Nini kauli ya Kikwete kuhusu ulinzi wa Majini na Utakatifu wa Ikului? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini kauli ya Kikwete kuhusu ulinzi wa Majini na Utakatifu wa Ikului?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ibrah, Sep 17, 2010.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Wadau, hivi karibuni kinara wa utabiri wa nyota nchini Sheikh Yahya Hussein alitoboa siri kuwa kuanguka jukwaani kwa Kikwete wakati wa uzinduzi wa KAmpeni za Urais ni kwa sababu ya kutumiwa Majini na mahasimu wake katika kinyang'anyiro cha kugombea Urais! KAtika kauli hiyo, Sheikh Yahya alibainisha kuwa sasa anatoa ulinzi rasmi wa Kimapepo kwa Kikwete kauli ambayo imechukuliwa kwa mifazamo tofauti.

  Bahati mbaya hata Kiwete mwenyewe amekaa kimya juu ya kauli hiyo ya Ulinzi wa Majini anaopewa na Sheikh Yahya na sisi Watanzania tunashindwa kujua kuwa ameukubali ulinzi huo au la. BAhati mbaya hata Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rai kwa sasa ni kama iko likizo au kwenye Kampeni na kusahau wajibu wake wa kutolea ufafanuzi kauli tata zinazolenga kumdhalilisha Kikwete, kuidhalilisha Serikali, kuidhalilisha Ikulu na Watanzania zilizotolewa na Mpiga ramli huyo ajiitaye Sheikh!

  Jana kwenye kamapeni za Kikwete na CCM pale Uwanaj wa Sheikh Amri Abeid Arusha, mpiga kura mmoja nilimsikia akisema amekuja kusikiliza tamko la Kikwete kukanusha kupewa Ulinzi wa Kipepo na Sheikh Yahya ili ajue kama ampe kura yake au la. Bahati mbaya sikukaa hadi mwisho maana Mh. Kikwete alianza kuhutubia saa 12 jioni.

  Nahofia sana, tena sana iwapo atachaguliwa kuwa Rais huku Ikulu na yeye 'Rais' akilindwa na Majini. Nina hofu kubwa Ikulu kugeuzwa kuwa sehemu ya Waganga wa kienyeji na Wachawi, na Wapuiga Ramli. Huku kuakuwa ni kuidhoofisha Ikulu na nchi kwa ujumla. Tafadhali sana Kikwete au Kurugenzi ya MAwasiliano ya Ikulu itoe tamko ii wengine tufanye maamuzi ya uchaguzi wa Rais hata kwa kigezo hicho.
   
 2. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kikwete anakubaliana na Shehe Yahaya.
  Kikwete analindwa na majini ya shehe huyu anayeirudisha Tanzania kwenye karne ya 10
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hawezi kusema lolote kwa sababu ni muumini wa maSheik na watanzania twatawaliwa na nguvu za kiza
   
 4. e

  edger blaston New Member

  #4
  Jun 11, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  thatz true
   
 5. D

  Dr.Mbura Senior Member

  #5
  Jun 11, 2011
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mchungaji Gwajima alimpaga JK siku saba aukanushe huo ulinzi ya mapepo aliposhindwa akatangaza rasmi mbele ya watu elfu sitini kwa kuwa rais amekaa kimya yeye ni mwanga na huyo mchawi Yahya akampa mwaka mmoja aache uchawi asipofanya hiyo atakufa na sasa kweli amekufa. Gwajima alimwambia JK umeshinda kupitia uchawi lakini kuna mchale wa Mungu unamwinda na hatamaliza miaka mitano madarakani
   
Loading...