NINI KIFANYIKE ILI KURAHISISHA ZOEZI LA MAANDALIZI YA KUPIGA KURA NCHINI.

mhanila1

JF-Expert Member
Dec 15, 2017
1,030
2,000
Wanabodi wenzangu binafsi nimetafakari sana utaratibu ambao umekuwa unatumika wa kuandikisha wapiga kura kila uchaguzi unapokaribia na kujiuliza je huu utaratibu ndo mzuri kuliko njia nyinginezo.

Katika kutafakari nimeona huu utaratibu wa kujiandikisha kila tunapofanya uchaguzi siyo utaratibu mzuri kwakuwa kwanza unasababisha watu wengi washindwe kupiga kura kwasababu ya kuwa mbali na vituo walivyojiandikisha. Mfano wanafunzi wa vyuo vikuu na wafanya biashara wa ndani ambao wanalazimika kusafiri mara kwa mara.

Sababu nyingine ni usumbufu usio walazima kwa wananchi ambao wangeweza kwenda mara moja tu siku ya kupiga kura kama wanatambulika. Hali hii inadhihirishwa na mwitikio hafifu sana wa watu kujiandikisha kwa ajiri ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika mwezi Novemba, 2019,

Kwakuwa kuna zoezi linaloendelea la kuwapatia Vitambulisho vya taifa watanzania wote waliofikia umri wa miaka 18 na kuemdelea, sheria yetu ya uchaguzi ifanyiwe marekebisho na kutambua Kitambulisho cha taifa kuwa ndicho kitumike kwenye chaguzi zote hivyo kusiwe na haja ya kuandikisha wapiga kura badala yake wenye Vitambulisho vya taifa waruhusiwe kupiga kura.

Endapo kutakuwa na baadhi ya watanzania ambao hawajapata vitambulisho basi waruhusiwe kutumia namba za Vitambulisho zinazotolewa na NIDA. Hata hivyo kwakuwa zoezi la kuwapatia vitambulisho vya taifa limekuwa la kusuasua serikali isimamie zoezi hilo ili liweze kukamilika haraka ili watu wote waweze kupatiwa Vitambulisho vya taifa.

Utaratibu huu utapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi yasiyo ya lazima ya kuandikisha wapiga kura wakati inaeleweka kwamba kila raia aliyefikisha miaka 18 na kuendelea ana sifa ya kupiga kura.

Hivyo wakati wa kupiga kura mfumo wa NIDA uunganishwe na mfumo wa Tume ya Uchaguzi ili iwe rahisi kusoma vitambusho vya wapiga kura kabla ya kuruhusiwa kupiga kura ili kuhakikishakuwa anayepiga kura ni raia mwenye kitambulisho cha kitambulisho cha taifa kilichotolewa na NIDA.

Naomba kutoa hoja.
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
172,416
2,000
KWA NINI WANANCHI HAWATAKI KUJIANDIKISHA?

Na Thadei Ole Mushi.

Mawazo yangu binafsi!!

Mwaka Jana mwezi wa kumi Katibu mkuu ccm Dr Bashiru alilalamika wapiga kura kupungua kwenye chaguzi za marudio, Dr Bashiru alinukuliwa akisema wapiga kura wanaojitokeza kupiga kura walikuwa chini ya asilimia Hamsini ya waliojiandikisha.

Namuona Mh Jafo naye akiingia kwenye issue ile ile kuwa zoezi la kujiandikisha kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa nao unasua sua. Hapa ndipo watafiti wanapotakiwa kufanya utafiti kwa nn wananchi hawataki kushiriki uchaguzi?

Ninapredict factor NNE hapa.

1.Chaguzi za marudio za mradi wa jiuzulu, unga mkono, gombea tena, shinda kwa lazima ni factor mojawapo ya wananchi kuchoshwa na chaguzi. Wananchi wa naona hata wakipiga kura kuna watu wapo mahali wanamatokeo yao tayari.

2. Hakuna Elimu iliyotolewa ya kutosha kati ya uandikishaji wa daftri la kudumu kwa ajili ya uchaguzi mkuu 2020 na daftari hili la ukaazi kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa. Zoezi lilianza kabla ya Elimu hii ya kutofautisha kutolewa.

3. Mikutano ya vyama vya siasa kuwa na zuio za hapa na pale kumeshusha morali ya Demokrasia nchini. Mwanachama wa Chadema wa kawaida was Mbinga kwa miaka minne hajawahi kukutana na mwenyekuti wake wa chama kwenye mkutano. Mwenyekiti hana ruhusa ya kufanya mikutano akienda Mbinga atafanyia mikutano ndani na hapa atakutana tu na viongozi. Kwenye maandishi kikatiba tunatumia mfumo wa vyama vingi ila practically ni kimoja kinaoparete kwa mwavuli wa udola na kukagua utekelezaji wa ilani.

4. Vijana ndio chachu ya chaguzi zote duniani.... Hakuna uhusiano wa moja kwa moja uliopo kati ya vijana wanaosaka ajira usiku na mchana na viongozi wa kuchaguliwa. Mwitikio wa vijana ni mdogo sana, angalia kwenye media utaligundua hili sana.

Tunakoelekea.

Pamoja na population yetu kuobgezeka idadi ya wapiga kura itazidi kupungua. Lazma tulifanyie kazi eneo hili.

Agizo la waziri.

Waziri Jafo amesema atapeleka dokezo kwa Mh Rais kwa mikoa ambayo uandikishaji utadorora ikiwezekana waadhibiwe. Mh Rais naye kashakubali kuwa atawashughulikia. Wakuu wa mikoa wataanza kuhaha kuomba watu wajiandikishe ili wasikutane na rungu la mh Rais.

Wanaweza kujiandikisha lakini je watapiga kura ? Hili ni eneo jingine.

Ole Mushi.
0712702602
 
JoJiPoJi

JF-Expert Member
Aug 8, 2009
2,891
2,000
Ubabe wa Kiongozi Mkuu Ndio Chanzo Cha Wananchi Kupuuzia Hilo Zoezi.
Na Huu Ni Mwanzo Tu, Uchaguzi Mkuu Ndio Hali Itakuwa Mbaya Zaidi.
 
nipekidogo

JF-Expert Member
Apr 17, 2019
1,594
1,980
Kama nimekuelewa hivi, na hii pia itapunguza wingi wa vitambulisho, ingawa swala la kuandikisha kila uchaguzi haliwezi kuepukika kwakuwa wkt huo kuna wanaokuwa wamefikisha miaka 18 inayowaruhusu kupiga kura so naungana na wewe kitambulisho cha NIDA ndio kitumike kupigia kura kwenye chaguzi zote mbili.
Na hii itasaidia wale wanaofikisha miaka 18 kutokusubili mpk uchaguzi inakuwa akifikisha umri wa miaka 18 anajiandikisha anapata ID ya NIDA inakuwa inatumika kupata huduma zote!
 
mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
29,281
2,000
Wasihangaike na uchaguzi bali wajitangaze wao ni washindi ili tubane matumizi.
 
ChizzoDrama

JF-Expert Member
Sep 29, 2019
1,248
2,000
KWA NINI WANANCHI HAWATAKI KUJIANDIKISHA?
Na Thadei Ole Mushi.
Mawazo yangu binafsi!!
Mwaka Jana mwezi wa kumi Katibu mkuu ccm Dr Bashiru alilalamika wapiga kura kupungua kwenye chaguzi za marudio, Dr Bashiru alinukuliwa akisema wapiga kura wanaojitokeza kupiga kura walikuwa chini ya asilimia Hamsini ya waliojiandikisha.
Namuona Mh Jafo naye akiingia kwenye issue ile ile kuwa zoezi la kujiandikisha kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa nao unasua sua. Hapa ndipo watafiti wanapotakiwa kufanya utafiti kwa nn wananchi hawataki kushiriki uchaguzi?
Ninapredict factor NNE hapa.
1.Chaguzi za marudio za mradi wa jiuzulu, unga mkono, gombea tena, shinda kwa lazima ni factor mojawapo ya wananchi kuchoshwa na chaguzi. Wananchi wa naona hata wakipiga kura kuna watu wapo mahali wanamatokeo yao tayari.
2. Hakuna Elimu iliyotolewa ya kutosha kati ya uandikishaji wa daftri la kudumu kwa ajili ya uchaguzi mkuu 2020 na daftari hili la ukaazi kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa. Zoezi lilianza kabla ya Elimu hii ya kutofautisha kutolewa.
3. Mikutano ya vyama vya siasa kuwa na zuio za hapa na pale kumeshusha morali ya Demokrasia nchini. Mwanachama wa Chadema wa kawaida was Mbinga kwa miaka minne hajawahi kukutana na mwenyekuti wake wa chama kwenye mkutano. Mwenyekiti hana ruhusa ya kufanya mikutano akienda Mbinga atafanyia mikutano ndani na hapa atakutana tu na viongozi. Kwenye maandishi kikatiba tunatumia mfumo wa vyama vingi ila practically ni kimoja kinaoparete kwa mwavuli wa udola na kukagua utekelezaji wa ilani.
4. Vijana ndio chachu ya chaguzi zote duniani.... Hakuna uhusiano wa moja kwa moja uliopo kati ya vijana wanaosaka ajira usiku na mchana na viongozi wa kuchaguliwa. Mwitikio wa vijana ni mdogo sana, angalia kwenye media utaligundua hili sana.
Tunakoelekea.
Pamoja na population yetu kuobgezeka idadi ya wapiga kura itazidi kupungua. Lazma tulifanyie kazi eneo hili.
Agizo la waziri.
Waziri Jafo amesema atapeleka dokezo kwa Mh Rais kwa mikoa ambayo uandikishaji utadorora ikiwezekana waadhibiwe. Mh Rais naye kashakubali kuwa atawashughulikia. Wakuu wa mikoa wataanza kuhaha kuomba watu wajiandikishe ili wasikutane na rungu la mh Rais.
Wanaweza kujiandikisha lakini je watapiga kura ? Hili ni eneo jingine.
Ole Mushi.
0712702602
hapo kwenye hoja ya pili nakataa mambo za elimu ya kujiandikisha sidhani Kama kuna MTU haijui ..sababu si zoezi geni limegeuka kuwa utamaduni.
Ni sawa na MTU aseme kafa kwa ugonjwa Wa ukimwi eti kwa kukosa elimu juu ya zinaa (ni uongo)
Jibu ni moja tu WANANCHI HAWATAKI
 
mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,544
2,000
Kwani huyo mkuu wa mkoa naye tunamchagua?? Kama akichapwa bakora au rungu inaniumiza nini?? Walitakiwa waanze siku nyingi kutoa elimu ya kujiandikisha. Sio unaamka asubuhi unasema nenda kajiandikishe la ka sivyo nitakushughulikia au nitamshughulikia mkuu wako wa mkoa. Nadhani hizi kauli zinawachajisha zaidi watu. Wapo walio tiyari kuuonja huo mtiti
 
Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
7,732
2,000
Wawalipe wananchi kama motisha, na wawafuate majumbani kuwaondolea usumbufu.
Ikibidi wateue hao wanaowataka kutawala serikali za mitaa.
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
9,650
2,000
Kitambulisho cha Taifa kilikuwa ni suluhu la hiyo milolongo yote! Kina sifa zote zinazostahili.Tatizo ni wanasiasa na watendaji serkkalini, wanaowaza kupiga tu hela za walipa kodi kupitia michakato lukuki! Hivyo kuwasusia hizo siasa zao, ni dawa tosha kabisa.
 
ChizzoDrama

JF-Expert Member
Sep 29, 2019
1,248
2,000
Kwani huyo mkuu wa mkoa naye tunamchagua?? Kama akichapwa bakora au rungu inaniumiza nini?? Walitakiwa waanze siku nyingi kutoa elimu ya kujiandikisha. Sio unaamka asubuhi unasema nenda kajiandikishe la ka sivyo nitakushughulikia au nitamshughulikia mkuu wako wa mkoa. Nadhani hizi kauli zinawachajisha zaidi watu. Wapo walio tiyari kuuonja huo mtiti
wananchi wafuatwe majumbani mbona wao tukiwachagua tuna wafuata ofisini ! KUTESA KWA ZAMU
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom