Nini kifanyike kukomesha Wanaume kuwatelekeza Mke na Mtoto/Watoto wao?

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
6,162
8,820
Ni jana tu tulikuwa tunazungumza na Mtu akanieleza namna ambavyo Dada yake alivyopambana na maisha mpaka kufikia kujijenga kiuchumi, aliweza kujijengea vyumba vyake viwili vya kuishi na biashara yake ya duka la rejareja.

Baadae alipata mwenza na kubahatika kupata Watoto wawili, baadaye Baba Watoto akaondoka na kumuachia Dada mzigo wote wa malezi hali iliyosababisha hali ya biashara kuyumba na ikambidi kufunga lile duka na inasemekana Jamaa tayari ameanzisha familia nyingine huko alipo huku Mama amebaki anateseka na Watoto.

Na leo nimesikiliza vipindi redioni nako nimesikia stori za kina Mama waliokimbiwa na Wenza wao na kuachiwa Watoto tena wenye changamoto za kiafya.

Tukomeshaje hili?.
 
Tunashukuru mabmdogo wakiwapa ukimwi wanaume zetu ndo wanarudi tuwauguze. Haki ya nani, utateseka mbaya nitakavyokufanyia.
 
Nasikiliza redio hapa Njia Panda...huyu Mama angekuwa na Mumewe wangeshirikiana Wamsaidie huyu Mtoto wao.
 
Dawa ni kujitunza na kujiheshimu. Ni kweli kuwa Kuna wanaume ambao hawajui kuwa kuna majukumu, na hao ndio kimbilio lenu. Kisa? Handsome,maarufu,ana six park,tunaendana,anavaa vizuri,mtanashati,ana gari,ana kazi nzuri n.k

Iwapo hamtafanya machaguo sahihi au mtayumba mkiwa katika machaguo sahihi kwa kuonyesha dharau,kiburi,jeuri,kukosa uaminifu na msimamo na kushindana na wanaume hivi vilio vitaendelea.

Poleni
 
Kuku akizaa anatunza watoto mwenyewe,mbuzi akizaa anatunza watoto mwenyewe, wanyama wote wakizaa wanatunza watoto wao wenyewe isipokua binadamu tu ndio hawezi kutunza watoto wake mwenyewe.

Kwa wanyama wote wa jinsia ya kike binadamu ama mwanamke ndie kiumbe selfish tu kwa mwanaume wake, hawezi kutunza watoto mwenyewe kama wanyama wengine, hawezi ama hataki kumruhusu mumewe awe na wanawake wengine kama wanyama wengine.

Anyway, haya ni mawazo yangu tu 😂
 
Dawa ni kujitunza na kujiheshimu. Ni kweli kuwa Kuna wanaume ambao hawajui kuwa kuna majukumu, na hao ndio kimbilio lenu. Kisa? Handsome,maarufu,ana six park,tunaendana,anavaa vizuri,mtanashati,ana gari,ana kazi nzuri n.k

Iwapo hamtafanya machaguo sahihi au mtayumba mkiwa katika machaguo sahihi kwa kuonyesha dharau,kiburi,jeuri,kukosa uaminifu na msimamo na kushindana na wanaume hivi vilio vitaendelea.

Poleni
Hiyo "chaguo sahihi" ni dhana pana maana hakuna Mwanaume atakayemfuata Mwanamke akiwa ameonesha uhalisia wake...huwa wananyenyekea na kumpa Mwanamke wakati mgumu kumjua kiundani.
 
