Nini hatima ya mimi myonge wa taifa hili iwapo nitakupa nafasi ya kushika HATAMU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini hatima ya mimi myonge wa taifa hili iwapo nitakupa nafasi ya kushika HATAMU

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Eng Mayeye, May 25, 2011.

 1. E

  Eng Mayeye Member

  #1
  May 25, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi mzalendo mtanzania halisi. Nimechoshwa na kelele za marumbano zinazogonga masikio yangu kila kukicha na kila mmoja akimnyoshea kidole mwenzie kuwa ni mkosaji.. Sasa nataka uniambia wewe "NIKIKUPA DHAMANA YA KUSHIKA HATAM, UTAIFANYIA NINI NCHI YANGU NA KWA NJIA GANI ILI KUNIONDOLEA KERO ZINAZO NIKABILI?"
   
 2. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mnyonge wa taifa hili anastahili kurudishiwa heshima yake. Kupewa tena haki ya kumiliki rasilimali zake za asili,kupewa tena haki ya kufurahia miaka 50 ya uhuru kwa kupata mahitaji muhimu, kupewa tena haki anapoitafuta haki hiyo mahakamani. Kurudishiwa uwezo wake wa kuwawajibisha wale wote wanaotegemea uongozi kujinufaisha wao badala ya kutumikia wananchi.
   
 3. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2011
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Ni muhimu kwa wanyonge wote kujua kwamba heshima yao watajiletea wenyewe, haki yao watapigania na wataipata wenyewe, uwezo wa kuwawajibisha viongozi wanaojinufaisha badala ya kuwatumikia
  wanao.
  Waondoe unyonge wa fikra kwanza, hayo mengine yote yatapatikana.
  Viongozi wezi, mafisadi, wanyonyaji wanatumia unyonge wa fikra za wananchi kwa kuwatumia wananchi wenyewe kutimiza malengo yao.
   
 4. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2011
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 702
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wewe ni mtanzania au mtanganyika ?Mbona tunachanganya!
   
 5. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Ili swali niulize 2015. Hata ivo biashara asubuhi jion mahesabu. Sasa usichoke kuendelea kusikia biashara hii/siasa/harakati,mwisho utaona hesabu yenye faida jioni.
   
Loading...