Nini huwa sababu kuu za kuachwa au kusalitiwa na mpenzi, mchumba au mke wa ndoa?

Handsome boy 1

Senior Member
Jun 2, 2021
105
250
Kumekuwa na wimbi la usaliti sana siku hizi na tumekuwa tukishuhudia visa hata humu JF kuhusu usaliti na kuachana kwa wanandoa wachumba au wapenzi sababu ni nyingi sana lakini unavyoona wewe sababu kuu hasa inaweza kuwa nini?
 

Nyendeke

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
1,547
2,000
Utandawazi, maendeleo ya sayansi na Technologia na kubadilika kwa Mfumo wa Maisha katika Jamii zetu, vimepelekea kumomonyoka kwa Maadili, Jambo ambalo limepelekea Uovu kuwa ni Jambo la kawaida na la kujivunia Yani kuwa Malaya au Mzinzi imekuwa ni fasheni na linakuongezea umaarufu...!!!
 

adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
12,026
2,000
1. Kuingia Kwenye mahusiano kwa kuangalia sifa za nje. Unlikely and non merit basis
-Weupe
-Maji ya kunde
-Morphology (maumbile ya mwili) six pack, namba nane nk
-Urefu, hasahasa wanawake kupenda hiki kigezo
-Sura nzuri nk

Hizi sifa za nje zinamchango mdogo sana linapokuja suala la kudumu katika mahusiano. Ukiingia ndani unakutana na mambo ya Ajabu ajabu .... Tabia za ndani za mtu
-Majivuno
-Kujisikia
-Kujiona bora
-Kiburi
-Dharau
-Kununanuna
-Uchoyo
-Uvivu
-Ubinafsi
Nk
Teyari ufaaaa wakutosha ... maudhi, na Amani kutoweka


2. Tamaa ya vitu na mali..... uwezo
Fedha na Mali

Ukiingia unakosa zile sifa za msingi Ambazo ni.....

A. Upendo wa kweli

B. Utu

C. Unyenyekevu

D. Hisia za kweli

E. Thamani ya mwenza

F. Uvumilivu na kujitoa kwa dhati

Lakini sijuwi, mrefu, six pack, mweupe, mrembo, handsome ni ujinga tu na ndio vigezo vinavowaponza wengi kuingia mahusiano ya hovyohovyo na kujikuta Kwenye migogoro na mwishowe kutengana au kusalitiana.
 

tajiri tumbo kubwa

JF-Expert Member
May 27, 2021
325
500
ni hali ya maisha kubadilika kwa hali ya jamii,binti rafiki ya mtu au mke wa mtu anaangalie binti rafiki yake ana simu aina gani, anapelekwa out wapi, nae mke wa mtu anaangalia mke wa jirani au wale wanafanya kazi nao, je wanavaa namna gani, je wanakula aje, sasa kaa waume wao hawana hela, basi binti kaa huyu na mke kaa huyu anatembea je ya ndoa au mahusiano.ni hali ya maisha kubadilika na tamaa, siku hivi asilimia 80% ya binti na wake za watu hutoka na mwanaume wengine, hali baya sana
 

Madame S

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
15,837
2,000
Kila ndoa iliyovunjika ina sababu zake tofauti labda kila aliyeamua kuvunja ndoa yake ndo aseme sababu na uzuri Madame S ashajiandaa kuchukua notes chukua soft copy ndo nzuriπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
niko vizuri kwenye kuandika lakini mwandiko wangu naweza kuuusoma mwenyewe japo wakati mwengine natatizika vile vile
 

Demi

JF-Expert Member
Nov 22, 2016
25,349
2,000
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ tulitakiwa tupuyange tu kama wanyama vile au tufanye kama South Africa KE mmoja anaweza kuolewa na ME wa idadi atakayo mradi yeye mwenyewe na ME wameridhia 🀣🀣
hata msoma taarifa ya habari kaona kituko hahahahahaha
Tupuyange Kama wanyama ingependeza, wivu usingekuwepo. Matatizo mengi humu duniani yanasababishwa na mapenzi ya ubinafsi..eti kama ni wako ni wako tu, kiuhalisia hatuwezi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom