Embassy Hotel na Motel Agip: Nini hasa kilitokea?

MpendaTz

JF-Expert Member
May 15, 2009
2,185
884
694A9159-319D-4CC1-9B70-69CBFF47176D.jpeg

Nimekuwa naangalia jengo la iliyokuwa Embassy Hotel kwa muda mrefu sana sasa imefungwa na hakuna hata dalili yoyote ya kufufuliwa au kutumika kwa shughuli nyingine ya kibiashara.

Jengo lipo mahali pazuri sana lakini linasikitisha sana linavyochakaa na sina hakika kama linalipiwa kodo stahili kwa jiji. Kitendo cha kuliacha jengo hilo katika hali ile ni hasara kwa Taifa.

Nimejiuliza sana kuwa ni kitendawili cha aina gani hicho kimeshinda wakuu wote wa mkoa wa Dar-es salaam na mawaziri wa ardhi na mawaziri wakuu kwa muda mrefu kiasi hicho?

Kama kuna mwenye habari zozote kuhusu Embassy Hoteli na hili jengo kwa ujumla tunaomba atuwekee hapa.

Natanguliza shukrani zangu.
 
Hilo Hotel lilikuwa nzuri sana miaka ya nyuma mi wakati nilipokuwa mdogo hata la pili ilikuwa bado nzuri nakumbuka yale mandhari yalikuwa mazuri mno na Imalaseko pia ilikuwepo kipindi hicho nakumbuka kwenye mwaka 85 - 89 hivi!!

Ila kwa sasa halifai kwa biashara ya Hotel we angalia hata pale palivyo hapavutii kwa hotel,panafaa kwa shughuli nyingine lkn siyo hotel!!
 
Inasemekana katika ule mkumbo wa kuuza mashirika nayo ilipata mwekezaji anaitwa Marealle, akaingia kwenye mgogoro na wafanyakazi kuhusu stahili zao, kesi ilienda mahakamani sina hakika kama imeshaisha. Na pia taarifa zilizopo ni kwamba bwaba Marealle ni mpenzi mkubwa wa kesi nadhani watapelekeshana sana.
 
Mpenda TZ

ni kweli hii hoteli imekaa mahali pazuri saana kibiashara, kwa sasa kuna kesi nadhani ipo mahakamani,

Mwanzoni Hii hoteli ilikuwa inamilikiwa na Karmali Jumas (KJ Motors 40%, Government 40% na kibo Hotels 20%, kulikuwa na mchakato wa serekali kuziuza hisa zake kwa KJ Motors nadhani Kibo as minority share holders hawakuridhika, then wafanyakazi walikuwa wamefungua tena kesi mahakamani naamini mpaka leo shauri leo lipo mahakamani

Haya yote yanachangiwa na kuboronga kwa iliyokuwa PSRC,
 
Kama serikali imeshindwa kulimaintain basi tukabidhiwe wasanii tuibadili iwe kituo cha biashara ya utalii.
serikali itavuna mapato mengi na watalii watamiminika kwani ipo city centre na kila sanaa na products za utalii zitapatikana pale.

Just serikali haishindwi kutupatia sisi wasanii ila kwa kuwa hatuna fedha wanadhani akili zetu hazina fedha
 
Nimekuwa naangalia jengo la iliyokuwa Embassy Hotel kwa muda mrefu sana sasa imefungwa na hakuna hata dalili yoyote ya kufufuliwa au kutumika kwa shughuli nyingine ya kibiashara.

Jengo lipo mahali pazuri sana lakini linasikitisha sana linavyochakaa na sina hakika kama linalipiwa kodo stahili kwa jiji. Kitendo cha kuliacha jengo hilo katika hali ile ni hasara kwa Taifa.

Nimejiuliza sana kuwa ni kitendawili cha aina gani hicho kimeshinda wakuu wote wa mkoa wa Dar-es salaam na mawaziri wa ardhi na mawaziri wakuu kwa muda mrefu kiasi hicho?

Kama kuna mwenye habari zozote kuhusu Embassy Hoteli na hili jengo kwa ujumla tunaomba atuwekee hapa.

Natanguliza shukrani zangu.

Wakikusikia "vijana" wa mjini unaliuzia hilo jengo wataku-mind kinoma, embassy siku hizi imegeuka gesti poa, unakamta mlupo wako unaongea na mlinzi mambo shwari, kwa kawaida wenyewe wanasema huwa wanawapoza walinzi kwa buku tano, ingawa vitanda mwanzoni vilikuwa na vumbi "(kwasababu ya kutotumika) sasa hivi mambo shwari kwani walinzi wanasafisha ili "biashara" yao iende sawa. Hiyo ndio bongo bwana kila mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake, wengine wana-access ya EPA basi acha na walinzi wa embassy nao wajipatie ka-EPA kao kadogodogo.
 
ah nchi hii bana we acha tu
wameiua agip kwa sababu ya kumfurahisha moi na new africa yake.
miafrika bana we acha tu
Mkuu hapo kwenye BOLD sijakuelewa ila naona kama kuna point fulani muhimu saaaaaaaaaaana, Please iweke wazi mkuu huenda yapo mengi tusiyo yajua kuhusiana na hilo.
 
Inasemekana katika ule mkumbo wa kuuza mashirika nayo ilipata mwekezaji anaitwa Marealle, akaingia kwenye mgogoro na wafanyakazi kuhusu stahili zao, kesi ilienda mahakamani sina hakika kama imeshaisha. Na pia taarifa zilizopo ni kwamba bwaba Marealle ni mpenzi mkubwa wa kesi nadhani watapelekeshana sana.

hakuna kesi sasa, imeshauzwa.
 
Mkuu Kunta Kinte (What is your name?... Kunta Kinte (Roots))

Akina Marealle wakikusoma hapo penye bold/red watakula sahani moja na wewe!

Anywayz : Embassy Hotel ilishauzwa na yaliyobakia ni mystery : Obladi Oblada - Life Goes On

Mkuu BE kauziwa nani?? nadhani siyo siri. Kuna ujanja fulani Tanzania wakubwa hujifanya kuua biashara halafu inaaschwa inakaa muda halafu unasikia imeuzwa. Kumbe ni aliyekuwa madarakani kipindi kile kajichorea "retiirement benefits" zake binafsi. Hata hiyo Mote Agip, nina hakika uko mpango wa kifisadi hapo. Wapo wanaoujua, wamwage mchele hapa!
 
hilo jengo limesha uzwa kwa kampuni moja hivi juzi juzi na pia AGIP hotel zote zimepata new owners so let just see what they will do with the hotels will try get the link for you guys
 
Asante sana Mkuu, jinsi ambavyo disputes zinakuwa handled Tanzania inasikitisha sana. Najiuliza hizo mahakama zilikuwa zinashindwa nini kuamua hiyo kesi kwa wakati ili Hoteli iendelee kuajiri na kulipa kodi na kuliongezea pato Taifa? Huu ni mfano mmoja wa tu ipo mingi ya namna hii karibu kila Mkoa. Kwanini mahakama huwa hazipewi muda maalum wa kuhakikisha wanatolea uamuzi jambo kama hili?? Halafu busara zingekuwa zinatumika kuamua mambo kama hayo ingesaidia sana. Sasa hiyo Hotel kukaa hivyo siyo mwajiri wala wafanyakazi wamefaidika na hata Taifa pia. Kinyume chake wamepoteza fedha nyingi mahakamani. Isitoshe wamejikuta wanawachangia kwa zamu Mahakimu waliohusika na kwa kushindana. Huu ni uzembe uliokithiri Taifa lenye viongozi wenye busara haliwezi kukaa kimya na kuangalia mambo kama haya yakitokea katikati ya mji wake Mkuu! Wakati mwingine unaweza kujiuliza hivi tulidai na kupigania uhuru wa nini?? Labda ilikuwa mapema mno??
 
Back
Top Bottom