasa,hovyo kabisa!
Tatizo kubwa kwa wanasiasa wengi ni maslahi binafsi. Mawaziri hawawazi kuisaidia nchi kwa kumshauri Mh Rais vizuri. Wao wanawaza kufanya vitu ili kupata cheap popularity.

Haya ndo mambo ambayo kama Taifa tunatakiwa tujikite nayo na sio kuwaza mambo ya ovyo.

Kuna muda namuonea huruma Magufuli kuwa anazungukwa na watu wa hovyo wasioweza kushauri mambo mazuri kwa mustakabali wa Taifa na vizazi vijavyo
 
Hatuwezi kujisifu kuwa tuna utajiri wa akili au fedha au afya njema kama mazingira yetu ni machafu kiasi hiki
 
Mkuu

Mawe tu ndio ana shida yeye mwenyewe!

Yeye akitamka tu lazima kifanyike,ila yeye hatamki!

Ndio kwanza kaenda kuharibu river basin yote ile ana jenga Stiglers!

Kakata miti yote mto mzima,kang’oa mawe yote,kaharibu uoto wote na karibu robo ya pori la Selous kaharibu lote sababu ya Stiglers!

Wakati angetumia gesi ya Kusini na angepata matokeo makubwa zaidi ya umeme!

Mkuu hatuna mtu mkereketwa wa mazingira!

We are all fucked!
 
Kweli kabisa ndugu, Ni aibu ukitembea Tanzania. Watu hawajali kabisa mazingira na inaonekana kama na serikali either hawajui au hawaoni kuwa kuna umuhimu wa kutunza mazingira.

Watu hawajui kuwa mazingira bora na mazuri ni moja ya kichocheo kikuu cha afya njema. Hawajui kuwa uwepo wa miti unapunguza hewa chafu angani ivyo kupunguza risky za watu kupata magonjwa kama kansa n.k
 
JPM ana nafasi ya kurekebisha haya.
Suala ya Umeme wa mto Rufiji hata mie sikulisupport kwa sababu za mazingira ila kwa sababu umeme wa maji haunaga athari kubwa za kimazingira niliona ni vizuri ujenzi ufanywe.

Shida inakuja kwamba kwa kasi ya uharibifu wa mazingira mikoa ya Pwani, Morogoro na Iringa ambayo ndo inatoa maji ya Bwana lile je litakuwa efficient kwa miaka mingi ijayo??? Yaani kiwango cha Maji kitakuwa kile kile au kitaongezeka????
 
Kuwe na push ya makusudi toka kwa mwenye nchi!

Otherwise ni total destruction all the way through!
 
Amani iwe kwenu wadau,

Kama kawaida natumai wote mpo salama na mnaendelea vyema na mapumziko ya mwisho wa wiki.

Kama kawaida Nipo kwenye mfululizo wa kuleta mada mbalimbali ambazo naamini kama Taifa tukizifanyia kazi tunaweza kupata matokeo chanya katika uchumi na ukuaji kama Taifa.

Nilishawai kusema mwanzo kuwa kati ya vitu ambavyo Chama Kikuu hapa Tanzania walifeli ilikuwa ni kushindwa kupanga miji vizuri ivyo kupelekea ujenzi holela katika maeneo mengi nchini Tanzania.

Nilipendekeza kuwa njia sahihi ya kuondoa Tatizo hilo ni kutosubiria upimaji wa Serikali au kampuni binafsi ila tuanze kwa kuzipa Serikali za mitaa mamlaka ya kupanga maeneo yake na kuwaelekeza wananchi wake kujenga kimpangilio.

Hili hadi sasa niamini ni jambo litakaloleta mapinduzi makubwa sana katika mitaa yetu na miji yetu kupendeza na kupangika vizuri na Kikubwa ni pia halihitaji bajeti wala fedha.

Nilileta pia mapendekezo ya kuanzishwa kwa mabalaza ya kiuchumi, amani na mazingira kuwa kama vyombo vikuu vya juu vya kumshauri Mh Raisi katika mambo yanayohusu uchumi, amani na mazingira.

Nilipendeleza yaundwe kisheria kama lilivyoundwa baraza la usalama la taifa na ndo yawe vyombo vya mwisho vya kumshauri Mh Rais kwa maendeleo ya nchi na Taifa kwa ujumla.

Jana nilileta mada kuhusu nini kifanyike ili kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi na
Leo napenda kuzungumzia juu ya hatari ninayoiona inaweza kulikumba Taifa siku chache zijazo za usoni na hatari iyo ni nchi kugeuka jangwa na kupelekea kupata shida ya chakula na uzalishaji wa Nishati na kuongezeka kwa magonjwa kama kansa.

Naiona hii shida kulikumba Taifa kwa sababu dalili tayari ziko wazi. Kama una fuatilia Habari za ndani utakuwa uliona wakati Mh Rais ametembelea mbuga ya katavi alikuta kuna shida kubwa ya Maji iliyopelekea mto kukauka na kuamuru hifadhi ichimbe mabwawa na kuweka Maji kwa ajili ya wanyama.

Kama unatembea maeneo ya Tanzania utakuwa umeona pia maeneo ya Dodoma, Singida, Tabora, shinyanga na mwanza yalivyoathilika na ukame unaoenda kutishia uhai wa taifa siku si nyingi.

Sio hivyo tu utagundua kuwa hata mradi wa umeme wa rufiji pia una hatari wa kutozalisha umeme wa kutosha huko mbeleni kwa sababu mto Ruaha hali yake si Nzuri kabisa, ukame unaitisha sana mikoa ya Iringa na Morogoro ivyo kupelekea hatari kubwa kulala kutokea huko mbeleni.

Hata mikoa ya Kilimanjaro na Arusha nayo inaonekana kuwa na shida ya ukame unaopelekea kuanza kutokea shida ya maji

Kama Taifa lazima tushtushwe na hali hii na lazima kama watu tunaoona dunia inaenda wapi tutoe mchango katika kushauri nini kifanyike ili kuliokoa Taifa huko mbeleni.

Katika kupambana na Changamoto hizi za kimazingira napendekeza kama Taifa tufanye mambo yafuatayo

1. Ianzishwe kampeni maalum ya upandaji miti itakayoongozwa na jeshi la kujenga Taifa nchi nzima. Ipande Miti Mingi nchi nzima na msisitizo uwe kwenye vyanzo vya Maji na mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Iringa, Shinyanga, Simiyu, Mwanza, Kigoma na Kilimanjaro. Then mikoa mingine ifuate.

2. Serikali iache utaratibu wa kugawa maeneo ya hifadhi kwa wananchi kwa kiasi vizuri tu eti watu wanaongezeka. Maeneo ya hifadhi yalindwe na kuongezwa zaidi kwa faida za vizazi vijavyo.

3. Serikali ije na mkakati maalumu kwa kubadirisha aina ya ufugaji nchini. Inunue na kuingiza nchini teknolojia ya kufuga mifugo michache katika eneo dogo kibiashara. Teknolojia hii wapewe wafugaji kwa lazima na isiwe na majadala. Mambo ya kufuga ng’ombe 1000-5000 yasiwepo tena.

4. Mamlaka za vijiji na mitaa zisimamiwe ipasavyo kuhakikisha kunakuwa na miti ya kutosha kwenye vijini/ mitaa yao na hili lisimamiwe na kamati za ulinzi za wilaya.

5. Serikali iangalie kutumia njia za kilimo kama za Israel katika kuleta mapinduzi ya Kilimo. Watu wapewe pembejeo nzuri na njia za asili za kupambana na majanga ya kilimo kama kutumia wanyama na ndege mfano bundi kwa maeneo yenye panya wengi zitumike.

Hili litasababisha tusitumie Madata ambayo yanaharibu rutuba ya Ardhi na kupelekea kilimo kuwa kigumu na watu kuhitaji maeneo makubwa zaidi kwa ajili ya kilimo.

Naomba kuwasilisha.
Sijui hata niongeze nn. Umemaliza kila kiitu... Serikali ICHUKUE MAWAZO HAYA MAZURI
 
Kweli kabisa ndugu, Ni aibu ukitembea Tanzania. Watu hawajali kabisa mazingira na inaonekana kama na serikali either hawajui au hawaoni kuwa kuna umuhimu wa kutunza mazingira.

Watu hawajui kuwa mazingira bora na mazuri ni moja ya kichocheo kikuu cha afya njema. Hawajui kuwa uwepo wa miti unapunguza hewa chafu angani ivyo kupunguza risky za watu kupata magonjwa kama kansa n.k

Nakubaliana na wewe!
Uchafu wa mtu utaujua kwenye fikra zake, matendo au mazungumzo yake!
Viongozi na watu wenye mawazo machafu hawawezi kusimamia usafi wa mazingira!

"As You Think;
As You Act;
So, You become!"
 
Mkuu

Mawe tu ndio ana shida yeye mwenyewe!

Yeye akitamka tu lazima kifanyike,ila yeye hatamki!

Ndio kwanza kaenda kuharibu river basin yote ile ana jenga Stiglers!

Kakata miti yote mto mzima,kang’oa mawe yote,kaharibu uoto wote na karibu robo ya pori la Selous kaharibu lote sababu ya Stiglers!

Wakati angetumia gesi ya Kusini na angepata matokeo makubwa zaidi ya umeme!

Mkuu hatuna mtu mkereketwa wa mazingira!

We are all fucked!

Yaani nikitafakari ukweli kwamba kwa sasa tu as we speak; hali si nzuri down-stream Rufiji basin and within/along the Great Ruaha River!
Sasa how will the situation be with an HP dam in place? 5yrs, 10yrs, 100yrs from now?
Kuna vitu tunajimwambafy tu lakini vinasaidia kuthibitisha kuwa ama akili zetu ni chafu sana ama sisi ni viumbe wa ajabu sana!
 
Back
Top Bottom