Nini husababisha Septic tanks (chemba za choo) kujaa mapema?

Kifaranga

Senior Member
Jan 6, 2011
144
31
Wakuu habari za leo?

Naomba kujuzwa kuhusu septic tanks! Nimehamia kwenye kibanda changu ninakaribia kumaliza mwaka tangu nihamie.

Kuna kitu nakiona hapa ambacho sicho cha kawaida kwenye chemba zangu za choo, kwani ile chemba kubwa (soakaway au ditch sijui ndio kiingereza) kimeanza kujaa mapema sana. Yaani kimeshafikia zaidi ya nusu!

Sasa najiuliza maswali hii inaweza kuwa imesababishwa na nini? Ninachohisi kwanza ni mvua za masika inawezekana mvua yote ile ya masika kuanzia mwezi wa pili mpaka wa tano itakuwa imeingia kule kwani yale maji hayatoi harufu kaki sana na pia ile septic tank ishaanza kupeleka mzigo kwenye ditch.

Pia inawezekana ufundi wa kujenga haukufuatwa vizuri (yaani fundi amekosea).

Sasa naombeni ushauri kwanza inaweza kusababishwa na nini na pili njia rahisi ya kutatua tatizo hili.

Nimesikia kuna dawa ambayo unanunua kisha unaimwagia kwenye chemba kubwa kisha maji yananyonywa yote mpaka chini, ni dawa gani hii na inapatikana wapi na bei yake.

Nashukuruni wataalam

Nawakilisha
 
Kwa kiasi kikubwa baada ya mvua kuanza kunyesha kwanza water table huwa inapanda lakini pia seepage ya maji ya mvua kwenye udongo hufanya udongo uwe saturated na hivyo kushindwa kunyonya maji yaliyomo kwenye soak away pit

Dawa ni kunyonya hayo maji taka ili kutoa nafasi kwa maji taka mapya
 
nauza dawa ambayo nakiangalia choo chako nacalculate dose nakupa, advantage: inakata harufu,pia ina activate bacteria wanakua active wanadigest uchafu wote.Ofisi ipo river side au nipgie nikupe ushauri free 0754079678
 
Nenda Kkoo sokoni (ndani ya jengo la soko) na utapata dawa za kushusha level ya Choo. Sijui bei ila kwa mwenye kibanda kama wewe naamini hiyo bei itakua affordable
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom