Nini hatma ya kesi hizi Tanzania?

nderingosha

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
3,965
2,000
..Utawala huu unaomiliki vyombo vya dola lazima watoe hatma ya kesi hizi..vinginevyo umma utaamini walihusika kufanya madhila haya...hata kama watakuwa wametoka madarakani....

..Tuanze kujikumbusha kama ifuatavyo:


  • Tuanze na Dr.Mwakyembe na tuhuma za kupewa sumu hadi kubabuka mwili na makucha...Mengi yakasemwa..kelele zikapigwa hadi na kina Sitta..lakini polisi na DPP wakazuga uchunguzi..Mwakyembe akapelekwa India na watawala kufanyiwa detox....aliporudi akapewa uwaziri na mchezo ukaisha na watanzania wakasahau kama kawaida yao hadi leo.....Nahoji tena.. nani walihusika kumbabua Mwakyembe?
  • Ikaja issue ya Dr.Ulimboka....kudanganywa na mtu wa ikulu(kwa madai yake) na hatimae kutekwa na kuteswa mbaya porini ...mithili ya kutaka kutolewa roho...Mungu si athuman akapona ..polisi wakazuga wakakamata Mkenya wakaweka ndani...baadae ikajulikana hakuhusika..kesi mpaka leo haina majibu..na wabongo kama kawaida yao wamesahau....Nahoji tena ...nani walihusika??....


  • Ikaja issue ya kina Kubenea na Kibanda kunyofolewa kucha na kupasuliwa macho na kumwagiwa tindikali....wote wakatibiwa na dola je ya nchi na hata kutembelewa na mkulu .....lakini hadi leo hatma y kesi zao haijulikani na watanzania wamesahau kama kawaida yao....Nahoji tena .....nani walihusika??....


  • Zikaja issue mpya zilizoitwa ugaidi...makanisa yakachomwa Zenj na Dar...padri akauliwa kinyama Zenj....mabomu yakapigwa makanisani na mikutanoni Arusha na Dar..tena mabomu mengine yakarushwa mbele ya polisi....na watu wakapoteza maisha na wengine wakawa vilema...Kelele zikapigwa nchi nzima na maaskofu wakalaani na kutoa maamko makali...watawala wakaahidi uchunguzi...mabomu yakajulikana yalikotoka lakini hadi leo kimya....hakuna aliyekamatwa na kufungwa na umma kumjua...na watanzania wamesahau kama kawaida yao....na watawala kimyaaa...kama vile hamna kilichotokea.....Nahoji tena nani walihusika na madhila haya??......Inawezekanaje polisi na DPP wa taifa hili hawajakamata na kafunga wahusika wa matukio yooote haya???  • Mwisho....kukawa na kupigwa na polisi hadi kufa kwa mwandishi Mwangosi....tena akiwa kazini lakini hadi leo hamna kinachojulikana kwa mkasa huu wa kusikitisha.....na cha ajabu wakuu wa polisi waliokuwa eneo husika walipanda vyeo....Hii inatoa picha gani kwa umma??.....Majuzi amefariki kwa maradhi mwandishi Max wa mlimani TV...tumeona hadi rais katoa pole... vipi kwa mwandishi Mwangos alieuwawa kinyama mbele ya polisi???hii inatoa picha gani kwa umma??......Nahoji tena nani wahusika wa madhila haya kwa umma??....mbona alipouliwa kinyama kamanda Burlow kule mwanza wahusika walikamatwa fasta?Kuendelea kukaa kimya kwenye hatm ya madhila haya bado kutaendelea kuifanya system ionekane ilihusika....na hivyo kustahili adhabu hata kama watakuwa wameondoka madarakani....kwanini wahusika hawakamatwi..na kufungwa????

Tafakari.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom