Nini kifanyike ili media na social media zihabarishe umma kuhusu uwajibikaji na kujitambua badala ya kutoa habari kiburudani?

sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
3,021
5,253
Kwenye Forum Meeting inayojadili uwajibikaji kutoka ripoti ya CAG, JF imeulizwa na taasisi ya WAJIBU, kuwa Nini kifanyike kuhusu media na social medias kuhusu kuhabarisha umma juu ya uwajibikaji na kujitambua.

Msingi wa swali ni kwa kuwa uchambuzi wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuripotiwa na vyombo vya habari katika mfumo wa burudani au vichekesho, je kifanyike nini ili media zitoe taarifa katika namna ya kuwaeleza wananchi wajibu wao ama kuonesha uwajibikaji kwa viongozi. JF imewakilishwa na Bw. Francis Nyonzo.

IMG_2023-04-28-09-29-43-670.jpg

Mzungumzaji mmoja wa MEDIA anasema kuwa Tanzania kuna wanahabari wengi au wote ni wanahabari lakini tuna waandishi wa habari wachache sana.

Wengi ni wanahabari wanaovizia matukio ili watrend lakini hakuna waandishi wa habari ambao wanafanya uandishi wa kina na consistency.

Mfano, mwanahabari anaripoti kuwa Hela zimepigwa lakini hajui chochote kuhusu bajeti ilivyoandaliwa kabla ya huo upigaji nk. Sasa hawa ni wanahabari na sio waandishi wa habari
 
Kama taifa tuna tatizo kubwa la ujinga karibu katika kila sekta. Si wanafunzi, wasomi, vyama vya siasa, wanaharakati, nk yaani wote maji ga nyanja -- akisema JKN.

Uzi huu hapa unaiangazia hali yetu hohe hahe kama ilivyo:

Watanzania wajinga na kuvuna wanayopanda

Hebu ishuke mada yenye mwelekeo wa ngono uone kulivyokuwa na hamasa. Si wanaume si wanawake. Jamii imegubikwa na vijana wa hovyo kwenye kila kona.

Subiri uone wenye stamina hata ya kutia neno hapa. Staajabu ya Mussa ndugu yangu.

Nini kifanyike:

Ninadhani vyama vya siasa vinakosa watu sahihi kuihamasisha na kuiamsha jamii vilivyo. Ninadhani wanakosekana kina Lissu, Maalim Seif, Mtikila na wa namna hiyo kwenye nafasi sahihi.

Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu

Tuipiganie demokrasia kamili kwenye vyama hivi kuwapata viongozi wenye kudhamiria kama hawa.

Ninadhani wapigania haki wa dhati wanapaswa kuchukua nafasi zao kuihamasisha jamii ya wanaobakia, vilivyo.

Prof. Shivji na maoni yake kuhusu kadhia ya Law School

Watanzania tumekuwa zaidi ya makondoo kutofahamu Hata upana wa mlango.

FutD12pWIAEjDDU.jpeg

Wako wapi wanafunzi au graduates wa vyuo vikuu humu JF? Tunajaribu kuwapigania LST, wenyewe wako wapi? Au kwenye magroup yao ya Whatsapp? Au ndiyo hawa kina Leaky, Paskali Yonda, carina, Ujamaa ni muhimu na wa namna hiyo?

Wako wapi wanachama wa vyama vya siasa? Au waliopo ndiyo hawa waliopikwa na kuiva hivi?

Kuna Radio fulani inachambua habari za michezo kuanzia saa 3 Hadi saa 6 mchana then saa moja Hadi saa 3 usiku. Yaan kwa siku hutumia masaa matano kwa ajili ya habari za michezo tu.
 
Kama taifa tuna tatizo kubwa la ujinga karibu katika kila sekta. Si wanafunzi, wasomi, vyama vya siasa, wanaharakati, nk yaani wote maji ga nyanja -- akisema JKN.

Uzi huu hapa unaiangazia hali yetu hohe hahe kama ilivyo:

Watanzania wajinga na kuvuna wanayopanda

Hebu ishuke mada yenye mwelekeo wa ngono uone kulivyokuwa na hamasa. Si wanaume si wanawake. Jamii imegubikwa na vijana wa hovyo kwenye kila kona.

Subiri uone wenye stamina hata ya kutia neno hapa. Staajabu ya Mussa ndugu yangu.

Nini kifanyike:

Ninadhani vyama vya siasa vinakosa watu sahihi kuihamasisha na kuiamsha jamii vilivyo. Ninadhani wanakosekana kina Lissu, Maalim Seif, Mtikila na wa namna hiyo kwenye nafasi sahihi.

Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu

Tuipiganie demokrasia kamili kwenye vyama hivi kuwapata viongozi wenye kudhamiria kama hawa.

Ninadhani wapigania haki wa dhati wanapaswa kuchukua nafasi zao kuihamasisha jamii ya wanaobakia vilivyo.

Prof. Shivji na maoni yake kuhusu kadhia ya Law School

Watanzania tumekuwa zaidi ya makondoo.

View attachment 2602141

Wako wapi wanafunzi au graduates wa vyuo vikuu humu JF? Tunajaribu kuwapigania LST wenyewe wako wapi? Kwenye magroup yao ya Whatsapp? Au ndiyo hawa kina Leaky, Paskali Yonda, carina, Ujamaa ni muhimu na wa namna hiyo?

Wako wapi wanachama wa vyama vya siasa? Au waliopo ndiyo hawa waliopikwa na kuiva hivi?

View attachment 2602138
Wewe Leo ni siku ya KAZI asubuhi tuuu unapoteza mda kuandika status za watu waliokwisha tangulia mbele za haki unawatakia Nini? Kama unataka mbadla wa hao tupo sisi ndio maana unaona nchi na uchumi unaendelea, usalama na amanii vinaimalika Hadi wewe unapata mda wa kutoa maoni yako.
 
Kuna Radio fulani inachambua habari za michezo kuanzia saa 3 Hadi saa 6 mchana then saa moja Hadi saa 3 usiku. Yaan kwa siku hutumia masaa matano kwa ajili ya habari za michezo tu.
Watumiaji wanataka nini, wateja wanapenda ugali wewe utapika makande?
 
Media sahv wao ni kuchambua habari za michezo na mambonya umbea wa kina mondi, konde kajala nk

Ova
 
Issue ni watawala wanalipankwaajilinyankuhakikisha kinachosikika hakileti madhara kwa wanachokifanya kwa maana ya ufisadi nk. Hivyo hao wachambuzi wanalipwa mishara na pesa inayokuja na maelekezo ya nini kisemwe na kip kisipewe uzito kwahyo kufupisha ni kwamba huwezi kupataa uchambuzi au maswali yenye tija ya kujenga ilihali wanaoweza kusikika kwa niaba ya wengi ni wanufaika wa ufisadi huo.
 
Mada iko wazi nini kifanyike kubadili hali hiyo? Kunategemewa mwongozo wako ndugu mjumbe.
 
Mfumo wa utawala ubadilike kiongozi kwa maana ya mkuu wa nchi anavitu ving sana ambavyo yeye ndo mwamuzi wa mwisho kwahyo inatengeneza mazingira ya kuogopana kwasababu yeye ndo anaamua nani awe nani kwa wakati gani kwahyo ni mfumo kusema kwweli hautupi nafasi ya kuhoji juu ya nini kinafanyika kwa kuogopa kukosa teuzi au kutenguliwa kwenye nafasi zetu tulizonazo aisee naomba niishie hapa mkui
 
Tatizo letu liko pande mbili.

- Ni upande wa media, siku hizi tumekuwa na wanahabari wenye njaa wanaofanya kazi kwa kutazama namna ya kuufurahisha upande fulani ili mwisho wa siku wakumbukwe mkono uende kinywani, hawa wanahabari wamegeuka.chawa hivyo usipoteze muda wako kuwasubiri wakupe habari za maana kwa kina.

- Serikali yenyewe, hii ilishajijengea dhana ionekane ina nguvu mbele ya jamii, ndio inaamua habari gani ziende kwa wasikilizaji na wasomaji, hivyo kama kuna habari inayoonekana itakuwa mwiba kwa serikali mfano ripoti ya CAG itakayowaamsha wanachi wadai Pesa zao wanazoibiwa kila siku, usitegemee media itaachwa huru kuuhabarisha umma.

Mfano wa hili ni lile suala la kukopa hovyo, Hando akashughulikiwa na kituo chake cha EFM kwa maelezo toka juu, siku alipokwenda Msoga kwenye tamasha la kuukaribisha mwaka mpya lililoandaliwa na Kikwete, Majizzo ambae ni mmiliki wa EFM, akapongezwa na Kikwete kwa uamuzi wa kumshughulikia Hando alie laani kukopa hovyo.

Kuhusu nini kifanyike, naona kwanza serikali inatakiwa iwaachie wadau wa habari wafanye mambo yao kwa uhuru, pawepo na sheria zitakazowahakikishia wadau wa habari kutimiza majukumu yao kwa weledi na uhuru bila uoga wa kuogopa mkono wa serikali, lakini pia kama kuna sheria zozote zinazowakandamiza wanahabari kwa sasa, zifutwe.
 
Kwenye Forum Meeting inayojadili uwajibikaji kutoka ripoti ya CAG, JF imeulizwa na taasisi ya WAJIBU, kuwa Nini kifanyike kuhusu media na social medias kuhusu kuhabarisha umma juu ya uwajibikaji na kujitambua.

Msingi wa swali ni kwa kuwa uchambuzi wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuripotiwa na vyombo vya habari katika mfumo wa burudani au vichekesho, je kifanyike nini ili media zitoe taarifa katika namna ya kuwaeleza wananchi wajibu wao ama kuonesha uwajibikaji kwa viongozi. JF imewakilishwa na Bw. Francis Nyonzo.

Mzungumzaji mmoja wa MEDIA anasema kuwa Tanzania kuna wanahabari wengi au wote ni wanahabari lakini tuna waandishi wa habari wachache sana.

Wengi ni wanahabari wanaovizia matukio ili watrend lakini hakuna waandishi wa habari ambao wanafanya uandishi wa kina na consistency.

Mfano, mwanahabari anaripoti kuwa Hela zimepigwa lakini hajui chochote kuhusu bajeti ilivyoandaliwa kabla ya huo upigaji nk. Sasa hawa ni wanahabari na sio waandishi wa habari
Habari za kuhabarisha na za maana watanzania wengi hawazisomi sio kwamba hakuna media zinatoa hizo habari ila wanaotembelea hizo media ni wachache kuliko wanaotembelea kula tunda kimasihara
 
Back
Top Bottom