Nini huwa unakumbuka cha kwanza ukifikiria/ukisikia ‘Mother’s Day’?

Jumapili hadi ijumaa niliachwa nioge mwenyewe jumamosi mchana naogeshwa huku nikisuguliwa na jiwe huku likitemewa mate.... kilikuwa ni kifurushi cha wiki kwa kweli🙁🙁 big up mama saivi najua kuoga adi taulo halichafuki
😅😅😅doh pole mpaka taulo haichafuki 👏
 
Mama angu kamwe siwezi kumsahau maana kama sio yeye nisingekuwa vile nilivyo leo. Alijitoa sana kwa ajili yangu ma ndugu zangu akahakikisha tunakula, tunavaa na zaidi ya yote katusomesha kwa shida sana lakini hakukata tamaa hadi leo tuna elimu yetu. Mungu akupe maisha marefu mama angu mpenzi akuepushe na magonjwa, uwe na uzee mwema uone wajukuu na vitukuu vyako
 
Mangonifera,

Asante sana kwa haya umeeleza. Mama ndiyo msingi wa malezi ya watoto wenye muelekeo ambao unaweza kuwajenga na kuwaboresha kuwa watu wema katika jamii. Inahitaji kuwa na moyo jasiri, ndiyo maana ni rais kwa baba kumfurahisha mtoto kuliko mama ambao concern kubwa huwa zaidi katika hatma ya maisha ya baadae.

Hili suala la masingle mother kusemwa vibaya Jukwaani nalifikisha kwa Wahariri wa Jukwaa kuhakikisha ni suala ambalo linaangaliwa kwa ukaribu na kwa umakini, hivyo Asante kwa kulifikisha cc: Silencer

Hongereni sana kwa kusimama na kuweza kumudu maisha. Kikubwa, kukumbuka kutamka na kusema kwa mama zetu vile tunavyowathamini.


Hatimaye ufumbuzi umepatikana siku ya mama duniani!... Piga ban life ma -id yote yanayosema vby hawa watu
 
Umenifanya nielewe, si wote wanasoma content, nahisi pengine wewe ni wale mpe picha atakupa habari 🙈

Mie nimemtaja Babangu kutambua mchango wake pia na ni siku ya Mama.

Inatukumbusha siku ya mama ni moja tu katika mwaka mzima, na siku zilizobaki zote za baba.
 
Punguza basi mizinga Superbug, usidhani ana vingi, ni kwamba anajitahidi awezavyo, na kuna wakati unamuumiza ila unakuwa hufahamu sababu mara nyingi akina mama tunaficha maumivu.

Kumuenzi acha au legeza mizinga.

Mimi nikikwama nampiga mizinga mama mpaka Leo na ananipa zaidi ya ninachohitaji blessed mom.
 
Makiseo,

Inapendeza kumuenzi, haswa emotionally. Mwenyezi Mungu akujalie uwe mtoto mwema kwake mwenye kumpa faraja na amani.

Kila la kheri

Sina Maneno ya kutosha kumuelezea.. Nimeanza kutype hapa machozi yameanza kunitoka..Amejitoa kwa vingi sana kwa ajili yangu.. Sina cha kumlipa.. Sinaa..
Mungu akulinde Mama yangu NAKUPENDA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mr. Miela nimecheka sana! Hii post has made my day. Kuoga kwa doze 😅

Jumapili hadi ijumaa niliachwa nioge mwenyewe jumamosi mchana naogeshwa huku nikisuguliwa na jiwe huku likitemewa mate.... kilikuwa ni kifurushi cha wiki kwa kweli🙁🙁 big up mama saivi najua kuoga adi taulo halichafuki
 
Angalau siku hii ya Mama naweza kukumbuka mengi mazuri toka kwa mama. Kwa sababu yeye ndio aliyabeba majukumu yote ya mama na ya Baba pia. Tuliolelewa na Single mother's tunayo sababu ya kufanya kitu kwa ajili ya mama zetu.
 
Punguza basi mizinga Superbug, usidhani ana vingi, ni kwamba anajitahidi awezavyo, na kuna wakati unamuumiza ila unakuwa hufahamu sababu mara nyingi akina mama tunaficha maumivu.

Kumuenzi acha au legeza mizinga.
Ha ha ha mizinga ninayompiga mama yangu ni midogo hususan Kama bank za bongo zisipo tally na ac yangu hasa.

kwenye ishu.za kifamilia ila my mom is no#1 beneficiar of my youth accumulation. Katika Mambo ambayo najisifu kwa mama yangu ni kumpeleka hija Jerusalem na Peta tikva israel 2011
 
Nimependa mtazamo wako. Nimejifunza kitu.

Nimejifunza zaidi kwenye uzi wako na nikajiuliza maswali mengi sana bila majibu.

Shida niliyonayo nilikua rafiki sana na Baba, hata wakati wa msiba nilijua nimepata pigo kubwa sana na nnaamini ni kitu bora nilichowahi kuzawadiwa kwa haya maisha. Alitupiga na kuwa mkali pale unapokosea lakini baada ya adhabu maisha yanaendelea kana kwamba hakuna kitu kilitokea. Hapo ikaniaminisha kwamba kumbe Bsba anachochukia ni kosa nililofanya na sio mimi.

Kwa upande mwingine Mama alikua mkali vile vile tofauti ni moja tu, endapo ulikosea asubuhi, siku nzima hautakaa kwaamani, utasimangwa na kila ukipishana nae utachezea mwiko, upawa, ukuni au chochote alichonacho mkononi hata iwe sahani mradi hautapita salama. Nafikiri hii hali ukichanganya na yale maneno maneno yakaua vitu flani ndani yangu kabisa. Ile bond na Mama haipo. Lakini najua kabisa na kuthamini mchango wake kwangu sio tu malezi na kua mzazi lakini hata kwenye tabia, sijawahi kuwa kituko kwa watu.

Nimejitahidi kuleta ile ukaribu naomba nikiri nimeshindwa. Najitahidi kufanya kila niwezalo na kuna kipindi naongea nae lakini hiyo hali haidumu sana. Na yeye anaelewa kabisa jinsi tulivyo.

Licha ya hayo yote, huu uzi umenifanya nitafakari sana kwanini imefikia hapo na nini naweza kufanya tofauti na nilivyojaribu awali kuleta tofauti. Nimeongea na ndugu na marafiki baada ya kusoma huu uzi kuwajulia hali na kuonyesha kuthamini mchango qao wa kuwa Mama bora.

Mungu aendelee kumtunza, kumpa hekima na busara Mama na wamama wote duniani, awape nguvu na wepesi wa kupambana na changamoto zao.

Ubarikiwe pia kwa huleta hili bandiko.
 
Mrisho,

Mbona hata Father’s Day inasheherekewa? Kuthamini mchango wa Mama hakufuti nafasi ya baba.
Mothers are overly exagretated. ...something most don't understand is the fact that not everyone was raised by a single mother or rude father.

Men die earlier for the same society perception and stigma against father's. . Expecting them to be strong even at the time they need our love and passion... Jamii inamchukia sana baba
 
Nina mama na ndugu wa kike, nawapenda kama ndugu zangu wengine wa kiume! sioni umuhimu kwa nini hii kitu inakua soo documented, kwangu mie inawafanya waonekane kama walemavu wanaotaka watambulike ktk jamii.
 
Back
Top Bottom