Wanabodi wenzangu binafsi nimetafakari sana utaratibu ambao umekuwa unatumika wa kuandikisha wapiga kura kila uchaguzi unapokaribia na kujiuliza je huu utaratibu ndo mzuri kuliko njia nyinginezo.
Katika kutafakari nimeona huu utaratibu wa kujiandikisha kila tunapofanya uchaguzi siyo utaratibu mzuri kwakuwa kwanza unasababisha watu wengi washindwe kupiga kura kwasababu ya kuwa mbali na vituo walivyojiandikisha. Mfano wanafunzi wa vyuo vikuu na wafanya biashara wa ndani ambao wanalazimika kusafiri mara kwa mara.
Sababu nyingine ni usumbufu usio walazima kwa wananchi ambao wangeweza kwenda mara moja tu siku ya kupiga kura kama wanatambulika. Hali hii inadhihirishwa na mwitikio hafifu sana wa watu kujiandikisha kwa ajiri ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika mwezi Novemba, 2019,
Kwakuwa kuna zoezi linaloendelea la kuwapatia Vitambulisho vya taifa watanzania wote waliofikia umri wa miaka 18 na kuemdelea, sheria yetu ya uchaguzi ifanyiwe marekebisho na kutambua Kitambulisho cha taifa kuwa ndicho kitumike kwenye chaguzi zote hivyo kusiwe na haja ya kuandikisha wapiga kura badala yake wenye Vitambulisho vya taifa waruhusiwe kupiga kura.
Endapo kutakuwa na baadhi ya watanzania ambao hawajapata vitambulisho basi waruhusiwe kutumia namba za Vitambulisho zinazotolewa na NIDA. Hata hivyo kwakuwa zoezi la kuwapatia vitambulisho vya taifa limekuwa la kusuasua serikali isimamie zoezi hilo ili liweze kukamilika haraka ili watu wote waweze kupatiwa Vitambulisho vya taifa.
Utaratibu huu utapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi yasiyo ya lazima ya kuandikisha wapiga kura wakati inaeleweka kwamba kila raia aliyefikisha miaka 18 na kuendelea ana sifa ya kupiga kura.
Hivyo wakati wa kupiga kura mfumo wa NIDA uunganishwe na mfumo wa Tume ya Uchaguzi ili iwe rahisi kusoma vitambusho vya wapiga kura kabla ya kuruhusiwa kupiga kura ili kuhakikishakuwa anayepiga kura ni raia mwenye kitambulisho cha kitambulisho cha taifa kilichotolewa na NIDA.
Naomba kutoa hoja.