Nini hukumu yao siku ya Kiama kwa wale wasiopata neno la Mungu tangu wazaliwe hadi kifo?

Mkuu,hadith yenyewe ni miongoni mwa mamia ya hadith dhaifu na ya uongo(maudhu'u).
Sasa kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaachia kuwepo na hadith zenye uongo?

Na kama kaachia hadith zenye uongo, unajuaje kama hajaachia Quran yenye uongo?

Na kama inawezekana Quran ina uongo, na unaamini Mungu yupo kwa sababu Quran imesema, unajuaje kwamba Quran inaposema Mungu yupo, haisemi uongo?
 
Kauthibitosho ndiyo kanahitajika
Mpaka sasa hakuna aliyeweza kuthibitisha Mungu yupo.

Kwa sababu hayupo.

Ukisoma dhana ya kuwepo huyu Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, inajipinga yenyewe na inapingwa na ulimwengu tunaouona.

Kwa sababu Mungu huyo hayupo.
 
Hii ni dhana iliyopokatika dini nyingi.

Kwa minajili ya kwamba:

Kujiendeleza mwenyewe kiroho kunataka ubinafsi fulani. Kuufungia mlango ulimwengu. Lakini,njiahiyoinapunguza uwezowa kugusa maisha ya watu wengi.

Kutaka kugusa maisha ya watu wengi, maana yake utapunguza muda wa kujiendeleza mwenyewe kiroho.

Katika Buddhism, ukitaka kuwa Buddha,unapitiakuwa Bodhisattva.

Bodhisattva anakuwa na uchaguzi wa kufanyamawili.

Aukimbie ulimwengu na kuwahi kuwa Buddha.

Au.

Arudi kufanya kazi kwenye ulimwengu, na kugusa maisha ya watu weng ikama Bodhisattva, lakini achelewe kuwa Buddha.

Ni dhana ile ile.

Si kweli. Huwezi kumlinganisha Siddatha Sakyamuni; kazi na mafundisho yake na Yesu Kristo. Hawafanani hata kidogo.
 
Ulivyotaja hapo ni kwa yule ambaye ameshaijua dini ipasvyo kwa hivyo vitu vingi katika imani ni sharti kwake na si kwa yule ambaye hakupata dini kabisa na mungu anajua zaidi.
Kwa mfano kama kuna watu hawakupata dini kabisa siongelei north korea na nchi kama hizo kwa kuwa wale wanajizuia wenyewe wasipate kwa hivyo hukumu ipo pale pale,ila kwa yule ambaye tuchukulie alikuwepo katika jamii ambayo haimjui mungu wala haijui chochote kinachoendelea duniani (namaanisha hawaelewi nn maana ya technology hawajawahi kuona gari wala chochote cha morden yaani wao na pori na maisha yao ni yale ya kuhama hama kitu kinacho sababisha wawe mbali na watu wa jamii nyengine ) kwa hawa mungu atawahukumu kwa kupitia akili zao.
Kweli kabisaa
 
Sasa kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaachia kuwepo na hadith zenye uongo?

Na kama kaachia hadith zenye uongo, unajuaje kama hajaachia Quran yenye uongo?

Na kama inawezekana Quran ina uongo, na unaamini Mungu yupo kwa sababu Quran imesema, unajuaje kwamba Quran inaposema Mungu yupo, haisemi uongo?
Mkuu nikuulize swali kidogo ww unavyoamini nini chanzo cha ulimwengu na uhai duniani kwa ujumla?
 
Si kweli. Huwezi kumlinganisha Siddatha Sakyamuni; kazi na mafundisho yake na Yesu Kristo. Hawafanani hata kidogo.
Wapi nimemfananisha Siddatha Sakyamuni, au kazi na mafundisho yake na Yesu Kristo?
 
Mpaka sasa haijulikani Ipi dini sahihi, na kwanini liwe fumbo? Kama kuna jehanam kweli basi hatujatendewa fair. Labda kama haya Maisha yetu ni prank Tu hatutaenda popote
 
Mkuu nikuulize swali kidogo ww unavyoamini nini chanzo cha ulimwengu na uhai duniani kwa ujumla?
Sijajua, kwa sasa inaonekana atakayeweza kupata quantum theory ya gravity na ku reconcile Einstein's Relativity na Quantum Physics anaweza kutusogeza karibu zaidi huko kwenye jibu.

Pia, inawezekana dhana nzima ya "chanzo cha ulimwengu" ina makosa, kwa sababu inatokana na uelewa wetu wa ulimwengu uliopo katika mauzauza tunayoyaona katika scale yetu tu ya ulimwengu, ukirudi chini katika quantum level, hakuna "cause and effect", hakuna definite time na hivyo, dhana nzima ya "chanzo cha ulimwengu" inatoweka.

Kuhusu uhai, haujatoka kwa Mungu muweza yote, mwenye upendo wote na ujuzi wote kwa sababu

1. Huhitaji Mungu ili kutengeneza a complex system.
2. Kama unahitaji kitu complex kingine kuumba complex systems, mnayemuita Mungu naye atahitaji mumba wake na hivyo atakuwa si Mungu
3. Uhai tunaouona una mapungufu mengi sana. Magonjwa, kifo, vilema, ineficiency etc. Mungu huyo angekuwepo angumba mfumo wa uhai bora zaidi ya huu.
 
Mpaka sasa haijulikani Ipi dini sahihi, na kwanini liwe fumbo? Kama kuna jehanam kweli basi hatujatendewa fair.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, angekuwepo, asingekuwa unfair hivyo.

Ulimwengu huu umewezekana kwa sababu Mungu huyo hayupo.
 
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, angekuwepo, asingekuwa unfair hivyo.

Ulimwengu huu umewezekana kwa sababu Mungu huyo hayupo.
Yani kila nikiwaza haiingii akilini kabisa. Inakuwaje aliyetuumba Kwa mapenzi yake atupe adhabu Kali kiasi hicho na ashindwe kumpoteza shetani kabisa tuishi peacefully life Bila kukiuka amri zake. Hii dunia tungekuwa tunaongozwa na mungu mmoja basi hata dini ingekuwa moja. Na wamekufa watu wengi Sana tangu dunia iwepo na hakuna KUNDI la watu waliojitokeza Kuwa wamefufuka.
 
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?

Imekuwaje Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na uoendo wote akaumba ulimwengu ambao inawezekana tetemeko la ardhi likamzika hai na kumuua mtoto mchanga?

Huyu Mungu alishindwa kuzuia mambo kama haya alipokuwa anaumba ulimwengu? Au ni mkatili tu aliweza kuzuia lakini hakutaka?

Kama alishindwa kuzuia, ninkweli ana uwezo wote?

Kama aliweza kuzuia ila hakutaka tu, ni kweli ana upendo wote?

Unaweza kuthibitisha huyu Mungu yupo?
My signature. Niyakuja soon kwenye mjadala!

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
Yani kila nikiwaza haiingii akilini kabisa. Inakuwaje aliyetuumba Kwa mapenzi yake atupe adhabu Kali kiasi hicho na ashindwe kumpoteza shetani kabisa tuishi peacefully life Bila kukiuka amri zake. Hii dunia tungekuwa tunaongozwa na mungu mmoja basi hata dini ingekuwa moja. Na wamekufa watu wengi Sana tangu dunia iwepo na hakuna KUNDI la watu waliojitokeza Kuwa wamefufuka.
Ili ufaulu mtihani lazima usome kwa bidii..so ili uione pepo kuna maisha lazima upitie
 
Mfano nchi ya China 90%, North Korea 99% hawajui Quran wala Biblia. Pia huku Africa miaka ya 1900 kurudi nyuma dini zilikuwa bado hazijafika, nchi kama North Korea ni strictly prohibited.

