Nini hofu ya Spika Ndugai kuchukua hatua dhidi ya Wabunge kina mama 19 wanaodaiwa kuwa ni wa CHADEMA?

Hebu kila GT yeyote aitazame na kuisikiliza video clip hii ya Spika Ndugai Job mwanzo mwisho.


Umeelewa na kujifunza nini baada ya kusikiliza? Kwanini unadhani Spika wa Bunge la JMT ndg Job Ndugai anapata wakati mgumu kuchukua maamuzi sahihi kwa hawa kina mama na badala yake anapiga siasa chafu..?. Hapo nakuachia wewe msomaji..

MTAZAMO WANGU:

1. Ni wazi kuwa mtanange huu ni kati ya Bunge/Spika Ndugai vs CHADEMA na wala si CHADEMA vs Waliokuwa wanachama wake, kina mama 19 wakiongozwa na Halima Mdee.

2. Bunge la JMT ni chombo cha wananchi cha kutunga sheria na kuisimamia serikali. Linajumuisha wabunge wa makundi matano;

å Wa majimbo
å Wa viti maalumu wanawake
å 10 wa kuteuliwa na Rais
å 5 wa kuchaguliwa na BLW - Zanzibar

Kwa mujibu wa sheria zetu na katiba ya nchi, kila mbunge lazima awe amedhaminiwa (tokana) na chama halali cha siasa kilichosajiliwa kisheria.

Kazi ya Spika wa Bunge ni kuhakikisha analitazama na kulisimamia hitaji hili la kisheria na kikatiba kwa nguvu zote.

3. Sasa, kuna watu wanajiita "wabunge wa viti maalumu" wako ndani ya Bunge isivyo halali kwa sababu hawatambuliwi na chama cha siasa chochote.

Chama cha siasa kilichowadhamini, kimejitoa na hakiwatambui tena kuwa ni wanachama wake.

MASWALI YA KUONGOZA MJADALA HUU:

1. Umeitazama na kuisikiliza clip ya video hiyo hapo juu hadi mwisho? Spika Ndugai yuko sahihi? Kwa kiwango gani na kwa vipi?

2. Kwanini unadhani Spika Ndugai amegeuka kuwa wakili mtetezi wa kina mama hawa?

3. Je, ni jukumu la Bunge kumtetea mbunge aliyevuliwa uanachama wake na chama chama chake cha siasa?

4. Kama siyo jukumu la bunge, ni wapi mbunge anapaswa kwenda kutafuta haki yake ya uanachama anapokuwa na mgogoro na chama chake? Jibu ni MAHAKAMANI, au siyo jamani?

5. Kama hivi ndivyo ilivyo, je tunadhani kina Halima Mdee na wenzake hawajui hili? Na Je, Spika Ndugai hajui hili? Nini kipo nyuma ya pazia ya sakata hili?

6. Na mwisho, tujiulize. Spika Ndugai anapatwa na ugumu gani kuchukua maamuzi sahihi juu ya hawa na badala yake anazidi kulifanya jambo hili kuwa gumu na la ovyo zaidi?

7. Je, si kwamba anaogopa kufanya kosa la mwaka 2017 pale alipowafukuza ubunge wanawake 8 wabunge wa viti maalumu wa CUF kwa sababu kama hizihizi zinazowahusu hawa 19 wanaojiita wa CHADEMA?

Wote tunaelewa kuwa, Mara baada ya CUF Lipumba kuwafutia uanachama hawa wanawake 8, alipeleka taarifa kwa Spika wa Bunge la JMT na Spika haraka haraka akawatangazia kukosa sifa ya kuendelea kuwa wabunge.

Haraka haraka akaipa NEC taarifa na NEC haraka haraka kuteua wengine.

Kwa upande wa pili, hawa wabunge 8 walikimbilia mahakamani na mahakama kusitisha uamuzi wa CUF kufuta uanachama wa hawa 8 kwa muda mpaka shauri lao la msingi litakaposikilizwa.

Sote tunajua kilichotokea. Baada ya kurudi kuchukua nafasi yao bungeni, lahaula! wakakuta zimechukuliwa na watu wengine.

Kukawa na sintofahamu kiasi cha kutaka kuzua mgogoro wa kikatiba.

Je, Ndugai anaogopa hiki?

USHAURI KWA SPIKA NDUGAI:

Unaweza kufanya hivi Bwana Spika.

Washauri hao kina mama kukimbilia mahakamani ili kupata "stop order" ya maamuzi ya chama chao kuwafutia uanachama, kisha wataendelea kuwa wabunge wako.

Na wakati wakiisotea/kuipigania hiyo "stop order" mahakamani, usiwe na haraka kuipa NEC taarifa ili iteue wabunge wengine. Kwa kuwa unawahitaji sana wabunge hawa, tumia influence yako kuishawishi Mahakama kuukataa uamuzi wa CHADEMA..

Unachokifanya hiki kwa sasa ni siyo kabisa. Unanajisi katiba ya nchi yetu ukidhani kuwa unailinda...

Aidha huna audacity ya kuingilia maamuzi ya CHADEMA bila kujali walikosea ama la. Mahakama pekee ndiyo yenye mamlaka haya ya kuhoji uhalali wa maamuzi ya CHADEMA...

Washauri watu wako wafuate utaratibu huu. Ukidhani kuwa CHADEMA wataingia kwenye mtego wako huo, utakesha na mwisho wa siku ngoma lazima ikulalie wewe...!
Pascal jaribu kutoa majibu kwa maswali haya.
 
Wao kwa wao hawaelewani huko chadema mbowe anajuwa kinachoendelea ili ale ruzuku mnyika hajui chochote ndiyo maana mbowe yuko kimya hebu wajaribu kwenda mahakamani uone watakavyoumbuka hawawezi kwenda mahakamani mbowe ndio aliowaweka.

20210505_040610.jpg
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom