Nini hasa sababu ya Iran kutaka kufunga strait of hormuz?

Dunia imekuwa si mahali salama sana pa kuishi kabla hata ya kuinuka kwa Marekani. Kabla ya hapo yalikuwepo pia mataifa yenye nguvu sana na yaliyatawala mataifa mengine tena kwa lazima.

Kwa hiyo si rahisi kusema kwamba kutokuwepo kwa Marekani Dunia ingekuwa salama, hapana, hata kama Marekani isingekuwepo bado kungetokea tu taifa lingine ambalo lingei-Control Dunia. Nothing Changes!
Hapana c kweli, wale walio tawala siku za nyuma, walikuwa na tawaliwa kwa kuwa walikuwa hawana viongozi wakuwaongoza, na ule ujinga ulitawala.

Kwa sasa bora tupumzike na ujinga huo, hakuna wajinga tena duniani, yani Marekani asitufanye cc wajinga.
 
Nini maoni yako kuhusu Iran kuufunga mlangi bahari wa Hormuz??? Naona watu mnalalamika tu bila kutoa maelezo yenu!!!!
Hapana c kweli, wale walio tawala siku za nyuma, walikuwa na tawaliwa kwa kuwa walikuwa hawana viongozi wakuwaongoza, na ule ujinga ulitawala.

Kwa sasa bora tupumzike na ujinga huo, hakuna wajinga tena duniani, yani Marekani asitufanye cc wajinga.
 
Ni sahihi kusema hivyo kwasababu Israel ilikiuka haki za binadam kabla .
Vipi je ye Israel anavyotapa waziwazi kuwafyeka Palestines wa Ghazar sio kosa hilo?!
Embu acheni kasumba iliyojaa ushabiki maandazi na ushabiki kisheti ndani yake.
Angalieni haki pande zote
Huwezi kutembea mitaani una jambia mkononi na unatangaza kumfyeka jirani yako harafu wananzengo wanakuangalia tu lazima itakuwa haramu kwako kutembea au kumliki Jambia vivyo hivyo Iran ilipokuwa inatengeneza silaha hizo tangazo lake lilikuwa kuifuta Israel katika ramani ya Dunia.https://www.timesofisrael.com/iran-general-says-tehran-aims-to-wipe-israel-off-the-political-map-report/
 
Hahahaha naomba kukujibu mkuu!

North Korea wana tengeneza silaha za Nuclear ili kupiga taifa la Marekani.
Iran anatengeneza silaha za nuclear ili kupiga Marekani na washirika wake.

Israel alitengeneza hizo silaha ili kujilinda dhidi ya maadui zake.
Pakistan alitengeneza kujilinda dhidi ya India ambaye ni adui yake.
India alitengeneza kujilinda dhidi ya Pakistan.

Utaona tofauti hapo juu kuna nchi zilitengeneza na zinazoendelea kutengeneza, hakuna ushahidi wa wazi hata wasiri wakuthibitisha kuwa India na Pakistan wana hizi silaha za hatari kabisa ila kuna propaganda.

Iran huwa hawezi kumshambulia Israel kwa sababu hiyo.
BTW silaha za nuclear zinauwezo wa kukuathiri hata wewe uliyeko mbwinde huko usishabikie uundwaji wake wala kuwepo kwake
mmhh
 
Unajua kama hao Israel kufutwa ni sawa tuu?!
Mkuuu nimesoma post zako dah u ar very novice Kiukweli sio utani.
Inamaana hao Israel vitisho vya kilasiku vya kuifyatua Palestines hawafanyi kosa?!
Any way...Kipindi kile cha WWII ilikuwa ni struggle for power dominance,yeyote mwenye silaha yeyote angeitumia tu ili kubaki salama,Kipindi hiki kipo tofauti kidogo,huhitaji masilaha makubwa ili ku survive,Ndo maana hata US na Russia wanajitahidi kuyapunguza.Sasa inatokea nchi fulani inataka kumiliki Nuclear hapo hapo wanaahidi kuifuta nchi nyingine kwenye ramani ya Dunia.Halafu unataka asiwepo wa kukemea?..Mfano leo Itokee nchi iseme anataka kuifuta Belarus kwenye uso wa dunia,unafikiri Russia watakaa kimya?...
 
Kumekuwa na mijadala mingi mitandaoni watu wakiongelea ubabe wa Marekani katika sakata zima la kupelekea kudunguliwa kwa Drone ya Marekani kwenye mlango bahari wa hormuz,wengi hawaelewi ni kwa nini Marekani na Iran zineingia kwenye mgogoro mkubwa kiasi cha kuanza kutunishiana misuli.

Pamoja na mambo mengine ugomvi huo unasababishwa na Irani kutaka kuufunga ,lango bahari wa Hormuz baada ya kuona inazidiwa na vikwazo ilivyowekewa tanazo hilo lilitolewa na Rais Hassan Rouhan alitoa tangazo hilo July 3,2018 kwa wasafishaji wa mafuta wote wa eneo hilo baada ya Marekani kudai kuzuia usafirishaji wa mafuta yote ya Iran wakati huo huo mafuta ya nchi zingine yatakuwa yanaendelea kupitia katika mlango bahari wa Hormuz unaomilikiwa na Iran kitendo hicho ndicho hasa kilichopelekea Iran itoe tishio la kuufunga mlango bahari wa Hormuz.

Kwa upande wa Marekani wao wanashawishi Iraniwekewe vikwazo vya kiuchumi zaidi maana inahusika na vurugu nyingi zinazoendelea huko Mashariki ya kati na Marekani inategemea vikwazo hivyo vitauzorotesha uchumi wa Iran hivyo kusababisha kubadili misimamo yao dhidi ya maslahi ya Marekani katika eneo hilo.

KWA NINI MAREKANI NA IRAN WANATISHIANA KILA MMOJA?

Mwanzoni mwa November 2017 Marekani ilirudisha vikwazo vya kusafirisha mafuta vilivyokuwa vimewekwa na JONT COMPREHESIVE PLAN OF ACTION(JCPOA)ambavyo hapo nyuma vilikuwa vimeondolewa baada ya makubaliano ambayo Marekani ilijiondoa katika mpango huo na iliwaagiza washirika wake waache kununua wala kusafirisha mafuta kutoka Iran na wakati huo huo Marekani ikiwahamasisha washirika wake wa Ghuba ya uajem wazalishe mafuta kwa wingi ili kuzipa pengo la mafuta kutoka Iran na Libya hivyo kuikosesha mapato na kodi Iran.Ndiyo maana Iran ikatoa tishio la kuufunga mlango bahari wa Hormuz.

KWA NINI WANAHUSISHA STRAIT OF HORMUZ??

Mlango bahari wa Hormuz ni njia nyembamba inayopita kwenye Ghuba ya uajemi kati ya Oman na nchi ya Iran njia inayowezesha kupita 30% mpaka 40% ya mafuta karibu mapipa Million 17 yanasafirishwa kupitia Mlango bahari wa Hormuz kila siku na meli zote za mafuta lazima zipite hapo hii ni pamoja na usafirishaji wa mafuta kutoka katika kati bandari za Iraq,Kuwait,Bahrain na Qatar na Bandari ambazo ziko kwenye Falme za Emirates pia na bandari mhimza Saudi arabia.Kwa hiyo ukitishia Mlango bahari wa Hormuz utakuwa umetishia usafirishaji wa mafuta ulimwenguni na wasafirishaji wote wa mafuta ikiwemo Marekani ambayo inategemea usafirishwaji wa mafuta salama kupitia Mlango bahari wa Hormuz



JE IRAN HAPO NYUMA ILISHAWEKA TISHIO LA KUFUNGA STRAIT OF HORMUZ?

Ni kweli kabisa 2012 Iran iliwahi kutishia kuufunga mlango bahari wa Hormuz baada ya kuona uchumi wake unazidi kudorora kwa vikwazo ilivyowekewa na Marekani na washirika wake jumuia ya Ulaya kutokana na mpango wake haramu wa kutengeneza mabomu ya Nuclear.Mkuu wa vikosi vya wanamaji wa Iran alisema ni kitu kidogo sana kufunga mlango bahari wa Hormuz ambao hawataruhusu hata tone moja la mafuta kupita hapo kama nchi yao Iran itaendelea kubanwa na vikwazo visivyoisha vya Marekani cha ajabu vikwazo viliendelea na Iran haikuweza kufunga Mlango bahari wa Hormuz.

Tofauti kubwa iliyopo kati yao ni kuwa Iran inataka mazungumzo na Marekani lakini utawala ulioko sasa madarakani hautaki kabisa mazungumzo na Iran badala yake unafanya mazungumzo na kuimarisha mahusiano na washirika wake wakiwemo Israel na Saudi Arabia ambao wanaiona Iran kama adui yao mkubwa.

JE NI KWELI KWA SASA IRAN INAWEZA KUTIMIZA AZMA YAKE YA KUFUNGA STRAIT OF HORMUZ?.

Mbali ya misimamo mikali iliyo nayo Iran kuufunga mlango bahari wa Hormuz itakuwa imefanya maamuzi yanayoweza kuibua hisia kali kwanza kutoka kwa majirani zake wanaotumia mlango bahari wa Hormuz.Pia kufunnga mlango bahari wa Hormuz kutapelekea vita vya moja kwa moja na Marekani na jumuia ya nchi za Ghuba ambazo kwa pamoja zinataka mlango bahari huo uwe huru kutumiwa na nchi zote zilizoko eneo hilo maana zinauona mlango bahari wa Hormuzi kama Moyo au mshipa wa fahamu wa eneo hilo.Hata uchumi wa Iran unategemea meli zinazopita eneo hilo hivyo kuufunga mlango bahari wa Hormuz itakuwa sana kuutia kitanzi uchumi wa Iran.na kutaharibu sna usafirishaji wa mafuta duniani ambako hata Iran yenyewe itapata hasara kubwa.

JE SASA NINI KITATOKEA?

Mlango bahari wa Hormuz ni mhimu sana kwa mataifa yote kwa maoni yangu Iran haiwezi kuufunga mlango bahari wa hormuz hata kama itabanwa na vikwazo vipi Iran inaweza tu kulipiza kisasi kwa njia nyingine inazojua yenyewe au ku-Harass meli za mafuta zinazopita hapo kama walivyofanya na wanavyofanya kwa meli za mataifa mbalimbali kushambuliwa wakiwa katika eneo hilo na mashambulizi kama hayo ni kawaida sana kufanywa na Jeshi la wanamaji wa Iran IRGC ambalo limedhibiti eneo lote la Ghuba ya Uajemi baada ya vikwazo hivyo kuwekwa 2017.
Wakati Iran inajaribu kujitutumua kwenye vikwazo Marekani nayo imeamua kuongeza vikwazo kiasi ambacho jumuia ya Ulaya wameshindwa kuihakikishia Iran usalama wa Uchumi wake hivyo kusababisha Jeshi la wanamaji wa Iran kuanza tena kuzisumbua Tanker zinazopita kwenye mlango bahari wa Hormuz kwa kuzishambulia kwa makombora na ndiyo kilichopelekea Iran kudungua Drone ya Marekani iliyokuwa kwenye anga la kimataifa kitendo kilichopelekea Marekani kutoa tishia la kuishambulia Iran shambulio ambalo liliahirishwa dakika za mwisho kitu ambacho kwa wengi walikiona kama ni uoga wa Marekani kupambana na Iran.Kitaalama Marekani isingeweza kuingia vitani na Iran kichwa kichwa bila kujipanga na kuangalia faida na hasara kwa kuingia vitani na Irani kwa vyovyote vile kungeweza sababisha kufungwa kwa Mlango bahari wa Hormuz kitendo ambacho kingeumisha washirika wake walioko eneo hilo na mataifa yote yanayofaidika na mlango bahari huo.Hivyo kwa 100% mimi nilikuwa najua Marekani haiwezi kuingia vitani na Iran na tishio hilo lililotolewa na Marekani kwa Iran kwa kijeshi linaitwa SHOW OF FORCE (yaani kujionyesha una nguvu mbele ya adui yako)tu.Iran inajitahidi sana kukomaa pamoja na kuumizwa sana na vikwazo hivyo na kutumia vikosi vyake katika eneo hilo vinajaribu sana kuondoa ukali wa vikwazo lakini bado Marekani wamewakaba shingoni.

NANI ANAFAIDIKA KATIKA UGOMVI HUU WA MAREKANI NA IRANI?

Kwa vyovyote vile atakayefaidika katika ugomvi huu ni Urusi na China wao wanaombea vita itokee hata leo ili wao waanze kufaidika kumbuka China ni nchi ambayo nayo iko juu sana kiuchumi hivyo kuingia vitani kwa Marekani lazima uchumi wake utadorora hivyo kusababisha China na Urusi kuchukua nafasi Kitu ambacho si rahisi kwa mtu yeyote kukubali.Kwa aliyekuwa anategemea vita vya Marekani na Iran hivyo asahau kabisa kutokana hali halisi niliyoielezea hapo juu.Nakaribisha maswali.!!.
Sidhani kama kona ukweli hapo
 
Kujihami na. Kuipiga nchi ni vitu viwili tofaut.
Striking and protecting yourself ni vitu mbili tofaut.
Mtu unajiweza kujihami kwa kujiwekea ulinzi madhubuti kama Iran.
Kupiga it means kama anavyofanya USA KWa Libya na kwengineko pasi na reasonable factors ila ni ulafi wa mali tyu.
Mkuu duh kajifunze kiswahili pia
Naona umeuliza na kujijibu mwenyewe kutokana na chuki kukuzidi soma hapo niliko bold na rangi nyeusi.

Kwaheri
 
Kujihami na. Kuipiga nchi ni vitu viwili tofaut.
Striking and protecting yourself ni vitu mbili tofaut.
Mtu unajiweza kujihami kwa kujiwekea ulinzi madhubuti kama Iran.
Kupiga it means kama anavyofanya USA KWa Libya na kwengineko pasi na reasonable factors ila ni ulafi wa mali tyu.
Mkuu duh kajifunze kiswahili pia
Kwanini nijifunze kiswahili?
 
Daaaah aseee Nimeamini we jamaa unaongea kishabiki.
Hivi nani anayeiharibu Palestine ukanda wa Ghazar na Jerusalem ?!
Kaka hii chai yako yamoto sana
Mtoe China, U.S na Israel hapo hawa hawana malengo ya kuharibu taifa lolote.

Ila N.K wana malengo hayo kwanini aachwe atengeneze kiongozi?
 
Namsaidia.
Kuna movie inaitwa haksaw ridge inahusiana na ww2 .
Kuna mzee mwisho wa ile movie ndiye aliyekuwa anaelezea vita ya pili ya dunia kwasababu yeye alishiriki kama muokoaji.
Alisema kwa mdomo wake"we were about to lose a war against Japan because they were too strong to us if not that atomic bomb to make them surrender all plans of USA could be down"
Asa hapo jiulize nimekuachia homework.
Which plans of USA could be down?
Na kaka ukumbuke kuwa USA ilikua ikimuuzia silaha kundi la kina Britain ,France ili kukinzana na Kina Germany,Italy na Japan.
Na walishawekeana contract vita ikiisha walipane hayo maden.
Ndio maana USA kuona maji yapo shingoni aliamua kupiga Nagasaki ili awapooze Japan maana walikua wakimwashia moto wa gesi ya oryx.
Naam mimi ni muhuni msomi! Mjasiri haachi asili I'm thug than the word thug.

Naomba nikuulize maswali mawili kama huwa unafatilia historia.
Kwanini marekani aliipiga Nagasaki?

Na kwanini Hiroshima milipuko ilitokea kwenye vinu vyao vya nuclear?
 
Sina chuki nao ila atleast acha ushabiki simama katika haki.
Hawa jamaa ni madhulumu sanaa wanaua mpk watoto wa kipalestine.
Na bora ingekuwa kidini ila wakristo na waislam wote wa ule ukanda wanamwombea mabaya huyu Israel na Netanyahu yake.
Then unasema hana haja ya kumpiga mtu ilhali anawapiga wanyonge Palestines.
Una chuki na Israel?
 
Bora azibe tu hiyo strait of hormuz ili America naye apate akili kuwa sio kila nchi anapotaka kuinyanyasa itakubali kunyanyasika kwa ulafi wake wa mali.
Maana vikwazo havina hata maana anavyoviweka dhidi ya wenzake.
Anataka yeye awakandamize wenzake atakavyo ilhali hii si sawa.
Bandiko langu in kwa nini Iran inataka kufunga Strait of Hormuz nashanga wenye vichwa vya panzi wanarukia vitu vidogodogo kuliko dhana nzima niliyoelezea kuhusiana faida na hasara za kufungwa kwa Mlango bahari wa Hormuz na akina nani watanufaika ikiwa kutatokea vita kati ya Iran na Marekani.Nilitarajia utaleta na we we maoni yako kuhusu hilo cha ajabu umekuja na Mihemko yako na chuki zako kuliko kutoa mchango wako wa mawazo ili sote tufaidike.
 
Sina chuki nao ila atleast acha ushabiki simama katika haki.
Hawa jamaa ni madhulumu sanaa wanaua mpk watoto wa kipalestine.
Na bora ingekuwa kidini ila wakristo na waislam wote wa ule ukanda wanamwombea mabaya huyu Israel na Netanyahu yake.
Then unasema hana haja ya kumpiga mtu ilhali anawapiga wanyonge Palestines.
Dua la kuku huwa halimpati mwewe! Tafuta Biblia ya agano la kale funua nyuma kabisa ya Biblia utaiona ramani ya Israel ya zamani sana ambayo ilikuja kuvamiwa na waarabu.

Hiyo ardhi ya Palestine ni ya Israel na maeneo yao wameanza kuyarudisha taratibu.

BTW sina ushabiki hata kidogo na sijawahi kushabikia vita, wananchi wa ukanda wa gaza wana sababisha wao kupigwa mabomu, sasa hivi wana uchora ukuta uliojengwa na Israel kwa maneno yao na katuni za chuki wanajua wanachokipata wanakamatwa wanapelekwa jela za israel na wanateseka mno.
 
Umeshindwaje kuichanganua tofauti kati ya kujihami na kuipiga nchi na kutamka directly jamaa kajiuliza na kujijibu mwenyewe ?!
Ummayed malengo ya Iran kutengeneza silaha za nuclear unayajua?

Malengo ya N.k kutengeneza silaha za nuclear unayaju?
Na je unafahamu athari za hizo silaha?

Najua utasema mbona U.S anazo je kila taifa likiachwa liunde silaha zake hii itakuwa dunia ya aina gani? Kumbuka Tanzania tuna madini ya uranium tunaweza kuunda pia
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom