BabaMorgan
JF-Expert Member
- Dec 18, 2017
- 4,045
- 10,476
Katika hali ya utafutaji imesababisha watu kutoka katika mikoa yao ya asili na kwenda mikoa ya mbali au hata nchi tofauti na walikozaliwa na kama ilivyo kwenye kutafuta wapo waliofanikisha kupata huku wengine wakiwa bado wanatafuta.
Kwa mtu ambaye yupo mbali na kwao panapotokea msiba au sherehe nyumbani kwa kawaida anatarajiwa na analazimika kushiriki kwa kuwepo eneo la tukio kwenye sherehe sio tatizo kwa kuwa linakuwa tukio lilopangwa lakini kwenye msiba inakuwa ni changamoto kwa kuzingatia wengi wetu hatuna mazoea ya kuweka akiba kwa ajili ya matukio ya dharura sasa hapa mtu ujikuta akiwa na majukumu mawili mosi ni kuchangia gharama za mazishi pili ni kushiriki kwa kuwepo.
Inapotokea mtu kushindwa kushiriki kwenye sherehe au msiba kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake katika tamaduni na Mila za kabila nini hukumu yake?