SoC01 Nini kifanyike kuchochea madadiliko kwenye nyanja za uchumi na biashara?

Stories of Change - 2021 Competition

Ak47al

New Member
Jul 13, 2021
1
1
Habari wana JamiiForums?

Bila shaka sekta na taasisi mbalimbali zimekumbana na mabadiliko makubwa na ni bila kuficha ni kwamba sio nchi yetu tu ila dunia nzima inapitia wakati mgumu tangu kuibuka kwa ugonjwa mpya wa uviko 19(COVID 19). Hakuna ambaye alijiandaa na mabadiliko haya ya kasi sana na ambayo kwa namna moja au nyingine hayakutegemewa lakini moja ya sekta ambayo kwa asilimia kubwa imeathiriwa ni sekta ya UCHUMI NA BIASHARA. Karibu ungana na mimi nikushirikishe kwa ufupi zaidi na kwa maoni yangu nini kifanyike kuleta mabadiliko kwenye nyanja hii.

IMG_1520.jpg


1.MAZINGIRA YA UWEKEZAJI YABORESHWE
Uwekezaji ni moja ya kitu chachu na muhimu sana katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi na biashara, nchi nyingi hasa za dunia ya tatu na zinazo kua kiuchumi zinategemea uwekezaji kwa namna moja au nyingine kuendeleza sekta hii. Tukisema mazingira ya uwekezaji yaboreshwe tunajumuisha pamoja na miundombinu inayozunguka masoko, viwanda na biashara kwa ujumla, miundombinu inapoboreshwa inavutia ata wawekezaji wanao taka kuwekeza kwenye biashara na viwanda husika, tathimini ya uboreshaji wa miundombinu ya masoko iwekwe.

Sheria zinazowakandamiza wawekezaji ziboreshwe, wawekezaji wapewe fursa kutoa maoni mbalimbali yatakayoweza kuvutia wawekezaji wengine kwa namna moja au nyingine. Kituo cha uwekezaji Tanzania TIC( Tanzania Investment center ) iendelee kupendekeza sera na mikakati ya kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini, kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo, kupanua wigo wa uwekezaji kwa kujikita zaidi kwenye maeneo ambayo nchi inaweza ikafanya vizuri zaidi kulinganisha na nchi nyingine, kuweka miundombinu thabiti ikiwa ni pamoja na barabara zinazopitika wakati wote, umeme na maji kwenye maeneo husika vipatikane mda wote. Kuondoa vizuizi mbalimbali na kutangaza nafasi na vivutio vya uwekezaji katika nchi mbalimbali

2.KUTOA ELIMU KWA WATU MBALIMBALI KUHUSU MAENDELEO NA FURSA ZA MASOKO ZILIZOPO NDANI NA NJE YA NCHI.
Kwa muda mrefu sana watanzania tumekuwa nyuma kwenye hili ni asilimia chache sana za watanzania wenye elimu ya kutosha kuhusu fursa zilizopo ndani na nje ya nchi kwa ujumla. Wadau mbalimbali wapewe elimu kuhusu maendeleo na fursa za masoko zilizopo ndani na nje ya nchi hii itasaidia kupata taarifa mbalimbali za mabadiliko ya kibiashara na teknologia kwa ujumla, kubuni njia tofauti za ufanyaji wa biashara ili kuendana na wakati hasa kipindi hiki cha mripuko wa ugonjwa wa uviko 19. Mfano mzuri ni biashara za mtandaoni ambazo kwa takwimu za United Nations Conference on Trade and Development (UNCTAD) biashara za mtandaoni zimeongezeka takribani asilimia 6 hadi 10 hasa kwenye kipindi hiki cha uviko 19.

a40ee57a-aaf2-4648-838a-3a67398b1c2a.jpg


Mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania (TANTRADE) iendelee kuhamasisha biashara ya nje kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na maonyesho ya bishara ndani na nje ya nchi mfano ni maonyesho ya Kimataifa ya Sabasaba na maonyesho yaliyofanyika jijini Beijing nchini china yalikuwa maonyesho ya kwanza ya biashara na uchumi kati ya China na Afrika mnamo mwaka 2019 na maonyesho ya Syrian ambayo hufanyika pia.

3.KUKUZA SOKO LA NDANI YA NCHI
Kukuza soko la ndani ya nchi ni lazima kuviwezesha viwanda vidogo vidogo na viwanda vya kati vikue na kufanya kazi kwa tija zaidi, utoaji wa mikopo kwenye viwanda ivi utasaidia katika ukuaji wa biashara za viwanda husika. Viwanda kama vya usindikaji wa vyakula na ngozi viendelezwe pamoja na viwanda vilivyo kufa viinuliwe tena upya. Bidhaa zinazotengenezwa ndani ya nchi zipewe kipaumbele katika biashara za matangazo nje na ndani ya nchi. Kubadili matumizi ya teknologia kutoka matumizi ya mikono mpaka mashine za kisasa kwenye viwanda vya ndani. Viwanda vingi vijishughulishe na uchakataji wa mazao ya kilimo, misitu na mifugo ili viweze kuzalisha bidhaa kama sigara, katani, mafuta ya kula, mbao na bidhaa zote za ngozi.

Mfano wa ngozi kabla na baada ya utengenezaji na bidhaa zinazo zalishwa

cbed9ed6-2cf9-42ba-bafb-f24151fdae16.jpg

f3e0296b-6055-4d0c-922d-08582d9e8018.jpg

Chanzo cha picha nukta habari


Pia uendelezaji wa wa miradi mipya kwa mfano mradi wa gesi wa songo songo Lindi na mradi wa makaa ya mawe ya mchuchuma na chuma cha liganga kwa ajili ya kukuza pato la taifa kwa ujumla.

4.KUBUNI MIKAKATI YA KUENDELEZA SEKTA ZA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO
Mikakati iandaliwe kwa ajili ya kuendeleza sekta ya viwanda ili kuinua viwanda vilivyo kufa. Wafanya biashara kupewa elimu ya masoko itakayo wawezesha kujua na kutambua mabadiliko mbalimbali ya masoko duniani. Mikakati iwekwe kwenye sekta husika ili kuhakikisha viwanda na wafanya biashara wanatumia mashine za kisasa zitakazo ongeza uzalishaji na kupelekea mabadiliko kwenye sekta husika. Kituo kama cha Tanzania Trade centre London ambacho kilianzishwa mwaka 1989 kwa lengo la kukuza mahusiano ya kiuchumi kati ya Tanzania na Uingereza na pia nchi jirani za bara la Ulaya na nje ya bara la ulaya kizidi kukuzwa ili kuvutia wawekezaji mbalimbali hasa wa kigeni, kukuza diplomasia ya uchumi, utalii na kupata taarifa na huduma za biashara kutoka nchi mbalimbali.

5. UBUNIFU, UENEZAJI NA UTUMIAJI WA TEKNOLOGIA INAYOFAA
Nchi nyingi zinazoendelea hasa barabi Afrika na Ulaya kwa ujumla zimekuwa zikibadilika kutokana na mabadiliko ya matumizi ya teknologia hususani kipindi hiki cha uviko 19. Ili kuleta ushindani mkubwa duniani ubunifu unahitajika sana katika ufanyaji wa maendeleo mbalimbali, wadau hasa wa biashara wanabidi wabadilike katika matumizi ya teknologia kwenye swala zima la kuendesha biashara na viwanda vyao husika kwa uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.

Ubunifu utasaidia katika kuboresha bidhaa husika lakini pia utumiaji wa mashine mpya na za kisasa utasaidia kuzalisha bidhaa zenye viwango vya ubora duniani na kwa asilimia kubwa. Shirika la utafiti na maendeleo ya viwanda (TIRDO) liendelee kutoa utafiti, ushauri mbalimbali wa teknologia za viwanda katika sekta husika lengo ni kuendeleza viwanda na kuongeza uzalishaji ambao utapelekea mabadiliko ya kiuchumi kwa namna fulani. Mfano mzuri ni kiwanda cha kukoboa mpunga jijini Mwanza kinacho jengwa chini ya usimamizi wa TIRDO kiwanda hiki kitakuwa na uwezo wa kuzalisha hadi tani 96 kwa siku.

2669d67b-49aa-4940-b7de-af2cb7429420.jpg

Pichani ni kiwanda icho kikiwa hatua za usimikaji wa mashine mpya za kisasa
Chanzo cha picha Tirdo via instagram

aa858745-2606-4511-95a4-7058a3d9b1e5.jpg

Baadhi ya mashine izo mpya
Chanzo cha picha itv Facebook

Kuna njia nyngi sana zinaweza kwa namna moja au nyingine kuchangia mabadiliko kwenye sekta ya UCHUMI NA BIASHARA kikubwa kwetu sisi watanzania kila mmoja wetu awe tayari kupigania mawazo yake na kutokata tamaa kwenye chochote unachofanya kama unajua kitakutoa sehemu moja kukupeleka sehemu nyingine kiuchumi pia kutumia fursa mbalimbali za biashara zinazo jitokeza mara kwa mara pia kuachana na utamaduni wa kwamba kila biashara inahitaji mtaji mkubwa sana ila kwa biashara yako ndogo tu ukifanya kwa malengo itakuletea mafanikio makubwa sana.
 
Back
Top Bottom