Kuna aina mbili za kutelekeza watoto

1. Wanaume wapumbavu wasiojielewa ambao wanazalisha wadada na kukimbia majukum( hawa inabidi sheria kali itungwe kuwadhibiti hata ikibidi waasiwe)

2. Kuna wababa wanakimbia mateso kwenye ndoa( hapa sasa ni papana sana )
Jaman kuna ndoa wanaume wanateseka au wanapitia nyakat ngumu nyie achen tu! Babangu alishawah nieleza kuwa kuna kipind alichoka mpk alitaka kukimbia mji

(Wanaume wa iv mateso au ndoa ikizid kuwa ngumu kwao mwishowe huona badala ya kumfukuza mama akateseke na watoto wao huondoka na kuacha kila kitu wanaenda kuanza moja maisha)

Jaman kuna wanawake wanasumbua kwenye ndoa hasa ukikubali kujishusha na kuwa mpole ili angalau ndoa iwe na aman wao wanaitumia nafasi vzr na kuona wamekutawala na kukunyanyasa vibaya mno
 
Wanawake wajifunze malezi kwa viumbe wengine... Dume akishatia mimba ndio basi

Check kuku, mbuzi, simba nk
Sasa mbuzi na binadamu wapi na wapi wewe..... Mbuzi wanakula ugali?!

Mbuzi wanafunga ndoa?!

Mbuzi wanapiga kura?! Ingawa tunajua mbuzi wote wanakadi ya ccm.

Mbuzi wanasmartphone?!

Mbuzi wanajenga nyumba?!

Mbuzi wanatoka out?!

Mbuzi wanafanya shopping?!

Mbuzi wanaajiriwa?!

Mbuzi wanasoma?!

Eti wewe, si nakuuliza lakini?!
 
Asubuhi nimsikiliza RFA kuna Mama kakimbiwa kaachiwa Watoto saba, sasa hivi nasikiliza Clouds hapa Mama alienda kwao kujifungua jamaa akakata mawasiliano, Mama kurudi mjini kakuta Jamaa kahama pale walipokuwa wanaishi.
 
Sasa mbuzi na binadamu wapi na wapi wewe..... Mbuzi wanakula ugali?!

Mbuzi wanafunga ndoa?!

Mbuzi wanapiga kura?! Ingawa tunajua mbuzi wote wanakadi ya ccm.

Mbuzi wanasmartphone?!

Mbuzi wanajenga nyumba?!

Mbuzi wanatoka out?!

Mbuzi wanafanya shopping?!

Mbuzi wanaajiriwa?!

Mbuzi wanasoma?!

Eti wewe, si nakuuliza lakini?!
Tunaongelea malezi mkuu...
 
Kutoroka mimba au mtoto ni urithi.

Wengi wanaokimbia watoto ukifuatilia utakuta hilo tukio yeye kalikopi tu kutoka kwa mmoja wa wanaukoo.

Ni kama kujiua kisa mapenzi.
 
Dawa ni kujitunza na kujiheshimu. Ni kweli kuwa Kuna wanaume ambao hawajui kuwa kuna majukumu, na hao ndio kimbilio lenu. Kisa? Handsome,maarufu,ana six park,tunaendana,anavaa vizuri,mtanashati,ana gari,ana kazi nzuri n.k

Iwapo hamtafanya machaguo sahihi au mtayumba mkiwa katika machaguo sahihi kwa kuonyesha dharau,kiburi,jeuri,kukosa uaminifu na msimamo na kushindana na wanaume hivi vilio vitaendelea.

Poleni
Hii ni kweli kabisa. Wanawake huwa hawahitaji mwanaume serious hadi wakishapigwa mashine na kuzaa na wanaume wasio na ramani ya maisha hawa masharobaro wao hao.

Wengi wa mabinti niliokuwa nawatamani sana enzi zile za kupevuka sasa hivi ni walezi wa watoto bila baba. Na tukionana ni salamu tu na kusaidiana kama vijana ila mazoea nao sina.

Na mbaya zaidi wengi aidha wanaingia 30 au ndio wameshaingia.......

Sasa huwa nauliza hizi akili wanazokuwa nazo wakati huu mbona hazikuwako kipindi kile cha Maringo na kubetuliana midomo. Kila siku mtu anarudishwa na magari tofauti anakuangalia jicho la we bado mdogo tulia niwape utamu wa kubwa zako.

Nikikutana nao nowadays nawapa jicho la mbwa wa polisi.....
 
Back
Top Bottom