Nini hutokea baada ya kufa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini hutokea baada ya kufa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Joyceline, Apr 14, 2009.

 1. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kuna habari nimezisikia kutoka kwa watu mbali mbali kwamba mtu anapokufa, akazikwa zile siku tatu yaani siku alipozikwa unahesabua ya kwanza unaongeza siku zingine mbili anakuwa bado yupo duniani anatembea tembea, na anamfuata yule mtu aliyekuwa anampenda sana au wanaelewana kama ni mchana anaingia ndani anamwangalia hasemi kitu, na wanasema mtu huyo uso wake huwa unan'gaa sana huwezi kumuona vizuri, anaondoka siku ya pili anarudi usiku anakuita kwa jina akijua umesikia anakwambia njoo nje ukikataa anakwambia nimekuja kukuchukua ukikataa anakwambia basi, endapo utakubali mnaondoka mnaongea mkifika njiani anakwambia au rudi tu ukirudi kesho yake unakufa. Sasa kwa wale ambao wanajua mila hizi na sio waoga na kwao ni kitu cha kawaida akisikia anaitwa anamwambia njoo ndani anakaa wanaanza kuongea anampa maagizo fulani ambayo hakumwambia na mambo mengine anaaga anaondoka anamwambia hutaniona tena duniani nimekuja kukuaga.
  Ila aliyeniambia anasema hizi mila zipo sana kwa kabila la Wapare wale wazee wa siku nyingi wanajua na wanaona ni kitu cha kawaida mi nilishidwa kuelewa na mtu akifa asipokuja huwa wanuliza mbona fulani hajaja kuaga, au wanamuuliza yule aliyekuwa rafiki yake fulani ameshakuja kukuaga?

  Naombeni kama kuna mtu mewahi kusikia hiki kitu au anajua atuelezee zaidi.
   
 2. K

  Kilambi Member

  #2
  Apr 14, 2009
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mi sijawahi kusikia ila nimeona tu kwenye tamthilia ya "the second chance!
   
 3. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kilambi nadhani hujanielewa, second chance ni tofauti na hii story yangu, second chance ni roho ya mtu aliyekufa inaingia kwa mtu mwingine anaanza kuishi tena. Lakini hii ni tofauti nimesema marehemu ndani ya siku tatu anakuja kuaga wapendwa wake au mpendwa wake then basi anakuwa amekufa moja kwa moja kama watu wengine hataonekana tena anaonekana ndani ya hizo siku tatu za mwanzo tu. nadhani umenilewa.
   
 4. k

  kapuchi Senior Member

  #4
  Apr 14, 2009
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 167
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mimi sijawahi kusikia stori za namna hiyo ila mtu bwana akiisha kufa huwa amekufa,roho yake hutengana na mwili kabisa na kwenda mahali ambapo mwenyezi ajuaaye mambo na siri za binadamu amemuandalia kutokana na vile huyo jamaa alivyoishi hapa duniani,akisubiri ile hukumu yamwisho,aidha kwenda kukaa kwenye pepo ya mungu au jehanamu ya moto.

  hili suala la kutembe tembea kwa huyo aliyekufa si kweli,inawezkana ni roho za mizimu au mapepo zinazofaya kazi ya kuwatembelea ndugu au rafiki za huyo marehemu aidha zinatafuta mahali pa kuingia na kukaa au kuvuruga amani katika ukoo au jamii ile.
   
 5. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Imani yangu ni kwamba mtu akishakufa hana mawasiliano tena na duniani. Hiyo roho yake yaweza kwenda sehemu ambayo wanadamu hatuijui na hatunauhakika nayo may be peponi (hypothetical/belief).
   
 6. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  mtu akifa ndiyo mwisho wa mchezo, consciousness inaisha na entropy level inaenda zero.

  Ni vigumu kuwa na hakika lakini kwa yanayojulikana sasa hili ndilo linaloonekana kutokea.
   
 7. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...tafakari njozi zako baina ya saa 8:32 usiku na saa 9:28 usiku zitakupatia jibu. :)
   
 8. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hata mimi naamini baada ya kufa mawasiliano na duniani yanakatika. Lakini hiki chanzo changu cha habari kiliniambia vitu vya kushangaza nilimtolea mifano, biblia inavyosema kuhusu wafu yeye akasisitiza kikwao hicho kitu kipo na kinaendelea kutokea mpaka vizazi vya sasa hivi, nikasema au ni mzimu wa marehemu huwa unarudi au? yani alinielezea vitu vingi nikashangaa. ndo maana nikauliza kama kuna mtu amewahi kusikia hizi habari
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Apr 15, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mnapoambiwa ponda mali kufa kufa kwaja ,mnzania nini ,si mnaona mafisadi wanavyokomba ,wanajua wakifa ndio imetoka ,na haya mambo ya mapenzi na nini yote haya ,alizianeni hapa hapa duniani ukiwa hai ,usiingie na tamaa ya kwenda peponi ni moto mtindo mmoja ,yaani embu jipime ujione ka unaingia peponi ,uone kama utaenda kweny kundi la kula uhondo ,yaani wewe hapa unatakiwa uwe mtu wa kuvuruga tu ,unaponda kikweli ila kama mswalihina basi iwe hivyo.

  Hiyo huyo mdada mada yake inaulizia kuhusu maghost na mila flani flani ambazo amezisikia kuwepo hapa Tanzania aidha naweza kusema hakuna kitu hicho,ila inakuwa ni njozi na njozi zinatafsirika ,kivyakevyake na zinakuwa na ukweli kwa kiasi fulani na zoko njozi za kuchoka hizi hazina maana yeyote ni kukuliwaza usingizini tu.
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Apr 15, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Joyceline,
  Acha kutazama na kuamini kipindi cha - Ghost Whispers!..
   
 11. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #11
  Apr 15, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Dada yangu Joyceline, haya mambo ni mambo ya Hadithi za kusadikika. Myth. Hayana ukweli hata kidogo, nimambo ya imani za kijadi, katika kuendeleza dhulma na unyang'ani katika koo husika.

  Kwanza nikufahamishe jambo moja, si kabila na koo za kipare tu zenye tabia hizi. Hata hizo nchi zilizo endelea kuna jamii zenye kuamini jambo hilo la maiti kurudi tena na ikiwezekana kuondoka na mmoja wa wanadungu, hususani yule anaye mpenda sana. Ngano za kale (Myth) ambazo watu wengi siku hizi wanazifuata bila kujuwa kuwa ni urithi wa kipagani, ni huu uvaaji wa nguo nyeusi msibani.

  Wapagani wa kale waliamini kuwa ukivaa nguo nyeusi kwenye msiba basi maiti ya mtu yule haitakuona itakapo rudi duniani. (kwa mtindo huo ulio ueleza hapo juu). Imani hii ikapelekea watu wengi kuvaa nguo nyeusi wakiamini kuwa hawata onekana pale maiti itakapo kuja kutaka kuambatana nayo. Hii ni sawa na kusema kuwa paka mweusi ni nuksi, au ukisikia sauti ya bundi ni uchuro, nk, nk.

  Tukirejea kwenye suala la maiti kuja kutoa maagizo fulani fulani, hii ni aina ya dhurma, ninasema dhurma kwa sababu suala la maiti au mfu kuja kutoa maagizo mara nyingi huyo mfu umtokea mzee wa ukoo au mtu ambaye anajuwa kabisa akisema hata pingwa. Na mara nyingi maagizo hayo uhusiana na mambo ya urithi katika njia ya kuwadhurumu wenye haki ya kurithi.
  Unavyo fikiria mzee wa koo fulani au huyo anaye semekana kuwa ni kipenzi chake akisema kuwa mfu fulani kanijia na kanifahamisha jinsi kadhaa wa kadhaa, ni nani wa kupinga...!? na kama ni kweli wafu huja kutoa maagizo kwa nini wasije au wasitokee kwenye kikao cha mazishi na kwanini wasubiri mpaka wazikwe? Na kama ni kweli kwa nini wasitokee wakaonekana na wana ndugu wote. Kwa nini hawe mzee fulani au mtu moja fulani tu!? Huu ni utapeli uliochanganyika na wizi.

  Aliye kufa amekufa dadangu, yatakayo kumbukwa ni yale matendo yake aliyoyafanya hapa duniani tu basi.

  Ukisikia siku nyingine wazee wakidai fulani hajaja kuaga ujuwe wamesahaulika kwenye ulaji (Urithi wa mali). Lakini wakipewa chochote kitu kutoka kwa wafiwa, hutasikia hayo maneno ya mfu hajaja kuaga.
   
 12. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #12
  Apr 15, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  asante nimekuelewa sana, nilikuwa napata utatanishi.
   
 13. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #13
  Apr 15, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  siyo kwamba naamini , mimi ni mkristo na niko makini na imani yangu sana, kilichopelekea kuandika haya ni hivi,

  Last week nililala kwenye msiba nikalala na mfiwa sasa tumelala chini mimi nilikuwa karibu yake,usiku nikasikia anaongea kama anajibishana na mtu, anaitika anasema sawa, nikajua anaota asubuhi nikamwuliza ndo akaanza kunipa hizo habari fulani kaja kuniaga kwamba kuna maagizo alikuwa anapewa.
   
 14. Y

  Yana Mwisho Member

  #14
  Apr 15, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mpendwa Joyceline,
  Kwa imani yangu na nahakikishiwa na maandiko matakatifu kuwa mtu akishakufa ni mwisho wa mchezo. Hayo mengine yanayoweza kutokea ni michezo ya kuigiza tu, na yawezekana ni roho chafu toka kuzimu. Hakuna mawasiliano kati ya mfu na aliye hai. Biblia inasema; 'Kama wanadamu walivyowekewa kufa mara moja, baada ya kufa hukumu' Waebrania 9:27.


  Hebrews 9:27 (New International Version)
  27Just as man is destined to die once, and after that to face judgment,
  [/B][/B]
   
 15. KIFARU

  KIFARU Senior Member

  #15
  Apr 15, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 172
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Anachoongea joyceline kinauwezekano kipo, ila sema watanzania wengi tunapenda kuletewa chakula kilichotayari kuliwa kuliko kwenda kuanza kukiandaa shambani as seed mpaka ukipike mwenyewe ndo uanze kula,namaanisha watanzania wavivu wa kufanya tafiti, na ndo maana vitu vikitoka nje ya nchi tunavishangaa sana
   
 16. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #16
  Apr 15, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ..Je na wewe unataka ukishaundei uzagaezagae mitaani? siku hizi mgambo wa city wanakamata wazururaji ohoo usije ukashikwa
   
 17. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #17
  Apr 15, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  mimi sitaki, lakini hazururi aanaenda kwa mlegwa tu na mlegwa ndo anamuona
   
 18. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #18
  Apr 15, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mi shetani nimemwona amekaa kama picha iliyoko kwenye negative ,ni kutishana tu.
   
 19. I

  Ikena JF-Expert Member

  #19
  Apr 16, 2009
  Joined: Oct 24, 2007
  Messages: 482
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 60
  Mimi fikra zangu huwa zinanipelekaga kwingine kuhusu kifo.

  Isije tukaja kujilaumu kwanini hatukujiuaga mapema ili tufaidi raha ambazo pengine wenzetu waliofariki wanazipata,regardless matendo yao yalikuaje hapa duniani.

  Nafikiri kunamaisha mazuri/bora kwa wote baada ya kufa.
   
 20. a

  ashikudire New Member

  #20
  Apr 16, 2009
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Joycline kwa sababu wewe ni mkristo soma sana bible mambo yote yako huko.
  Mtu akifa amekufa na hana ushirika tena na walioko duniani, swala la mtu aliyekufa kuja kuaga kwa muda wa siku tatu au zozote hilo halipo kabisa.

  Shetani ni mjanja sana na hutumia vitu vingi kuhalalisha uongo wake na kuwapotosha watu. Kimsingi huyo dada alikuwa anaongea naweza kusema na mizimu au pepo kama alivyosema mmoja wetu.

  Mara nyingi katika kabila mbalimbali au koo au familia mambo ya mizimu yametawala sana kila jambo linalotokea watu husika wanauliza mizimu, kwa kutambika na kadhalika. Huu ni uomgo mkubwa.

  Mizimu au mzimu ni pepo ambalo linavaa sura ya mtu aliyekufa na kuanza kufuatilia watu aliokuwa nao karibu au familia. Kimsingi huyo pepo kazi yake ni kuwafanya watu wa mhusika kuona kwamba wanaongea au wanapata maelekezo fulani toka kwa aliyekufa, mwisho huamini na yale mambo wanayoambiwa na pepo huyo huwa hutokea. Hii yote ni machukizo mbele za Mungu, mtu akifa amekufa na hana mawasiliano tena duniani.

  Nakusihi usiamini vitu hivyo hata siku moja hata kama una ndugu yako amekufa akikujia kwa ndoto au vyovyote vile kemea kwa Jina la Yesu hatakuja tena.
   
Loading...