Nini kifanyike ili kiongozi asipendelee kwao kama Hayati Dkt. Magufuli alivyoipendelea Chato?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
14,924
2,000
Ni wazi kuwa rais Magufuli aliipendelea sana wilaya ya Chato katika kupeleka maendeleo. Alijenga uwanja wa ndege wa kimataifa, alijenga hospitali kubwa ya rufaa ya kanda, alijenga chuo cha Veta, alianza kujenga hoteli ya nyota tatu, mipango ya kujenga uwanja wa mpira. Na mambo mengine mengi sana.

Haya mambo hayakuanza na Rais Magufuli, ni vile tu yeye aliyafanya kwa kiwango cha kushangaza.

Sasa siku nyingine atatokea kiongozi atafanya zaidi ya Magufuli alivyofanya. Nini kifanyike ili kuzuia Rais au kiongozi yoyote asiweze kufanya kitu kama hicho?
 
thesym

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
3,525
2,000
Bunge lenye uwiano mzuri Kati ya upinzani na chama tawala linaweza punguza hili tatizo. Inakuwa si rahisi serikali kupitisha ajenda zake inavyoamua Tu. Ila kama zaidi 75% ya wabunge ni CCM, hata mradi usipobarikiwa na Bunge wao ni Sawa Tu.

Ukiitazama USA, Rais wakati mwingine mipango yake inakwama kutokana na uchache wa Kura za senate au congress
 
Oct 27, 2020
97
400
Ugatuzi wa madaraka. Magufuli alikuwa anafanya kazi iliyokuwa ifanywe na local government institutions, ila tu yeye alipendelea eneo/wilaya moja. Kungekuwa na serikali za mitaa/mikoa ambazo ziko huru kujiamulia mambo yake na kutekeleza mipango yake mwenyewe, Magufuli asingekuwa na haja ya kufanya aliyoyafanya.

Ugatuzi wa madaraka unasaidia kukuza na kukomaza demokrasia, kugawanya na kupunguzia majukumu central government, na kusogeza maendeleo na huduma kwa wananchi, kwasababu wao ndo wanajua nini hasa wanataka kwenye maeneo wanayoishi.

Serikali iko too centralized, ndo maana hata unakuta ili kujenga zahanati, madarasa, barabara za mitaa, hata choo tu, lazima idhini itoke serikali kuu. Wakati hizo kazi na zingine nyingi zingeweza kufanyika na serikali za mitaa/mikoa.

Ni vile CCM wana-allergy na kushare madaraka kwa mfumo wa aina wowote ule ndo maana ukiwaambia waziimarishe na kuziacha huru serikali za mitaa, na kuanzisha utawala wa majimbo, wanapinga kwa nguvu zote. Wakati ni faida kwa wote.
 
Jp Omuga

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
4,702
2,000
Kwanza ni kukitoa chama chakavu, pili kuweka katiba imara yenye taasisi imara na tatu kutochagua vichaa kwenye uongozi
Umepiga mule mule!

Na haya ndo kila siku nawaambia wale wanaodai Tume Huru na Katiba Mpya bila kwanza kuiondosha ccm!

Nawaambia ccm si chama cha siasa. Ni dude fulani hivi lipo lipo between serikali na wananchi kwa misingi ya kuwarubuni rubuni!
Transformation ya ccm kutoka kuwa chama dola kuja kuwa chama cha siasa haijawahi kukamilika!

Hivyo ujinga wa wananchi ndo mtaji mkubwa sana kwa ccm ili kuendeleza mifumo yake ya ovyo.

Kwa misingi hiyo; sidhani kama ccm wataridhia michakato ya Tume Huru na Katiba Mpya. Na wakiiridhia ujue wataivuruga tu!

Tusome alama za nyakati ccm wanavoendesha na kusimamia mambo ya kimafia mafia - wajumbe wao, polisi wao, n.k
 
Kumbisalehe

JF-Expert Member
Nov 25, 2014
717
1,000
Inahitaji fikra pana zaidi ya hapa tulipo.

Ni kipi alichofanya Magufuli Chato ambacho hakina umuhimu kwa wananchi wa kule?

Ukisema ni kiwanja cha ndege, unamaanisha kinatumiwa na wanafamilia ya Magufuli peke yao? Na kimejengwa nchi nyingine na sio Tanzania? Na ikiwa ni hivyo ili kuweka usawa ungependa kila wilaya iwe na kiwanja chake? Kama sio kila wilaya, ni wilaya ipi kikijengwa kwako wewe itakuwa sawa na haitaonekana ni upendeleo?

Wewe fanya kazi na ulipe kodi kisha mwakilishi wako bungeni ndio awajibike kuisimamia serikali itekeleze ilani yake kwa yanayohitajika huko uliko ambayo yako kwenye ilani.

Kilichopo ni kuwa watu wakimchukia Magufuli (ikiwa ni pamoja na wewe) lakini facilities alizosimamia zikawekwa au kujengwa wanazitumia. Ni sawa ndege alizonunua, makelele mengi ila mnapanda hizo hizo kwenda kwenu.

Fanya kazi, lipa kodi, jenga nchi yako.
 
Black belts

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
1,859
2,000
Ni wazi kuwa rais Magufuli aliipendelea sana wilaya ya Chato katika kupeleka maendeleo. Alijenga uwanja wa ndege wa kimataifa, alijenga hospitali kubwa ya rufaa ya kanda, alijenga chuo cha Veta, alianza kujenga hoteli ya nyota tatu, mipango ya kujenga uwanja wa mpira. Na mambo mengine mengi sana.

Haya mambo hayakuanza na Rais Magufuli, ni vile tu yeye aliyafanya kwa kiwango cha kushangaza.

Sasa siku nyingine atatokea kiongozi atafanya zaidi ya Magufuli alivyofanya. Nini kifanyike ili kuzuia Rais au kiongozi yoyote asiweze kufanya kitu kama hicho?
hatari sana
 
Mightier

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
5,755

Acheni Nongwa na Uswahili Kiongozi asipopendelea Kwao apendelee wapi? Kupendelea Kwao ni Dhambi?

Hivi siyo nyie nyie ambao leo mnamcheka Hayati Nyerere kuwa hakupajenga Kwao Butiama?

Watanzania tuna PhD's nzuri za Unafiki.
 
Kitombile

JF-Expert Member
Mar 21, 2021
737
1,000
Ni wazi kuwa rais Magufuli aliipendelea sana wilaya ya Chato katika kupeleka maendeleo. Alijenga uwanja wa ndege wa kimataifa, alijenga hospitali kubwa ya rufaa ya kanda, alijenga chuo cha Veta, alianza kujenga hoteli ya nyota tatu, mipango ya kujenga uwanja wa mpira. Na mambo mengine mengi sana.

Haya mambo hayakuanza na Rais Magufuli, ni vile tu yeye aliyafanya kwa kiwango cha kushangaza.

Sasa siku nyingine atatokea kiongozi atafanya zaidi ya Magufuli alivyofanya. Nini kifanyike ili kuzuia Rais au kiongozi yoyote asiweze kufanya kitu kama hicho?
Zanzibar kujengwa hotel za kitalii za bilions of dollar, kiwete kipindi anapendelea pwani kwenye uwekezaji wa viwanda pamoja na mashule hamkuona? Acheni ngebe
 
Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
1,300
2,000
Ni wazi kuwa rais Magufuli aliipendelea sana wilaya ya Chato katika kupeleka maendeleo. Alijenga uwanja wa ndege wa kimataifa, alijenga hospitali kubwa ya rufaa ya kanda, alijenga chuo cha Veta, alianza kujenga hoteli ya nyota tatu, mipango ya kujenga uwanja wa mpira. Na mambo mengine mengi sana.

Haya mambo hayakuanza na Rais Magufuli, ni vile tu yeye aliyafanya kwa kiwango cha kushangaza.

Sasa siku nyingine atatokea kiongozi atafanya zaidi ya Magufuli alivyofanya. Nini kifanyike ili kuzuia Rais au kiongozi yoyote asiweze kufanya kitu kama hicho?
Ninyi mliopewa madaraka sasa hivi chuki zenu ambazo mnashindwa kuzidhibiti zitawatokea puani huko mbeleni. Ofisi ya Tanesco inayojengwa ni ya kwake binafsi au kwa matumizi ya umma? Bajeti ya fedha hizo aliidhinisha nani wakati viongozi wasimamizi wake walikuwepo na bado wako madarakani? Mnataka kuonesha chuki zenu dhidi ya JPM kwa kuonesha ni kwa jinsi gani watu wanatakiwa wahudumiwe? Mradi kama huo haupo mahali pengine Tanzania? Kwanini mnaendelea kumzonga mtu asiyekuwepo kujitetea na mnatishia kushitaki wasaidizi wake?

Anzeni kwanza na walioko juu kwa sasa kwa sababu ndio walishiriki moja kwa moja kuidhinisha mradi kama huo.

Chato ni sehemu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kama ilivyo Kizimkazi, Kiwengwa, Mkokotoni nk

Mbona Msoga kuna makazi ya rais mstaafu yenye hadhi ya Ikulu ikiwa na hospitali kubwa ambayo hata Chalinze hawana lakini hakuna kinachosemwa?

Ifike pahala chuki hizi zikome mara moja kwa sababu mnatengeneza VISASI ambavyo havitakoma. Msijidai kwamba mtabaki madarakani, mnasubiriwa chini ili muadabishwe vizuri.

Mnaachia wezi mnafungulia mashitaki feki watu wasio na hatia kwa sababu ya chuki zilizokubuhu, inda na nongwa zinazonuka uvundo wa uharifu ndani yake.

Kumbe wakati JPM analalamika hujuma kufanyika ninyi ndio mnaziongoza kwa kuzipitia kwa wapinzania ambao kimsingi hawakuwa na nia ya kukwamisha maendeleo.

Achaneni na kesi feki ya Mbowe na Sabaya ili kurejesha mstakbali huko mbeleni
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom