Nini hatima ya demokrasia ya vyama vingi vya siasa na mtindo wa ruzuku tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini hatima ya demokrasia ya vyama vingi vya siasa na mtindo wa ruzuku tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zed, Apr 7, 2009.

 1. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2009
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Pengine nizue mjadala ambao unalenga utitiri wa vyama vya siasa nchini Tanzania. Vyama ambavyo vimekuwa haviiletei tija siasa ya Tanzania, kwa maana ya kuchagiza mabadiliko ya kweli na demokrasia ya maendeleo.
  Tanzania ina utitiri wa vyama ambavyo vinaishi kwa ruzuku tu na viongozi wake wamekuwa vibaka wa ruzuku hizi! Vyama ambavyo si vya siasa ila vyama vya ugomvi wa kung’ang’ania ruzuku na udikteta wa viongozi wapendao maslahi yao binafsi. Vyama vya namna hii vinadhalilisha siasa za vyama vingi kwa kuifanya siasa ya maficho ya viongozi matapeli wa ruzuku tu!
  Mfano hai ni malumbano ya sasa ya chama cha TLP ambayo yanatia aibu na kudhalilisha demokrasia ya vyama vingi! http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=3885 TLP kimeashindwa hata kutekeleza katiba yake yenyewe kwa sababu za ukata! ( TLP kimeshindwa hata kuitisha mkutano mkuu wa uchaguzi wenye idadi ya wajumbe wanaoelzwa katika katiba yake!) Hii ina maana kwamba chama cha TLP hakina wanachama wanaoweza kukisupport shughuli zake za kisiasa. Kwa maana hiyo basi TLP kimefilisika. Je vyama kama TLP kwa sasa si hatari kwa demokrasia ya kweli Tanzania?
  Kwa mang’amuzi (experience) ya nchi nyingine ni kwamba vyama vinavyofilisika kifedha, pia huondolewa katika ushiriki wa kisiasa kwa muda fulani vikingojea kujiweka sawa kifedha au vikishindwa baadaye hufutwa kabisa! Je si wakati muafaka wa msajili wa vyama kutangaza vyama vinavyoshindwa hata kugharimia utekelezaji wa katiba yake kuwa vimefilisika na kufutiwa usajili wake? Kwa kuwa ni vyama ambavyo havina wanachama wakuvisupport?
  Je ruzuku si chanzo cha kiburi cha vyama kutowajali wanachama na kutotafuta wanachama na kutokukusanya michango yao, bali kungojea ruzuku tu!
  Je kwanini chama kama CCM kilichoanzishwa tangu mwaka 1954 na kilicho na miradi lukuki na chenye kujigamba kuwa na mamilioni ya wanachama kiiendelee kupata ruzuku ya mabilioni? Wakati vyanzo vyake vya fedha na wanachama wake wangelitosha kabisa ku-support shughuli zake za kikazi. Labda chama hiki ni cha genge la viongozi na wapambe zao na si cha wanachama wakereketwa walio tayari kugharamia shughuli za chama chao!
  Kwanini watanzania walazimishwe kulipa kodi kufadhili vyama ambavyo si wanachama wake? Kwanini wanachama tu wasivichangie hivyo vyama?
  Hata kama vyama vitaendelea kupata ruzuku kwanini mapato na matumizi ya ruzuku ya vyama yasikaguliwe na mkaguzi mkuu wa fedha wa serikali na kuchapishwa kwenye magazeti ya serikali kila baada ya miezi 6 ili sisi walipa kodi ambao si wanachama wa vyama hivi tujue mapato na matumizi ya kodi zetu?
  Adui ya mmoja mkubwa wa demokrasia ya kweli ya vyama vingi ni RUZUKU. Vyama vya siasa vyenye dhamira na nia njema ya demokrasia ya kweli na vyenye support ya grassroots ni lazima vipinge ruzuku! Lazima watanznia tupinge ruzuku na tuwe tayari kugharamia demokrasia yetu!
   
Loading...