Nini jipya litakalo fanywa na baraza la mawaziri litakalotangazwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini jipya litakalo fanywa na baraza la mawaziri litakalotangazwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mutwale, May 3, 2012.

 1. Mutwale

  Mutwale Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wanajanvi, kunataarifa za uhakika kwamba leo Mkuu wa kaya atatangaza baraza jipya la mawaziri, lakini napata taabu sana kughamua jipya litakalo fanywa na hao wateule, maana, 1. kikwazo kikubwa ni mfumo wa utawala uliopo, hakika hautawapa wateule nafasi za kuonyesha umahiri wao. 2. Makundi yanayokinzana yaliyopo dani ya chama ambamo watatoka na tatu serikali na chama tawala kupoteza mvuto mbele ya wananchi.

  Wote kama sio wengi tunakubaliana kwamba walau Mh. Makofuly amakuwa ni mbwa anaye bweka,lakini je situnakumbuka jinsi alivyo pigwa biti na mkuu wa kaya aliyemteua na MP? je hawa wanaoteuliwa hataweza kuzuiliwa kufanya kazi zao?

  Je Mwanuri, ninani asiyejua kwamba anajitahidi kupiga biti watendaji wa halmashauri? Lakini mbona ubadhirifu ulizidi kushika kasi? hii inadhihirisha kwamba mfumo wa utawala na utendaji ndio mbovu na hauwezi kurekebishwa kwa kubadili baraza la mawaziri bali mfumo mzima!

  Kwa kuwa tumebakiza miaka mitatu kufanya uchaguzi mwingine, JK akaushe tu, mpaka 2015 tutabadili mfumo mzima kwa kuweka Chama Kipya madarakani.
   
 2. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa, mfumo mbovu na wakulindana ndiyo tatizo hapa Tz! Yani hata kama ukiwa mzuri kiasi gani kwa mfumo huu utalazimishwa kuwa mwizi au kunyamazishwa mdomo. Mwone mzee kingunge, alijifanya mjamaa, hata nyumba akakosa akawa anaangalia watu tu, ila sasa baadae amelazimishwa na mfumo (tetesi - familia yake ilipewa tenda ya parking za magari dar, na stand ya ubungo mwanzoni kabisa). Kwa hiyo akalazimishwa kuacha ujamaa wake, Mwakyembe anajifanya anapingana na mfumo (tetesi - kapewa sumu walitaka wale kichwa), Magofuli na cheche zake unaona anavyoandamwa mara na PM, mara na JK mwenyewe! Kwa hiyo wapo wengi, ukichomoza kichwa kutetea nchi hii bana kinakatwa mara moja. Lazima tupigane tubadilishe huu mfumo wa kifisadi, la sivyo hata abadilishe mara ngapi bado watakuwa wezi tu, na baadae kila mtu ataonekana hafai kama ilivyo sasa kwa CCM. Nani utamwamini ndani ya serikali ya CCM? hakuna, labda wapo wazuri lakini mfumo na nidhamu ya uwoga inawafanya wote waitwe mafisadi
   
 3. Olaigwanani lang

  Olaigwanani lang JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 480
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kweli hakuna jipya....sina matumaini yoyote ....mambo ni yale yele tuu...
   
 4. Lastname

  Lastname JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 925
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tatizo ni JK, huu ni uozo wa kuusafisha 2015 tuanze na moja
   
 5. Lastname

  Lastname JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 925
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mimi nataka afanye hivyo ili kuongeza maadau wake na ugomvi nfdani ya CCM, maana mabifu yataongezeka sana.
   
Loading...