Nini husababisha kutokujiamini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini husababisha kutokujiamini?

Discussion in 'JF Doctor' started by Titus, Oct 28, 2008.

 1. Titus

  Titus Member

  #1
  Oct 28, 2008
  Joined: Jul 28, 2007
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Poleni na majukumu viongozi na mniwie radhi kama nitakuwa nimekosea title, ila ipo hivi, mara nyingi ninapokuwa nafanya presentation yoyote ile na hasa kama nitakuwa nipo mbele ya watu wanaozidi watano, huwa naishiwa na maneno na niaanza kutetemeka sana, 'confo' lote linashuka na ninasahau kila kitu nilichakiandaa, kama ni ppt inabidi nianze kusoma bila hata ya ufafanuzi, hili ni tatizo kwangu na ninaomba mnifahamishe kama ni tatizo la kiafya/kiakili na ninawezaje kuwa na 'confo' la kawaida, mara nyingi inabidi niwe nimetandika konyagi ili niweze kupresent vizuri, lakini hii naona haifai kiutendaji, naombeni ushauri wenu.
   
 2. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hilo la Konyagi kidog umekosa shabaha!I suggest uwe unafanya practise nyumbani kwako kwa kuhutubia mkeo na wanao kama hauna!If that does not work out jaribu pipi machungwa!There is something about them that gets your fear off!
   
 3. Kinyau

  Kinyau JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2008
  Joined: Nov 24, 2006
  Messages: 793
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Titus pole sana
  Tatizo hili hukumba watu wengi sana, Moja ya sababu kuu ni makuzi kuanzia nyumbani kama mtoto hajengewi mazingira ya kujiamini ni tatizo, eg mtoto anapotaka kusema kitu wazazi wakamcheka au kumwambia anyamaze basi mara nyingi atajenga hofu hata kuongea kwa wenzake.
  Pia mashuleni, kama walimu hawawapi wanafunzi kujibu maswali, kujadiliana, kufanya debate basi watoto huwa na woga wa kuongea mbele za watu.

  Jaribu hatua hizi chache
  1. Jiandae ipasavyo kwa mada utakayoongelea-Pitia taratibu mada na ijue inside out
  2. Fanya zoezi: baada ya kujiandaa basi fanya zoezi la kutoa mada hiyo ,mualike rafiki yako akusikilize na kukukosoa.Ukiwa fiti jiweke sawa kwa siku yenyewe kwa mavazi nadhifu.
  3. Presentation;
  a) Kupunguza hofu salimiana na audience wako wanapoingia chumba cha presentation
  b) Anza kwa kujitambulisha na kama wao ni wachache basi wape nafasi wajitambulishe au kama mwafahamiana basi anza na mada
  c) wakati wa presentation usisimame wima kama mlingoti, hii huongeza stress kwani misuli na damu havishughuliki sana, tembea tembea, angila kona tofauti na endelea kutoa mada taratibu

  d) Hakikisha unashirikishana vema na unaowapa mada kwa kuuliza maswali, kuomba extra comments,nk

  e) Chagua "cheerleaders"(sijui niwaitaje) :katika presentation lazima kuna watu wanafuatilia kwa makini labda wanatikisa vichwa au kusmile ukitoa point fulani hawa ndio tunawaita cheerleaders ktk presentation;Utapojihisi unakosa confidence pata courage fro these cheerleaders na amini kuwa hata kama kuna kitu nakosea kidogo basi kuna watu wanafurahia presentation yangu.

  f) Tumia body language vizuri: kama unaelezea janga linaloikumba kampuni huwezi kucheka cheka, body language ionyeshe kweli nawewe umeguswa na janga hilo. Kama unaeleza sera mpya za kampuni pia utaonyesha userious fulani,na kama unaleza jinsi kampuni ilivyovuka malengo kwenye mauzo na kukamata wateja wengi hakika hapo uso wako utakuwa excited kwani ni habari ya neema kwa kampuni. Huwezi kusema "ninafuraha kuwaeleza mafaniko makubwa tuliyopata mwaka jana" huku umenuna na uso umejikunja,audience wanaona body language inavyopingana na maelezo yako

  g)Amini kuwa unaweza na kila presentation iwe bora kuliko iliyopita: remember the rule of thumb "Practise makes perfect"

  my take:
  ktk society yetu public speaking imekuwa ni tatizo sana, tu wasomi, tu nadhifu but we cant speak our thoughts out. Basi tuanze kwa watoto, tuwajengee mazingira ya kujiamini-hata kumpa mtoto akueleze jinsi alivyospend siku yake yatosha.
  Na shule zetu ziwape changamoto watoto kwa midahalo na majadiliano.
   
 4. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Titus,
  Umenikumbusha landlord wangu mmoja nadhani alikuwa na tatizo la kutojiamini kwani kila alipotaka kuzungumza na sisi wapangaji wake ilikuwa lazima akatie kilaji kidogo kiasi kwamba nilidiriki kumuuliza siku moja kuwa hivi hawezi kufanya mazungumzo nasi akiwa sober? Jibu alilonipa ni kuwa kila mtu ana style yake ya kujiandaa kuzungumza katika hadhara. Pole, inatokea nadhani ushauri waliotoa wana-JF wengine ukiuufanyia kazi unaweza kukusaidia.
   
 5. Titus

  Titus Member

  #5
  Oct 29, 2008
  Joined: Jul 28, 2007
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kinyau,
  ushauri wako ni mzuri, ni kweli hili tatizo ni la watu wengi na kila mtu anamtazamo wake tofauti, changamoto hii ianzie kwenye makuzi ya watoto wetu as from majumbani mpaka mashuleni pia, thanks a bunch
   
 6. Kinyau

  Kinyau JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2008
  Joined: Nov 24, 2006
  Messages: 793
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Anytime Sir
   
 7. M

  Mundu JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2008
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Titus, kila binadamu ni muoga kwa kiasi fulani! hakuna mtu ambaye anaweza kwa asilimia mia kujidai kuwa ni kigaga wa Public speaking. Pia inategemea na topic unayotaka kuzungumza. mara nyingi kwenye presentation, presenter pekee ndiye anayejua nini cha kuongea... wengine ni wasikilizaji tu.

  Naongezea kwa yake aliyosema Kinyau.
  1. Jiandae vema kabla hujapresent.... hakikisha unajua unachikisema... kama ni namba zielewe vizuri na kuwa atayari kuzifafanua na kuzitetea
  2. fanya presentation kavu nyumbani, au kwa rafiki. Hii huitwa ''Dry Run''. rekodi na muda unaotumia... nyingi ya presentation zina time limit
  3. Ijue hadhira yako... wale watu watakao kuwapo katika presentation... know who is who na wana influence gani?
  4. Anza na opening Gambit... Hii ni ile utambuzi wa presentation yako. Kwa mfano waweza sema hivi "mnapenda kufahamu siri ya mafanikio ya kampuni yetu?" Hii huleta msisimko wa hadhira kukusikiliza
  5.Maintain eye contact na hadhira yako... hii husaidia hata unapofanya interview kwani huonyesha kujiamini
  6. Itumie vizuri lugha ya mwili katika kuzungumza na kutenda. Hii huitwa Body language
  7.Ukisha manage the first two minutes za presentaion.. the rest ni kutiririka tu.
   
Loading...