Tueleweshane hapa maustadhi na wachungaji....
Chief hili swali nilishawahi kuuliza nikiwa na umri wa miaka 9 na nilijibiwa kwamba Mwenyezi Mungu anayajua ya dhahiri na ya siri katika moyo(akili) za wanadamu hivyo kwa kipimo hicho atawajua watu wema na waovu na pia kwa mtazamo wangu siku hiyo huenda kukawa na mtihani maalum kwa watu wa kundi hili maalum na wale watakaofaulu wataenda mahali pema na wale watakaofeli wataenda kulipia mabaya yao
 
Wapi nimemfananisha Siddatha Sakyamuni, au kazi na mafundisho yake na Yesu Kristo?
Unapojibu hoja niliyoitoa kwa kuyaweka mafundisho ya Kibuddha sawa na nilichosema kuhusu Yesu Kristo huku ukimalizia " ni dhana ile ile" ndipo nilipoona jitihada zako kumlinganisha Yesu na Buddha.
[
 
Neno la Mungu lipo hata nje ya maandishi ya vitabu vitakatifu. Pia kuwasiliana na Mungu siyo lazima kupitia ukristo na uislamu tu.
 
Unapojibu hoja niliyoitoa kwa kuyaweka mafundisho ya Kibuddha sawa na nilichosema kuhusu Yesu Kristo huku ukimalizia " ni dhana ile ile" ndipo nilipoona jitihada zako kumlinganisha Yesu na Buddha.
[
Nimelinganisha dhana, sijamlinganisha Yesu na Buddha.

Na dhana zinaweza kulinganishwa.

Kamaunakubali mafundishoya Kikristo,utakubalikwamba Yesu alijishusha kutokauungu wake pure kuja kuchanganyikana wanadamu, katika jitihada nzima ya kuwaokoa wanadamu.

Hapokuna kujishushana kuweka wengine mbelekulikowewe mwenyewe.

Kama unakubali mafundisho ya ki Buddha utaona kwamba Bodhisattvas huwa na uchaguzi wa kufundisha duniani au kupata Nirvana. Buddha aliamua kufundisha duniani.

Alijishusha. Aliweka watu wengine mbele.

There ends my comparison, of ideas. Common threads running through both life systems/ religions.
 
Ili ufaulu mtihani lazima usome kwa bidii..so ili uione pepo kuna maisha lazima upitie
Mtihani wa shule umewekwa kwa sababu.

Walimu hawana uwezo wakujua yote, hususan kujua anachojua mwanafunzi ni kipi. Hivyo, mtihani unamsaidia mwanafunzi, mwalimu na jamii nzima kujua huyu mwanafunzi anajua nini na nini hajui.

Mungu ambaye mnasema anajua yote, anajua mpaka mtu fulani ana uwezo gani na hana uwezogani, anaweka mtihani iliiweje?

Kwa nini asingefanya kwamba viumbe wake wote wanaishi peponi tu na jambo baya haliwezekani?

Alishindwa kufanya hivyo?
 
Nimelinganisha dhana, sijamlinganisha Yesu na Buddha.

Na dhana zinaweza kulinganishwa.

Kamaunakubali mafundishoya Kikristo,utakubalikwamba Yesu alijishusha kutokauungu wake pure kuja kuchanganyikana wanadamu, katika jitihada nzima ya kuwaokoa wanadamu.

Hapokuna kujishushana kuweka wengine mbelekulikowewe mwenyewe.

Kama unakubali mafundisho ya ki Buddha utaona kwamba Bodhisattvas huwa na uchaguzi wa kufundisha duniani au kupata Nirvana. Buddha aliamua kufundisha duniani.

Alijishusha. Aliweka watu wengine mbele.

There ends my comparison, of ideas. Common threads running through both life systems/ religions.

Dhana hazina nguvu kama zitatenganishwa na waliozitoa. Hakuna Buddhism bila Buddha ama Christianity bila Christ. Hakuna Marxism bila Marx.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom