Nini hatma ya Ocean Road?

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,753
7,844
Katika miaka ya hivi karibuni, nimeshuhudia mmomonyoka wa ardhi kwa kiwango cha kutisha ukingoni mwa barabara hiyo, aka barabara ya 'osheni-rodi!' hasa kwenye kile kpande kuanzia hospitali ya Aga Khan mpaka Tanganyika swimming club.

...hali hii ikiachiwa iendelee, huenda miaka kumi tu ijayo barabara hii itakuwa RIP, na bahari 'kugonga hodi kwenye ukuta wa ikulu!'. Umuhimu wa barabara hii licha ya kuwa inaelekea geti la mashariki mwa ikulu, vile vile kuna hospitali ya Ocean Road, Aga Khan na kusaidia kupunguza msongamano wa magari kutoka au kuingia city centre.

...early 80's palikuwa na kajimwendo toka kwenye ile miti ya mivinje mpaka baharini, lakini sasa mawimbi yanapiga mpaka karibia na magari, hasa hapa karibia na kona kuelekea Gymkhana.

Kabla hajasingiziwa Mw'mungu na kazi zake, ni Bora kuziba ufa, kuliko kujenga ukuta.

Wanamazingira mnatoa ushauri gani?
 
Morani75 + Fundi Mchundo + Mwikimbi

.....any idea on what to do along this beach area?........mnaweza kuweka picha angalau kuonyesha kinachoweza kufanyika...........any potential design kwa ajili ya ku-protect hii area?
 
Back
Top Bottom