Nini kifanyike kuirejesha ccm kambini.

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
0
Huko nyuma nguvu za ccm zilitokana na chama hicho kwa dhati kabisa, kuwa mtetezi wa wanyonge kwa kauli na vitendo. Msimamo huo ulibadirika ghafla wakati wa uenyekiti wa rais wa hawamu ya tatu. Tangu hapo, chama hicho kikaanza taratibu kushiriki katika hujuma ya maslahi ya wanyonge kwa faida ya walionacho. Kutokana na uelewa mdogo wa watu wetu walio wengi, imechukua muda mrefu kwa watu kutambua hali hiyo. Hata hivyo kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na baadhi ya wanamapinduzi, ukweli huo sasa hivi unajulikana kwa watu wengi, kiasi kwamba bila ya kutumia nguvu za dola ccm ilikuwa imebwagwa vibaya katika uchaguzi mkuu uliopita. Sasa swali, hii ccm itaendelea kubebwa na dola mpaka lini? Ni nini kinachoizuia kuwarejelea wananchi wa kawaida?
 

nyantella

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
889
225
Kila taifa hupata serikali inayo listahili!!!! kama CCM imedhoofu ina maana utaifa wetu umedhoofu!! period.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom