Nini hasa tatizo la Spika Ndugai wa Bunge letu?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,793
71,206
(Copied from somewhere)

TATIZO LA NDUGAI NI LIPI?

Kama ukimuuliza Mtanzania yeyote wa kawaida sana juu ya tatizo la spika wa bunge letu tukufu ni vigumu kupata majibu sahihi. Job Ndugai amekuwa mtu wa kubadilika badilika sana kulingana na nyakati. Wapinzani naona sasa walishamjua na wakipiga ngoma lazima akate mauno. Wanamchezesha kwa tune wanayotaka wao. Wanaujua udhaifu wake vilivyo. Ni vigumu kujua kama spika huyu amekuwa naibu spika wa bunge letu chini ya maspika mahiri kama Samwel Sitta (marehemu) na mama Anne Makinda. Alipikwaje? Aliokwa, alikaangwa au alipikwa mchemsho? Hivi anaamini Watanzania wanamwelewa?

Anafikiri Tanzania ya leo ni ile ya akina Pius Msekwa? Hajui kuna matoleo ya miaka minne mtaani ya wahitimu mtaani wenye weledi sana na hawana ajira? Ni wasomi pamoja na wadogo zao na wazazi wao na wanamchora tu? Kwa sasa Watanzania hata hawahitaji runinga ili kujua yanayoendelea. Kabla hajasema maneno yake, tayari wameelewa kuwa anatumika. Tatizo kubwa la Ndugai ni udhaifu! Niliwahi kuandika makala na ikachapishwa kupitia gazeti la Tanzania Daima toleo na. 5147 la aprili 17/2019.

Hivi wapinzani ndio tatizo la nchi hii? Wamekwamisha nini ambacho ni chema? Kwa nn tusiwaapuuze na kufanya mema kufuatana na ilani ya chama cha mapinduzi? Mbona huku mtandaoni MATAGA wanatangaza kuwa CHADEMA na upinzani umekufa Tanzania? Kwa nini kuhangaika na vilivyokufa? Unawezaje kuhangaika na marehemu au ndio kujitoa ufahamu? Mimi naona upinzani una nguvu sana kipindi hiki kuliko wakati mwingine wowote ule. Badala ya serikali kupambana na maadui wa taifa letu sasa kila kukicha ni kuwasakama wapinzani. Tumezalisha kundi la wajinga ambao kucha kutwa ni kusifia tu bila kufikiri.

Wapinzani wameamua kuaondoka bungeni kwa amani kabisa na sababu wamezitoa. Kubwa ni kujitenga ili kujiepusha na corona. Hii imekuja baada wenzao kuambukizwa ugonjwa huo. Wamejipa siku 14. Ndugai kama spika mwanzo alijifaragua kuwa hatishwi na misimamo ya CHADEMA! Akadai anaendeleà na vikao vya bajeti. Hakuna mbunge wa upinzani alijibu. Walinyamaza kwa sababu wanamjua. Baada ya muda mfupi tu Ndugai amegeuka tena. Na huu ndio udhaifu!

Ameanza kuwatuhumu wapinzani kuwa wameiba pesa za umma. Mbona hakusema mwanzo? Anaanza kuwaamuru warudi bungeni au warudishe posho zao. Naamini kuna taratibu za malipo ya Wabunge ambazo Ndugai hajatwambia. Atwambie yote ili tuwazomee hawa wabunge. Amesema ni wazururaji. Tayari kila mtu ndani ya serikali kuanzia juu mpaka chini wamepoteana. Kila mtu anasema lake. I am sure wapinzani wanawajua ccm vizuri sana kuliko hata wao wanavyojijua.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, ndugu Paul Makonda naye ameingizwa ngomani. Anawataka watoke nyumbani kwake. Hapa hata hajasoma katiba inasemaje kuhusu maisha ya Watanzania na wanapaswa kuishi wapi. Hapo kwa kuwa wapinzani wanajua katiba sawasawa, wamemunanga vilivyo! Yote haya ni udhaifu wa bunge.

Acheni wapinzani wakae karantini popote ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Na ninyi endeleeni na vikao huko, naona Ndugai ameanza kuokoteza hata wabunge waliohama vyama vyao kwa hiari yao wenyewe. Kama hujui, Mwambe aliyehama CHADEMA bila kufukuzwa ameambiwa arudi bungeni. Sasa swali ni anarudi kwa tiketi ya chama gani?

Wonders will never end in this country.
 
Tatizo la Ndugai anafanya kazi kama Mwigizaji aliye live jukwaani ambae lengo lake ni moja tu: Kuifurahisha hadhira!

Ndugai nae yupo jukwaani huku akili yake ikimweleza hadhira yake ni Magufuli, na kwahiyo lengo lake ni moja tu: Kumfurahisha Magufuli.

Na amini amini nawaambia! Usikute ka Ndugai na kenyewe kana tamaa ya Urais! Na hili kufanikisha lazima awe anajikomba komba kwa Rais!

Na amini amini nawaambia... Usikute Magu nae keshamjaza ujinga Ndugai kwamba hakuna yeyote anayemuamini kudumisha ndoto yake ya Dodoma kuendelea kuwa HQ ya nchi hata baada ya yeye kuondoka madarakani zaidi ya wewe (Ndugai).
 
Tatizo la Ndugai anafanya kazi kama Mwigizaji aliye live jukwaani ambae lengo lake ni moja tu: Kuifurahisha hadhira!

Ndugai nae yupo jukwaani huku akili yake ikimweleza hadhira yake ni Magufuli, na kwahiyo lengo lake ni moja tu: Kumfurahisha Magufuli.

Na amini amini nawaambia! Usikute ka Ndugai na kenyewe kana tamaa ya Urais! Na hili kufanikisha lazima awe anajikomba komba kwa Rais!

Na amini amini nawaambia... Usikute Magu nae keshamjaza ujinga Ndugai kwamba hakuna yeyote anayemuamini kudumisha ndoto yake ya Dodoma kuendelea kuwa HQ ya nchi hata baada ya yeye kuondoka madarakani zaidi ya wewe (Ndugai).
:D :D :D :p :p :p :p :p acha nicheeeeke kwanza..
 
Kama mtu mgonjwa na mnampa power. Tatizo sio lake..


Ninawaza kwa Sauti!

Nimesoma andiko la Mheshimiwa Mbunge Tarime Mjini Easter Matiko akielezea sababu kubwa ya kutokuingia kwake Bungeni.
Ameandika, yeye alikuwa Karibu sana na Mbunge wa Sumve Richard Ndasa na walikuwa wanaonana kwa ukaribu kila siku na hata siku kabla ya Mbunge Richard Ndasa kufariki alikaa nae kiti Karibu Bungeni na kuongea kwa muda mrefu, Kesho yake Mbunge Ndasa akafariki, baadae siku hiyo anapata taarifa kuwa Mbunge Ndasa alikuwa ameathirika na ugonjwa wa COVID-19.

Mheshimiwa Mbunge Easter Matiko baada ya kupata taarifa hizo, aliamua kujifungia ndani mwenyewe asionane na Mtu yeyote huku akijitathmini afya yake. Lengo lake Kuu ni kujizuia na kuambukiza wengine kama nae atakuwa ameathirika, lakini pia ameonana na Wabunge wengine siku hiyo alipokuwa na Marehemu Ndasa, ambao wengine wamejikarantini.

Nawaza kwa sauti huo mnyororo wa aliokutana nao yeye Mheshimiwa Easter, Lakini pia Wabunge wengine waliokuwa na ukaribu na Marehemu Mbunge Ndasa kabla ya mauti yake, halafu nasoma njia ya maambukizi ya Corona virus, naenda kutafakari maamuzi ya Mheshimiwa Mbunge Easter Matiko kujifungia ndani, ninaishia kumpongeza sana na kumuona ni Kiongozi aliyejali afya ya wengine!

Mheshimiwa Spika ameendelea kuwataka Wabunge waliojifungia karantini kurejea haraka Bungeni vinginevyo amewataka kurudisha posho na anafikiria kuwakata Mishahara yao!
Ninawaza kwa sauti hivi huyu Mheshimiwa Spika anaongoza Bunge kwa kufuata Kanuni za Bunge Au anafuata fikra zake tu??!!
Adhabu ya Mbunge zinatokana na Kanuni za Bunge, Je kwa Mbunge kutohudhuria kikao cha Bunge amekiuka Kanuni ipi za Bunge??!!

Naendelea kuwaza kwa sauti, leo anapoagiza Wabunge hao warejee Bungeni na wakatii hilo na tukamuona Bungeni Mheshimiwa Matiko na ikatokea Kumbe ameathirika na Corona virus na kupelekea kuambukiza wengine, Je Spika haoni atakuwa amesababisha maambukizi kwa wengine labda hata yeye mwenyewe Spika akaathirika!??

Binafsi sioni tatizo kwa Mbunge aliyeamua kwenda Bungeni kwa kujitahadhari na Corona, vilevile naona ni busara njema kwa yule Mbunge aliyeamua kujifungia ndani kipindi hiki cha vikao hadi siku zake 14 zitakapomalizika. Shida yangu ambayo nashindwa kuelewa ni kwanini Huyu aliyeamua kujifungia ndani amekuwa kero kubwa kwa Spika hadi kila siku kutoa kauli za kiubabe??! Ni kwanini pia Wabunge wa chama tawala wanakwazika sana na kila anayesimama kujadili Bajeti anatumia dakika zake kupambana na Wabunge hao badala ya kujadili hoja za Jimbo lake na Taifa kwa ujumla??!

Vikao vilivyopita unamuona Spika akiwa bize kuwatoa Bungeni na kuwapa adhabu Wabunge hao, leo wameamua kutohudhuria vikao, nilidhani ndio angefurahi, lakini ndio amekereka kweli!! Sijui anamiss kutoa adhabu??!!

Mheshimiwa Rais katika hotuba yake alionya wanasiasa kutokutumia ugonjwa COVID-19 kisiasa, na kushauri wanasiasa wote kuwa pamoja katika kupambana na Corona Virus!
Nafikiri Mheshimiwa Spika hakumuelewa Mheshimiwa Rais! Hiki kinachoendelea sasa hivi Bungeni ni siasa tupu!

Sitaki hata kuongelea barua ya Jeshi la Police leo kuwataka Wabunge waliopo Dar na sio Dodoma Bungeni waripoti wenyewe kituo cha Polisi ikiwa ni kutekeleza agizo la RC Dar!
Kuna mambo mengine ukiyafikiria unashindwa kuelewa mawazo ya Kiongozi na kubaki kuwahurumia Polisi kwa jinsi wanavyopitia wakati mgumu wa kutekeleza maagizo ya Viongozi wenye Madaraka makubwa!

Hii ni nchi yenye watu wapole sana na wavumilivu mno na unaweza kuhisi ukiwa na Madaraka makubwa Unaweza kuwafanyia utakacho!
Nchi zilizoingia kwenye machafuko zilianza kidogo kidogo kama hivi, tuombe sana Mungu tusifike huko!
Chonde chonde Viongozi wenye Mamlaka msitumie nafasi zenu kujenga maudhi kwa wengine. Tumieni vyema ndimi zenu.

Aaah mimi ninawaza kwa sauti tu nikiwa Sina nia ya mkwaza Mtu zaidi ya kuliangalia Taifa langu lisigawanyike!

Amani ni Tunda la Haki.

Tanzania ni yetu sote 💪🏾🇹🇿
 
Ndugai alikuwa na Audit Query ya matumizi mabaya ya fedha kwenye Audit report ya 2016/17. Kama unakumbuka allazwa Hospitali ya India na kutumia Bilions kwa kuwa alikwenda na familia, nurse na mpambe tofauti na sera inataka aende na msindikizaji mmoja.

Aliporudi utakumbuka alitaka kumtunishia kidogo Jiwe kwa kumtetea Zitto Kabwe alipotaka kushikwa ndani ya Bunge. Na kwa kweli alikuwa na nia ya kutaka kusimama kama Spika Huru na Mhimili wake. Jiwe akamtishia kupitia watu wa Usalama kwa kunmuambia akiendelea kupishana naye basi atazianika kashfa zake zilizoibuliwa na CAG. Nakwamba ifikapo 2020 hawatampitisha kuwa Sipka wa Bunge instead watampitisha Tulia Ackson.

Basi baada ya hapo ikabidi asalimu amri na kuanza kumunga mkono.
 
Tatizo la Ndugai anafanya kazi kama Mwigizaji aliye live jukwaani ambae lengo lake ni moja tu: Kuifurahisha hadhira!

Ndugai nae yupo jukwaani huku akili yake ikimweleza hadhira yake ni Magufuli, na kwahiyo lengo lake ni moja tu: Kumfurahisha Magufuli.

Na amini amini nawaambia! Usikute ka Ndugai na kenyewe kana tamaa ya Urais! Na hili kufanikisha lazima awe anajikomba komba kwa Rais!

Na amini amini nawaambia... Usikute Magu nae keshamjaza ujinga Ndugai kwamba hakuna yeyote anayemuamini kudumisha ndoto yake ya Dodoma kuendelea kuwa HQ ya nchi hata baada ya yeye kuondoka madarakani zaidi ya wewe (Ndugai).
Umenikumbusha ya JK kuwaaminisha watu watano (kila mmoja kwa wakati wake) kuwa yeye ndiye afaaye kwa awamu ya 5.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom