Nini kama Taifa tumepoteza baada ya kufutwa kwa mbio za mwenge na sherehe za muungano

astranaut

JF-Expert Member
Jul 30, 2018
1,276
1,021
Kama kichwa kinavyo jieleza hapo juu,Taifa limepata hasara gani kiuchumi baada ya kuahirishwa kwa sherehe za muungano na mbio za mwenge kwa mwaka huu na fedha zote kuelekezwa kwenye covid-19.Kutakua na hasara gani endapo yote haya yakiendelea hivi hivi na fedha zile zikawa zinaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo? naimani mwenge wa uhuru hauko kwenye katiba ya jamhuri ya muungano hivyo basi hata kama rais ikimpendeza akaufuta hatakua amevunja katiba aliyoapa kuilinda
 
Upungufu wa ongezeko la UKIMWI maana mwenge unapolala sehemu huwa unachochea ngono kwa wenyeji na kuongeza idadi ya waathirika
 
Hakuna hasara maana hata hiyo miradi wanayozindua angeweza kuzindua waziri tu. Mwenge ufutwe tu.
 
Wanufaika wa huo mwenge na hizo sherehe za Muungano, kamwe hawatakuelewa. Ila kama siyo mnufaika, hakika utaombea tu Corona iendelee kuwepo.
 
Kifo cha forojo ganze hakikuwa bure ilikuwa kafara iliyokamilika!!Hata nyerere RIP anajua hilo!!!Tusubiri kafara itakayotolewa badala ya mwenge kutokimbizwa mwaka huu!!!ndio!kafara ya chato!!!!
 
Kuna hasara kubwa sana maana jobless wataongezeka. Unasahau kabisa ile ni miradi ya wakubwa ya kuenzi watangulizi wetu Mwlm nyerere.
 
Back
Top Bottom