Nini hatma ya Zitto Kabwe katika Siasa za Tanzania?

Master Legendary

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
549
785
Wakuu nimekuwa nikimfuatilia Zitto kwa muda sasa,sasa hivi nimesikia anashiriki Uchaguzi Muhambwe wakati juzi alikuwa amesaini makubaliano na Chadema ya kupinga matokeo na kupigania Tume huru.

Mwanasiasa huyu pamoja na kwamba yuko smart kichwani ila anaonekana ni mtu hana Msimamo,kigeugeu,mnafiki,mzandiki,hatabiriki kiasi cha kutoaminika kabisa.

Alipokuwa Chadema alisikika akisema kuna Udini,Ukanda,Udikteta nk ila ukiangalia Chama chake kilivyo utaona Udini,Ukanda na Udikteta wa hali ya juu kiasi cha kujiita Nuru ya Chama.

Baada ya Uchaguzi wa 2020 kuisha alionekana kama mtu anayepinga matokeo kwa nguvu zote ghafla akaibukia kwenye Maridhiano akiwa amejificha na kumtuma Addo Shaibu.

Wakati wa Uchaguzi wa 2015 alijiita Mpinzani lakini akawa anawashambulia Chadema badala ya CCM huku watu wakiwa na Maswali mengi alipotoa Fedha za kuweka Mawakala wa ACT na Kumwaga Bendera za ACT nchi nzima.

Mwaka 2015 alionekana akishambulia UKAWA ila mwaka 2020 akaonekana kushabikia Muungano wa Upinzani

Na mengine mengi mnayafahamu yanayoonyesha undumilakuwili.

Sasa najiuliza huyu jamaa ni mwanasiasa Mzuri ingawa wengi wanadai anatumika na system,ila nini hatma yake katika Siasa za Tanzania?Hawezi kubadilishwa akawa Tunda zuri kwa Watanzania?
 
Yaani miaka yote hiyo hujamjua zito? Huyo huwa anaangalia fursa. Hakuna fursa itampitia karibu aiche hata kama anadhalilisha utu wake. Lile jina la "Joka lenye makengeza" kwenye kuzikamatia fursa lilimfaa zaidi zito kuliko chenge
 
Back
Top Bottom