Nini kifanyike ili wananchi wajue hatima yao ni ipi?

mtu watu

JF-Expert Member
Dec 10, 2017
2,113
2,000
Kumekuwa na sitofahamu juu ya mwenendo wa wananchi wa mwanza maeneo ya buhongwa kuzuiliwa na kusimamisha kuanzisha makazi yao kwa maeneo husika kisa eneo ilo linatakiwa na Jeshi la wananchi wa Tanzania (jwtz) kwa ajili ya kufunga Rada.

Ili suala limechukua muda mrefu sana mpaka ikapelekea wakazi wa eneo husika kusitisha ujenzi wao ambao ulikuwa ukiendlea huku wakisubiri muafaka wa jeshi ambapo mpaka sasa imekuwa kizungumkuti, wananchi wamekaa huku wakisubiri fidia mpaka sasa kimya.

Wananchi wa eneo husika wamepeleka lalamiko mpaka kwa mkuu wa mkoa wa mwanza ila suala ili limekuwa ni kupigwa kalenda tu.

Naandika haya kwa kuwa ni lalamiko linaloendlea mpaka sasa tangu mwak jana hawajui hatma yao ni ipi?

Je serikali ili suala inalifikiriaje mpaka sasa?

Je ni lini wananchi wa eneo husika watapatiwa fidia zao na kuhamisha makazi yao sehemu nyingne!?

Je serikali ya Mwanza na mkuu wa mkoa ameshindwa kutoa msaada ili jambo liweze kutimia?

Kwa nini hawatoi muda muafaka ni lini watatimiza wajibu huo?

Mkuu wa mkoa wa mwanza wananchi wako wanahitaji nguvu yako uweze kuwaunga mkono waweze kupata haki yako ili watafte maeneo mengine ya kuanzisha makazi yao.

Kama hakuna uhakika wa kulipwa fidia basi hawana budi kuendleza ujenzi wao kama awali!

Pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania simamia suala ili mapema ili wananchi wako watambue ya kuwa wanaye kiongozi wa wanyonge!

Nawasilisha!

wakati ukuta.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom