Nini haswa maana na asili ya maneno Mambo na Poa"

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
12,695
31,474
Habari za mchana wana JF,

Wakati nikiwa napambana na hali yangu nimewaza tu out of curiosity maana na asili ya maneno maarufu ya MAMBO na POA.

Mara nyingi yamekua yametumika na watu zaidi mijini ambapo kama haujui sababu za matumizi yake unaweza ukafikiri watu wanayoyatumia ni punguwani hivi.

Kimsingi, yanatumika kama salamu na majibu yake, lakini kwangu mimi salamu nadhani inatanabaisha mambo kadha wa kadha kwa yule anayesalimiwa kama: hali ya afya na usalama.

Hivyo basi, kwangu mimi nahisi haya maneno ni moja kati ya maneno ya mtaaani yaliyodumu kwa muda mrefu.

Naomba kujuzwa.
 
Salamu ya muda mrefu hasa kwa marika ya aina moja mfano vijana... Mimi yenyewe nimekua nimeyakuta yanatumika... Asili yake tuwaulize Wahenga labda

Usisahau na yale ya Shikamoo Marahaba
 
Salamu ya muda mrefu hasa kwa marika ya aina moja mfano vijana... Mimi yenyewe nimekua nimeyakuta yanatumika... Asili yake tuwaulize Wahenga labda

Usisahau na yale ya Shikamoo Marahaba
Ni kweli mkuu, tuwaulize wahenga wapya au wazamani?
 
Ilianza kama salamu ya kupromote condoms kwenye miaka ya tisini na nne hadi 95 hivi.
Kulikua na tangazo linasema, 'mambo'? Afu mdada anaitikia, 'mambo kwa soksi'. Baadaye sasa watu wakawa wanatumia kama salamu.. Mtu anakwambia, 'mambo'? Wewe unamjibu 'poa/safi'.
Thats as far as I can remember.
 
Mtu anapokuuliza mambo ni sawa na kukuuliza hali yako kiafya, na masuala mengine yanayokuhusu ikiwa yapo vizuri hayo mambo ndio unajibu poa na ikiwa tofauti basi jibu lake ni si mazuri.

Huo ni kwa mujjibu wa uelewa wangu lakini.
 
Kwa fikara zangu ni kuwa neno mambo lilitumika kama mbadala wa swali la "habari yako?" au "vipi hali yako?" na jibu tarajiwa ni "nzuri' au 'salama" n.k.....sasa vijana wa wakati huo wakafupisha swali la "vipi mambo yanaendaje?" au "mambo vipi" na kubakiza "mambo" n.k

Na jibu la poa limetoholewa kutoka jibu la kiingereza la "cool"
 
Ilianza kama salamu ya kupromote condoms kwenye miaka ya tisini na nne hadi 95 hivi.
Kulikua na tangazo linasema, 'mambo'? Afu mdada anaitikia, 'mambo kwa soksi'. Baadaye sasa watu wakawa wanatumia kama salamu.. Mtu anakwambia, 'mambo'? Wewe unamjibu 'poa/safi'.
Thats as far as I can remember.
Muhenga katika ubora wake
 
Nalikumbuka hili tangazo lakini salamu hii ilianza kabla nisawa na ilvyo mambo kwa yesu
 
Back
Top Bottom