Nini kifanyike ili reli ya Kaskazini isife kama ilivyokufa mwanzo?

Kikusya

JF-Expert Member
Oct 2, 2011
266
365
Mimi sijui kwa nini ile reli yetu ya kaskazini ilikufa na tufanyeje ili hii iliyofufuliwa isife kamwe? Tumejifunza mengi sana kwa hayati John Magufuli, na Mungu amuweke mahala pema peponi. Mimi nahamini kila binadamu ataenda peponi na hilo ndiyo kusudio la Muumba wetu.

Je kuna nini cha kujifunza kuhusu reli hii? Wangekuwa wenzetu wa Ulaya hii reli kwa sasa ingekuwa ya umeme na usafiri wa uhakika. Tunakosea wapi? Ukiachia mbali shirika letu la ndege lililovyokuwa hoi na sasa linafufuka .

Tafadhari sana tena sana wengine tunajisikia uchungu sana kwa kuona vitu vingi vizuri vinavyoanzishwa na serikali kutotunzwa , kufilisika na vingine kufa kabisa.
JE SABABU NI ZIPI? NA TUFANYEJE KAMA WAPENDA MAENDELEO? KUMBUKA TANZANIA NI YETU NA LAZIMA TUIJENGE, TUIENDELEZE, TUILINDE NA TUIPENDE KWA MOYO WOTE.

Je, ni usimamizi mbovu wa utawala?
Je ni kutokuwa waaminifu kwa mali ya umma?
Je ni uzembe na wizi wa baadhi ya wafanyakazi? n.k

Je adhabu gani serikali itoe kwa wale wanaohusika na hujuma, wizi , hasara , uzembe, au kuendesha haya mashirika na taasisi bila kupata faida?
Kwa sababu bila kupata faida na mikakati mizuri ya kuona mbele, hivi vyote vitakufa tena, na tutaanza kufufua tena. Tutakuwa taifa la kufufua tu, hatujui kuendeleza na kufikia viwango vya juu.

Naomba kama wewe huna la kuchangia n i tufanye taifa liende mbele ni bora usome tu au ikibidi jifanye unajikuna na sisi tutakuelewa tu. Ahsante wandugu.
 
Niko siti ya mbele kbsa Kwan mm pia natokea kazkazin mwa taifa hili

Ni kweli Ni muhimu San Sana kwa ukanda huo ukizingatia kuwa watu Ni wengi sna wenye kufanya usafir Kat ya dar na kazkanzi ..
Ingefah Zaid sgr ingeanza huku
 
Niko siti ya mbele kbsa Kwan mm pia natokea kazkazin mwa taifa hili

Ni kweli Ni muhimu San Sana kwa ukanda huo ukizingatia kuwa watu Ni wengi sna wenye kufanya usafir Kat ya dar na kazkanzi ..
Ingefah Zaid sgr ingeanza huku
Sawa kabisa, mimi natokea kanda za juu kusini lakini sina wivu wa kuendeleza sehemu yoyote Tanzania. Kinachoniuma nikuona miradi inakufa au kuliwa bila huruma.
 
Mifumo ya nchi inatakiwa kubadilishwa.
Serikali za majimbo itainua uchumi wetu kwa haraka sana.
 
Sikuizi kuna kaneno kamekuwa maarufu toka JKwete alivyokitaja kwenye msiba wa mwendazake. LEGACY kila raisi ana legacy yake akiondoka anaekuja anaitupa ya mtangulizi.

ubinafsi wa maraisi ndo changamoto. kilimo kwanza. serekali ya viwanda. huyuu sijui atakuja na nini. wote wanafanya nusu nusu bila kumalizika. anaechukua kijiti anapiga tege. kama uwanja wa chato,mbuga NK 错vyote hivyoo vitapigwa teke.

na huyuu ataanzisha vyake atafika nusu mwenzake akija ni teke.


asilimia 85 taifa liwe na vipaumbele vyake hiyoo 15 iliyobaki tuwaachie wanasiasa.
 
Back
Top Bottom