Nini hupelekea mtu kuwa na tabia/mawazo ya kutaka kujiua, namna ya kumgundua na kumsaidia mtu huyo

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
IMG_20210317_133631_807.jpg

Kujiua ni kitendo cha mtu kukatisha maisha yake. Tabia ya kutaka kujiua ni ile hali ya mtu kuchukua hatua zinazohusiana na kukatisha maisha yake. Mawazo na tabia ya kutaka kukatisha maisha inachukuliwa kama dharura ya ugonjwa wa akili.

Takwimu za 2016 zinaonesha kuwa karibu watu 3,001 walijiua nchini Tanzania kwa mwaka huo pekee, na kuiweka Tanzania kuwa nchi ya nne Barani Afrika kwa takwimu za kujiua, nafasi hiyo ni nje ya nchi zilizo na kiwango kikubwa cha kujiua.

Kwa mujibu wa American Foundation for Suicide Prevention, kujiua ni sababu ya 10 ya vifo duniani.


Sababu za kutaka kujiua

-Mara nyingi sababu kuu ya mtu kutaka kukatisha maisha yake hutokana na msongo wa mawazo unaotokana na hali ngumu ya maisha, vichocheo hatarishi katika maisha na kukata tamaa

-2019 ripoti kutoka Wilaya ya Ngara katika Mkoa wa Kagera zilionesha kuwa katika kipindi cha miezi mitatu watu wapatao 30 walijiua kutokana na mizozo ya ndoa na familia, kukatishwa tamaa katika mahusiano na mimba zisizotarajiwa zikitajwa kuwa sababu kuu.


Zifuatazo zinatambulika kama dalili za mtu anayetaka kujiua

-Huwezi kutambua kwa urahisi mtu anavyojisikia ndani ya mwili wake, kwahiyo ni kazi ngumu sana kumtambua mtu anayetaka kujiua. Hatahivyo kuna dalili za nje zinazoweza kukutambulisha dalili za mtu anayetarajia kukatisha uhai wake.

•Kutishia ama kuzungumzia kuhusu kutaka kujiua
•Kujitenga ghafla na marafiki, familia na jamii
•Kuongeza kiwango cha matumizi ya pombe na dawa za kulevya
•Tabia ya ukali ya ghafla
•Mabadiliko makubwa ya mhemko (mood swing)
•Kuongelea, kuandika au kuwaza kuhusu kifo mara kwa mara kama njia sahihi
•Tabia ya ghafla ya uzembe au kusukumwa kufanya jambo
•Kulala sana au kidogo
•Kuzungumzia kuhusu kukosa tumaini na upweke

Namna ya kuzungumza na mtu anaetamani kujiua

-Kama umemtilia shaka ndugu yako ama rafiki wa karibu ana dalili za kutaka kujiua basi unaweza kujaribu kuzungumza nae. Unaweza kuanza maongezi kwa kumuuliza maswali ambayo hayamuhukumu wala kumpinga.

Katika maongezi zingatia yafuatayo;

•Tulia na ongea kwa sauti ya utulivu
•Tambua ama kiri kwake kuwa hisia zake ni halali
•Muoneshe hali ya kumsaidia na kumpa moyo
•Mwambie kuwa msaada wa kile kinachomsumbua utapatikana na atajisikia vizuri pindi atakapotibiwa

-Hakikisha haufanyi tatizo linalomsumbua kuwa dogo au kujaribu kumlazimisha aache maamuzi yake. Kumsikiliza na kuonesha msaada wako kwake ni njia njema zaidi ya kumsaidia. Unaweza vilevile kumshauri aweze kupata msaada kutoka kwa mtaalamu.

-Vilevile unaweza kumsaidia kupata msaada kwa mtaalamu kwa kupiga simu au kumpeleka kwenda kuonana nae.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom