Nini kazi ya BASATA na Mwakyembe kwa wasanii??

sizonjemadawa

JF-Expert Member
Feb 11, 2017
1,053
1,304
Naandika uzi huu kwa masikitiko makubwa sana, yapata masaa 27 sasa hakuna tamko lolote kutoka kwa polisi, basata hata waziri wa dhamana Mwakyembe.

Roma ni msanii pia mwanadamu, anafamilia na watoto anawazazi na ndugu kuna watu wanamtegemea anamashabiki ambao akiimbia tunafurahi hadi machozi yanatutoka, tunaruka mpaka jasho linatutoka

Kitendo cha kukamatwa wasanii wa tongwe record, ni ishara mbaya sana kwa taifa hili hasa hatujui wako wapi, mpaka sasa na hakuna kauli yeyote kutoka serikalini, iwe jeshi la polisi.

Basata iko kimya mwakyembe yuko kimya hivi mnafanya kazi gani kwa wasanii hawa wanapopata matatizo, mnapenda kutoa matamko yasiyo na msingi ila wakipata matatizo hamuonekani, siku wakipata awards mnaenda jazana uwanja wa ndege kupiga picha, hiyo pekee haionyeshi uzalendo na malezi yenu kwa wasanii hawa, mnatakiwa mjitokeze hata wanapopata majanga kama haya, nilitegemea Basata wawe wa kwanza kuhoji, nilitegemea mwakyembe atoe tamko lake kuhusu wasanii wake ila wapi

Wasanii ni wakati wa kuungana, tukomeshe haya manyanyaso wanayotufanyia, kama wahariri wameungana na Heshima ipo kwa nini sisi wasanii tushindwe, juzijuzi Mr Ney ametishiwa maisha tumekaa kimya, tusisubiri matatizo wakati ni huu tuzibe hili pengo, mchango wetu ni mkubwa sana kwa taifa hili. Tunamashabiki wengi kuliko hata wanasiasa. hawa wanaotunyanyasa leo mwaka 2020 watatutafuta, tuwaonyeshe na sisi tutoe tamko la pamoja hatuna msaada mwingine kama siyo kuungana tu,
Hakuna Basata wala mwakyembe


Naombeni samahani kwa maandishi nimeandika kwa jazba na hasira zilizotwaliwa na woga wa kutishiwa maisha Yetu
 
Back
Top Bottom