sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,325
- 2,487
Habari za Jumapili wadau,
Ni matumaini yangu kuwa mpo salama, na wale ambao hawapo vyema, basi Mwenyezi Mungu awatie nguvu.
Hii mada ilikuwa inajadiliwa leo Radio One katika kipindi cha Familia kinachorushwa kila Jumapili na Abdalah Mwaipaya pamoja na binti Fariyah. ''NINI KINASABABISHA WANANDOA KUISHI KWA WASIWASI?''
Nikavutiwa na point moja kuwa; kuna wazazi ambao binti zao wakiolewa, hutengewa chumba, godoro na kitanda na huambiwa ukiona huko mambo ni magumu urudi mwanangu!
Kama kweli yapo, basi hiki ndicho chanzo kikubwa cha ndoa nyingi kuvunjika kwani binti huyo atakuwa anakaa kwenye ndoa mguu mmoja ndani na mwingine nje, sasa hapo hakutakuwa na ndoa.
Wewe mdau unalionaje hili la kumtengea binti chumba hadi godoro? Na je nini sababu ya kuishi kwenye ndoa kwa wasiwasi?
K a r i b u k w a m c h a n g o.