Nini kifanyike kuinusuru Arusha? Soma hapa tafadhali...

Amicus Curiae

JF-Expert Member
Sep 12, 2012
4,800
6,232
***MTAZAMO WANGU JUU YA MACHAFUKO JIJINI ARUSHA***

Martin Luther King aliwahi kusema...

"To know the enemy is half the victory"; yaani "Kumfahamu adui ni nusu ya kushinda vita"

Kwahiyo kwa lugha nyepesi kabisa hii ina maana kwamba, "UKIMFAHAMU" tu adui yako, unakua umeshinda 50% ya vita unayoenda kuipigana. Kwanini?

Kwasababu kumjua adui yako ni kufahamu mambo kama mbinu zake za kivita (je ni bora kuliko zako?), kufahamu ubora wa silaha anazotumia (je ni za kisasa kuliko zako?) n.k

Hivyo unapokwenda kupambana unakua unafahamu uanzie wapi na uishie wapi

Ukienda kupigana kwa kukadiria tu uwezo za mpinzani wako, mara nyingi utashindwa! Na ndio mana wataalam wakasema "Do not under-estimate the power of your enemy"

Sasa tuje ARUSHA, ni kweli kuna machafuko

Lakini hatujawa na uhakika kwamba ni nani hasa ni adui yetu, tuko dillema...kuna wanaoitaja CCM, wengine CDM, wengine wanayataja Mataifa ya Nje kama ndio maadui zetu

Hebu tuwe watulivu, tukishamfahamu adui ndio tujue ni vp tutakabiliana nae, tusiendeshwe na hisia/itikadi, kwasababu mfuasi wa CCM ataishutumu CDM, halikadhalika na mfuasi wa CDM ataikashifu CCM, ktk mazingira kama haya, kama adui ni Mataifa ya Nje, tayari anakua ametugawanya (divide and rule) na itakua rahisi kutumaliza kabisa!

Usijifanye mjuaji kwa kupost matusi humu, wa CCM unawatukana CDM na wa CDM unawatukana CCM, hakuna tuzo ya mfuasi bora wa chama, wala kuonyesha hisia zako hakutasaidia chochote ktk kurejesha amani Arusha...hata kama unapata coments na like nyingi, usivimbe kichwa ukajiona maarufu sana humu JF kwa kuwa na wafuasi wengi...kumbuka

HITLER alikua na wafuasi zaidi ya milioni na YESU alikua na wafuasi 12 tu, lkn YESU ni maarufu kuliko huyo HITLER ambaye kashaoza kaburini.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tz, Mungu ibariki Arusha!
 
Nilitegemea kupata kitu zaidi ya ulichoandika kwenye post hii!!! Nilitegemea utatupatia clue ya yanayotokea arusha,sijaona chochote!Heading nzito lakini ndani hakuna kitu,hongera kwa kuuteka muda wangu kuupitia uzi wako.
 
Adui wa Tanzania tunamjua ni mmoja tu CCM. Hao kina Ujinga, Maradhi, Umaskini na Ufisadi ni matunda ya kazi ya CCM.

So mleta mada usijaribu kuleta usingizi kwenye mada kwa ku-balance mambo. CCM na CHADEMA wapi na wapi? CCM peke yao ndio waleta machafuko sio Arusha tu bali nchini na hata nje ya Tanzania. Unafiki pembeni.
 
Ccm wamekamatwa wanaanza kuleta upembuzi yakinifu. Ni jana tu mkuu wa usalama wa mkoa, RC amewapiga watu mabomu wasitoe heshima zao za mwisho. Leo hii unakuja na ujinga wako humu ndani. Kwanini msitumie akili zenu wakati wote?

Get a life!
 
***MTAZAMO WANGU JUU YA MACHAFUKO JIJINI ARUSHA***

Martin Luther King aliwahi kusema...

"To know the enemy is half the victory"; yaani "Kumfahamu adui ni nusu ya kushinda vita"

Kwahiyo kwa lugha nyepesi kabisa hii ina maana kwamba, "UKIMFAHAMU" tu adui yako, unakua umeshinda 50% ya vita unayoenda kuipigana. Kwanini?

Kwasababu kumjua adui yako ni kufahamu mambo kama mbinu zake za kivita (je ni bora kuliko zako?), kufahamu ubora wa silaha anazotumia (je ni za kisasa kuliko zako?) n.k

Hivyo unapokwenda kupambana unakua unafahamu uanzie wapi na uishie wapi

Ukienda kupigana kwa kukadiria tu uwezo za mpinzani wako, mara nyingi utashindwa! Na ndio mana wataalam wakasema "Do not under-estimate the power of your enemy"

Sasa tuje ARUSHA, ni kweli kuna machafuko

Lakini hatujawa na uhakika kwamba ni nani hasa ni adui yetu, tuko dillema...kuna wanaoitaja CCM, wengine CDM, wengine wanayataja Mataifa ya Nje kama ndio maadui zetu

Hebu tuwe watulivu, tukishamfahamu adui ndio tujue ni vp tutakabiliana nae, tusiendeshwe na hisia/itikadi, kwasababu mfuasi wa CCM ataishutumu CDM, halikadhalika na mfuasi wa CDM ataikashifu CCM, ktk mazingira kama haya, kama adui ni Mataifa ya Nje, tayari anakua ametugawanya (divide and rule) na itakua rahisi kutumaliza kabisa!

Usijifanye mjuaji kwa kupost matusi humu, wa CCM unawatukana CDM na wa CDM unawatukana CCM, hakuna tuzo ya mfuasi bora wa chama, wala kuonyesha hisia zako hakutasaidia chochote ktk kurejesha amani Arusha...hata kama unapata coments na like nyingi, usivimbe kichwa ukajiona maarufu sana humu fb kwa kuwa na wafuasi wengi...kumbuka

HITLER alikua na wafuasi zaidi ya milioni na YESU alikua na wafuasi 12 tu, lkn YESU ni maarufu kuliko huyo HITLER ambaye kashaoza kaburini.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tz, Mungu ibariki Arusha!

umeongea point nilitaka nikugongee like but umeniuzi hapo penye nyekundu!
 
Siajona unamaanisha nini. Tatizo ukisema ukweli kuhusu mwenzako unaonekana unatukana
 
umeongea point nilitaka nikugongee like but umeniuzi hapo penye nyekundu!

Ni kweli kuna hitilafu kdg mkuu, imetokea hivyo kwasababu nilipost haya mawazo yangu kwenye mitandao kadhaa ya kijamii, so ili kuepuka kutype tena nikawa na-copy na ku-paste

All in all, that mistake is curable kwasababu haiathiri msg niliyokusudia kui-deliver
 
umeongea point nilitaka nikugongee like but umeniuzi hapo penye nyekundu!

DSC_0000009_2.jpg hakuna njia nyingine zaid ya sis wananchi wote kwa ujumla pamoja na dini zetu tunyooshe vichwa juu na kumlili mwenyezi Mungu atupe msaada watanzania.........lol
 
Adui wa Tanzania tunamjua ni mmoja tu CCM. Hao kina Ujinga, Maradhi, Umaskini na Ufisadi ni matunda ya kazi ya CCM.

So mleta mada usijaribu kuleta usingizi kwenye mada kwa ku-balance mambo. CCM na CHADEMA wapi na wapi? CCM peke yao ndio waleta machafuko sio Arusha tu bali nchini na hata nje ya Tanzania. Unafiki pembeni.

kweli we mwezi mchanga
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom