Amicus Curiae
JF-Expert Member
- Sep 12, 2012
- 4,800
- 6,280
***MTAZAMO WANGU JUU YA MACHAFUKO JIJINI ARUSHA***
Martin Luther King aliwahi kusema...
"To know the enemy is half the victory"; yaani "Kumfahamu adui ni nusu ya kushinda vita"
Kwahiyo kwa lugha nyepesi kabisa hii ina maana kwamba, "UKIMFAHAMU" tu adui yako, unakua umeshinda 50% ya vita unayoenda kuipigana. Kwanini?
Kwasababu kumjua adui yako ni kufahamu mambo kama mbinu zake za kivita (je ni bora kuliko zako?), kufahamu ubora wa silaha anazotumia (je ni za kisasa kuliko zako?) n.k
Hivyo unapokwenda kupambana unakua unafahamu uanzie wapi na uishie wapi
Ukienda kupigana kwa kukadiria tu uwezo za mpinzani wako, mara nyingi utashindwa! Na ndio mana wataalam wakasema "Do not under-estimate the power of your enemy"
Sasa tuje ARUSHA, ni kweli kuna machafuko
Lakini hatujawa na uhakika kwamba ni nani hasa ni adui yetu, tuko dillema...kuna wanaoitaja CCM, wengine CDM, wengine wanayataja Mataifa ya Nje kama ndio maadui zetu
Hebu tuwe watulivu, tukishamfahamu adui ndio tujue ni vp tutakabiliana nae, tusiendeshwe na hisia/itikadi, kwasababu mfuasi wa CCM ataishutumu CDM, halikadhalika na mfuasi wa CDM ataikashifu CCM, ktk mazingira kama haya, kama adui ni Mataifa ya Nje, tayari anakua ametugawanya (divide and rule) na itakua rahisi kutumaliza kabisa!
Usijifanye mjuaji kwa kupost matusi humu, wa CCM unawatukana CDM na wa CDM unawatukana CCM, hakuna tuzo ya mfuasi bora wa chama, wala kuonyesha hisia zako hakutasaidia chochote ktk kurejesha amani Arusha...hata kama unapata coments na like nyingi, usivimbe kichwa ukajiona maarufu sana humu JF kwa kuwa na wafuasi wengi...kumbuka
HITLER alikua na wafuasi zaidi ya milioni na YESU alikua na wafuasi 12 tu, lkn YESU ni maarufu kuliko huyo HITLER ambaye kashaoza kaburini.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tz, Mungu ibariki Arusha!