Kilangi masanja
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 4,169
- 4,523
Safi kaka familia za kibongo hata mtu awe na uwezo wa kifedha kuweka tu hose reel nyumbani mtihani, kuna fire alarm kifupi kuna mengi ngoja niuandae uzi vizuri tuzidi pashana habariunapojenga nyumba yako binafsi jaribu kuweka escaping root ya siri ambayo ni wewe, mkeo au yeyote mkubwa ndani ya nyumba ndio mtakuwa mnaijua..
Jitahidi nyumbani kwako kuwa na fire extinguisher kubwa na medium na hakikisha watu wote kuanzia dada wa kazi na watoto wanajua namna ya kutumia, jitahidi kufanya fire drills nyumbani kwako na kuwatrain namna ya kutumia fure extinguisher.
Ukiwa uko vizuri funga fire suppression system ndani, joto likifika degree kadhaa vinafyatuka na kuanza kuuzima huku wazimamoto wanasubiriwa..
Kwa wale wenye madirisha yetu haya ya nondo au hizi grills, jitahidi ndani kuwe na hydraulic jack na ikitokea dharula piga jack dirisha okoa walio ndani kwenye hiyo njia..
Kama unaweza kujilinda na vibaka achana na hii minondo na machuma kwenye madirisha yako weka vioo tu kwenye dharula kinavunjwa tu, milango tuachane na hii mininga na mageti baadala yake tumieni MDF kwenye dharula teke moja unatoka nao tu..
Mungu mwenyezi mwingi wa rehma atuepushe na majanga kama haya na amfanyie wepesi majeruhi apone haraka na awape pumziko jema marehemu.