Nini hasa sababu ya Iran kutaka kufunga strait of hormuz?

Echolima

Echolima

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2007
Messages
3,435
Points
2,000
Echolima

Echolima

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2007
3,435 2,000
Kumekuwa na mijadala mingi mitandaoni watu wakiongelea ubabe wa Marekani katika sakata zima la kupelekea kudunguliwa kwa Drone ya Marekani kwenye mlango bahari wa hormuz,wengi hawaelewi ni kwa nini Marekani na Iran zineingia kwenye mgogoro mkubwa kiasi cha kuanza kutunishiana misuli.

Pamoja na mambo mengine ugomvi huo unasababishwa na Irani kutaka kuufunga ,lango bahari wa Hormuz baada ya kuona inazidiwa na vikwazo ilivyowekewa tanazo hilo lilitolewa na Rais Hassan Rouhan alitoa tangazo hilo July 3,2018 kwa wasafishaji wa mafuta wote wa eneo hilo baada ya Marekani kudai kuzuia usafirishaji wa mafuta yote ya Iran wakati huo huo mafuta ya nchi zingine yatakuwa yanaendelea kupitia katika mlango bahari wa Hormuz unaomilikiwa na Iran kitendo hicho ndicho hasa kilichopelekea Iran itoe tishio la kuufunga mlango bahari wa Hormuz.

Kwa upande wa Marekani wao wanashawishi Iraniwekewe vikwazo vya kiuchumi zaidi maana inahusika na vurugu nyingi zinazoendelea huko Mashariki ya kati na Marekani inategemea vikwazo hivyo vitauzorotesha uchumi wa Iran hivyo kusababisha kubadili misimamo yao dhidi ya maslahi ya Marekani katika eneo hilo.

KWA NINI MAREKANI NA IRAN WANATISHIANA KILA MMOJA?

Mwanzoni mwa November 2017 Marekani ilirudisha vikwazo vya kusafirisha mafuta vilivyokuwa vimewekwa na JONT COMPREHESIVE PLAN OF ACTION(JCPOA)ambavyo hapo nyuma vilikuwa vimeondolewa baada ya makubaliano ambayo Marekani ilijiondoa katika mpango huo na iliwaagiza washirika wake waache kununua wala kusafirisha mafuta kutoka Iran na wakati huo huo Marekani ikiwahamasisha washirika wake wa Ghuba ya uajem wazalishe mafuta kwa wingi ili kuzipa pengo la mafuta kutoka Iran na Libya hivyo kuikosesha mapato na kodi Iran.Ndiyo maana Iran ikatoa tishio la kuufunga mlango bahari wa Hormuz.

KWA NINI WANAHUSISHA STRAIT OF HORMUZ??

Mlango bahari wa Hormuz ni njia nyembamba inayopita kwenye Ghuba ya uajemi kati ya Oman na nchi ya Iran njia inayowezesha kupita 30% mpaka 40% ya mafuta karibu mapipa Million 17 yanasafirishwa kupitia Mlango bahari wa Hormuz kila siku na meli zote za mafuta lazima zipite hapo hii ni pamoja na usafirishaji wa mafuta kutoka katika kati bandari za Iraq,Kuwait,Bahrain na Qatar na Bandari ambazo ziko kwenye Falme za Emirates pia na bandari mhimza Saudi arabia.Kwa hiyo ukitishia Mlango bahari wa Hormuz utakuwa umetishia usafirishaji wa mafuta ulimwenguni na wasafirishaji wote wa mafuta ikiwemo Marekani ambayo inategemea usafirishwaji wa mafuta salama kupitia Mlango bahari wa HormuzJE IRAN HAPO NYUMA ILISHAWEKA TISHIO LA KUFUNGA STRAIT OF HORMUZ?

Ni kweli kabisa 2012 Iran iliwahi kutishia kuufunga mlango bahari wa Hormuz baada ya kuona uchumi wake unazidi kudorora kwa vikwazo ilivyowekewa na Marekani na washirika wake jumuia ya Ulaya kutokana na mpango wake haramu wa kutengeneza mabomu ya Nuclear.Mkuu wa vikosi vya wanamaji wa Iran alisema ni kitu kidogo sana kufunga mlango bahari wa Hormuz ambao hawataruhusu hata tone moja la mafuta kupita hapo kama nchi yao Iran itaendelea kubanwa na vikwazo visivyoisha vya Marekani cha ajabu vikwazo viliendelea na Iran haikuweza kufunga Mlango bahari wa Hormuz.

Tofauti kubwa iliyopo kati yao ni kuwa Iran inataka mazungumzo na Marekani lakini utawala ulioko sasa madarakani hautaki kabisa mazungumzo na Iran badala yake unafanya mazungumzo na kuimarisha mahusiano na washirika wake wakiwemo Israel na Saudi Arabia ambao wanaiona Iran kama adui yao mkubwa.

JE NI KWELI KWA SASA IRAN INAWEZA KUTIMIZA AZMA YAKE YA KUFUNGA STRAIT OF HORMUZ?.

Mbali ya misimamo mikali iliyo nayo Iran kuufunga mlango bahari wa Hormuz itakuwa imefanya maamuzi yanayoweza kuibua hisia kali kwanza kutoka kwa majirani zake wanaotumia mlango bahari wa Hormuz.Pia kufunnga mlango bahari wa Hormuz kutapelekea vita vya moja kwa moja na Marekani na jumuia ya nchi za Ghuba ambazo kwa pamoja zinataka mlango bahari huo uwe huru kutumiwa na nchi zote zilizoko eneo hilo maana zinauona mlango bahari wa Hormuzi kama Moyo au mshipa wa fahamu wa eneo hilo.Hata uchumi wa Iran unategemea meli zinazopita eneo hilo hivyo kuufunga mlango bahari wa Hormuz itakuwa sana kuutia kitanzi uchumi wa Iran.na kutaharibu sna usafirishaji wa mafuta duniani ambako hata Iran yenyewe itapata hasara kubwa.

JE SASA NINI KITATOKEA?

Mlango bahari wa Hormuz ni mhimu sana kwa mataifa yote kwa maoni yangu Iran haiwezi kuufunga mlango bahari wa hormuz hata kama itabanwa na vikwazo vipi Iran inaweza tu kulipiza kisasi kwa njia nyingine inazojua yenyewe au ku-Harass meli za mafuta zinazopita hapo kama walivyofanya na wanavyofanya kwa meli za mataifa mbalimbali kushambuliwa wakiwa katika eneo hilo na mashambulizi kama hayo ni kawaida sana kufanywa na Jeshi la wanamaji wa Iran IRGC ambalo limedhibiti eneo lote la Ghuba ya Uajemi baada ya vikwazo hivyo kuwekwa 2017.
Wakati Iran inajaribu kujitutumua kwenye vikwazo Marekani nayo imeamua kuongeza vikwazo kiasi ambacho jumuia ya Ulaya wameshindwa kuihakikishia Iran usalama wa Uchumi wake hivyo kusababisha Jeshi la wanamaji wa Iran kuanza tena kuzisumbua Tanker zinazopita kwenye mlango bahari wa Hormuz kwa kuzishambulia kwa makombora na ndiyo kilichopelekea Iran kudungua Drone ya Marekani iliyokuwa kwenye anga la kimataifa kitendo kilichopelekea Marekani kutoa tishia la kuishambulia Iran shambulio ambalo liliahirishwa dakika za mwisho kitu ambacho kwa wengi walikiona kama ni uoga wa Marekani kupambana na Iran.Kitaalama Marekani isingeweza kuingia vitani na Iran kichwa kichwa bila kujipanga na kuangalia faida na hasara kwa kuingia vitani na Irani kwa vyovyote vile kungeweza sababisha kufungwa kwa Mlango bahari wa Hormuz kitendo ambacho kingeumisha washirika wake walioko eneo hilo na mataifa yote yanayofaidika na mlango bahari huo.Hivyo kwa 100% mimi nilikuwa najua Marekani haiwezi kuingia vitani na Iran na tishio hilo lililotolewa na Marekani kwa Iran kwa kijeshi linaitwa SHOW OF FORCE (yaani kujionyesha una nguvu mbele ya adui yako)tu.Iran inajitahidi sana kukomaa pamoja na kuumizwa sana na vikwazo hivyo na kutumia vikosi vyake katika eneo hilo vinajaribu sana kuondoa ukali wa vikwazo lakini bado Marekani wamewakaba shingoni.

NANI ANAFAIDIKA KATIKA UGOMVI HUU WA MAREKANI NA IRANI?

Kwa vyovyote vile atakayefaidika katika ugomvi huu ni Urusi na China wao wanaombea vita itokee hata leo ili wao waanze kufaidika kumbuka China ni nchi ambayo nayo iko juu sana kiuchumi hivyo kuingia vitani kwa Marekani lazima uchumi wake utadorora hivyo kusababisha China na Urusi kuchukua nafasi Kitu ambacho si rahisi kwa mtu yeyote kukubali.Kwa aliyekuwa anategemea vita vya Marekani na Iran hivyo asahau kabisa kutokana hali halisi niliyoielezea hapo juu.Nakaribisha maswali.!!.
 
Attachments:

neo1

neo1

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2013
Messages
549
Points
1,000
neo1

neo1

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2013
549 1,000
Kwa nini unauita mpango wa kutengeneza makombora ya nyukria ni haramu wakati Pakistan,India,Israel,North Korea anayo??

Kwa nin unasema anavuruga amani ya Mashariki ya kati wakati America na washirika ndo walianza uchokozi na vikwazo ya yeye aliona njia ya kujihami ni kuwa na vikundi vidogo vidogo kama Hamas,Hezbollah,hao wa Yemen.. Huoni pia ni mipango yake ya muda mrefu kupambana??
 
Mngoni clothes

Mngoni clothes

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2018
Messages
207
Points
250
Mngoni clothes

Mngoni clothes

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2018
207 250
Kwa nini unauita mpango wa kutengeneza makombora ya nyukria ni haramu wakati Pakistan,India,Israel,North Korea anayo??

Kwa nin unasema anavuruga amani ya Mashariki ya kati wakati America na washirika ndo walianza uchokozi na vikwazo ya yeye aliona njia ya kujihami ni kuwa na vikundi vidogo vidogo kama Hamas,Hezbollah,hao wa Yemen.. Huoni pia ni mipango yake ya muda mrefu kupambana??
Exactly
 
Dripboy

Dripboy

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2019
Messages
3,251
Points
2,000
Dripboy

Dripboy

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2019
3,251 2,000
Kwa nini unauita mpango wa kutengeneza makombora ya nyukria ni haramu wakati Pakistan,India,Israel,North Korea anayo??

Kwa nin unasema anavuruga amani ya Mashariki ya kati wakati America na washirika ndo walianza uchokozi na vikwazo ya yeye aliona njia ya kujihami ni kuwa na vikundi vidogo vidogo kama Hamas,Hezbollah,hao wa Yemen.. Huoni pia ni mipango yake ya muda mrefu kupambana??
Hahahaha naomba kukujibu mkuu!

North Korea wana tengeneza silaha za Nuclear ili kupiga taifa la Marekani.
Iran anatengeneza silaha za nuclear ili kupiga Marekani na washirika wake.

Israel alitengeneza hizo silaha ili kujilinda dhidi ya maadui zake.
Pakistan alitengeneza kujilinda dhidi ya India ambaye ni adui yake.
India alitengeneza kujilinda dhidi ya Pakistan.

Utaona tofauti hapo juu kuna nchi zilitengeneza na zinazoendelea kutengeneza, hakuna ushahidi wa wazi hata wasiri wakuthibitisha kuwa India na Pakistan wana hizi silaha za hatari kabisa ila kuna propaganda.

Iran huwa hawezi kumshambulia Israel kwa sababu hiyo.
BTW silaha za nuclear zinauwezo wa kukuathiri hata wewe uliyeko mbwinde huko usishabikie uundwaji wake wala kuwepo kwake
 
STRUGGLE MAN

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Messages
1,796
Points
2,000
STRUGGLE MAN

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
Joined May 31, 2018
1,796 2,000
Mnachekesha kweli nyie
Hahahaha naomba kukujibu mkuu!

North Korea wana tengeneza silaha za Nuclear ili kupiga taifa la Marekani.
Iran anatengeneza silaha za nuclear ili kupiga Marekani na washirika wake.

Israel alitengeneza hizo silaha ili kujilinda dhidi ya maadui zake.
Pakistan alitengeneza kujilinda dhidi ya India ambaye ni adui yake.
India alitengeneza kujilinda dhidi ya Pakistan.

Utaona tofauti hapo juu kuna nchi zilitengeneza na zinazoendelea kutengeneza, hakuna ushahidi wa wazi hata wasiri wakuthibitisha kuwa India na Pakistan wana hizi silaha za hatari kabisa ila kuna propaganda.

Iran huwa hawezi kumshambulia Israel kwa sababu hiyo.
BTW silaha za nuclear zinauwezo wa kukuathiri hata wewe uliyeko mbwinde huko usishabikie uundwaji wake wala kuwepo kwake
 
A

Adiosamigo

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2013
Messages
2,755
Points
2,000
A

Adiosamigo

JF-Expert Member
Joined Oct 2, 2013
2,755 2,000
Kamanda wa JWTZ hivi wewe uliona lini Iran kavamia jirani zake?

Iraq ndio alimvamia Iran

Saud Arabia ameivamia Yemen nchi jirani yake na warabu wenzake kabisa, eti kaenda rudisha serekali ya Yemen ya kisheria, wakati huyo Rais wa Yemen aliresign mwenyewe.

Alipo resign Yemen ikawa haiko kwenye amani ndipo pale Al Ansar Lah walipo ingia nakushika nchi.

Saud Arabia kaivamia Yemen sa alipo ona Al Ansar Lah wamemzidia nguvu, anadai Iran ndio inawasaidia, kweli hatukatai Iran anawasaidia lakini c sababu wao ni Mashia.

Al Ansar Lah wao c Mashia wao ni Mazediya kidogo wako karibu na Maibadhi kuliko Mashia, hata kuna watu wanawaita Maibadhi ni Shia c kweli.

Iran kuwasaidia wanyoge ndio zake, anawasaidia Hamasi na wakati ni Masunni na c Mashia.

Kwa hio kamanda wa JWTZ we ungemuliza USA yeye anataka nini pale ni kwake mbali, hapo c kwake.

Iran na Warabu miaka wanaishi kwa usalama aliye sababisha mchafuko ni USA.

USA akibaki kwake ni bora kwa faida ya dunia.
 
Mkuu nilitarajia utasubiri sehem ya pili uone nimeishia wapi lakini nashangaa umeanza kumchamba Tembo wakati bado zoezi linaendelea nisubiri nimalize sehemu yangu ya pili Ndiyo na we we upate picha kamili ili ufunguke vizuri!!!
 
Sawa kamanda wa JWTZ.
 
Omary Ndama

Omary Ndama

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2017
Messages
3,027
Points
2,000
Omary Ndama

Omary Ndama

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2017
3,027 2,000
Kamanda wa JWTZ hivi wewe uliona lini Iran kavamia jirani zake?

Iraq ndio alimvamia Iran

Saud Arabia ameivamia Yemen nchi jirani yake na warabu wenzake kabisa, eti kaenda rudisha serekali ya Yemen ya kisheria, wakati huyo Rais wa Yemen aliresign mwenyewe.

Alipo resign Yemen ikawa haiko kwenye amani ndipo pale Al Ansar Lah walipo ingia nakushika nchi.

Saud Arabia kaivamia Yemen sa alipo ona Al Ansar Lah wamemzidia nguvu, anadai Iran ndio inawasaidia, kweli hatukatai Iran anawasaidia lakini c sababu wao ni Mashia.

Al Ansar Lah wao c Mashia wao ni Mazediya kidogo wako karibu na Maibadhi kuliko Mashia, hata kuna watu wanawaita Maibadhi ni Shia c kweli.

Iran kuwasaidia wanyoge ndio zake, anawasaidia Hamasi na wakati ni Masunni na c Mashia.

Kwa hio kamanda wa JWTZ we ungemuliza USA yeye anataka nini pale ni kwake mbali, hapo c kwake.

Iran na Warabu miaka wanaishi kwa usalama aliye sababisha mchafuko ni USA.

USA akibaki kwake ni bora kwa faida ya dunia.
Pasipo Marekani dunia ingekuwa mahali salama Sana pa kuishi...
 
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Messages
32,002
Points
2,000
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined Jun 19, 2014
32,002 2,000
Kwa nini unauita mpango wa kutengeneza makombora ya nyukria ni haramu wakati Pakistan,India,Israel,North Korea anayo??

Kwa nin unasema anavuruga amani ya Mashariki ya kati wakati America na washirika ndo walianza uchokozi na vikwazo ya yeye aliona njia ya kujihami ni kuwa na vikundi vidogo vidogo kama Hamas,Hezbollah,hao wa Yemen.. Huoni pia ni mipango yake ya muda mrefu kupambana??
Huyu jamaa amerogwa
 
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Messages
32,002
Points
2,000
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined Jun 19, 2014
32,002 2,000
Ili kupata vichekesho kama hivi bonyeza *150*20#
Hahahaha naomba kukujibu mkuu!

North Korea wana tengeneza silaha za Nuclear ili kupiga taifa la Marekani.
Iran anatengeneza silaha za nuclear ili kupiga Marekani na washirika wake.

Israel alitengeneza hizo silaha ili kujilinda dhidi ya maadui zake.
Pakistan alitengeneza kujilinda dhidi ya India ambaye ni adui yake.
India alitengeneza kujilinda dhidi ya Pakistan.

Utaona tofauti hapo juu kuna nchi zilitengeneza na zinazoendelea kutengeneza, hakuna ushahidi wa wazi hata wasiri wakuthibitisha kuwa India na Pakistan wana hizi silaha za hatari kabisa ila kuna propaganda.

Iran huwa hawezi kumshambulia Israel kwa sababu hiyo.
BTW silaha za nuclear zinauwezo wa kukuathiri hata wewe uliyeko mbwinde huko usishabikie uundwaji wake wala kuwepo kwake
 
Otterhound

Otterhound

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2016
Messages
837
Points
1,000
Otterhound

Otterhound

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2016
837 1,000
Hahahaha naomba kukujibu mkuu!

North Korea wana tengeneza silaha za Nuclear ili kupiga taifa la Marekani.
Iran anatengeneza silaha za nuclear ili kupiga Marekani na washirika wake.

Israel alitengeneza hizo silaha ili kujilinda dhidi ya maadui zake.
Pakistan alitengeneza kujilinda dhidi ya India ambaye ni adui yake.
India alitengeneza kujilinda dhidi ya Pakistan.

Utaona tofauti hapo juu kuna nchi zilitengeneza na zinazoendelea kutengeneza, hakuna ushahidi wa wazi hata wasiri wakuthibitisha kuwa India na Pakistan wana hizi silaha za hatari kabisa ila kuna propaganda.

Iran huwa hawezi kumshambulia Israel kwa sababu hiyo.
BTW silaha za nuclear zinauwezo wa kukuathiri hata wewe uliyeko mbwinde huko usishabikie uundwaji wake wala kuwepo kwake
Waswahili hamkosagi vimaneno maneno. Punguzeni kushinda kwenye kahawa bwana 😁😁
 
FRANC THE GREAT

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Messages
1,545
Points
2,000
FRANC THE GREAT

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined May 27, 2016
1,545 2,000
Pasipo Marekani dunia ingekuwa mahali salama Sana pa kuishi...
Dunia imekuwa si mahali salama sana pa kuishi kabla hata ya kuinuka kwa Marekani. Kabla ya hapo yalikuwepo pia mataifa yenye nguvu sana na yaliyatawala mataifa mengine tena kwa lazima.

Kwa hiyo si rahisi kusema kwamba kutokuwepo kwa Marekani Dunia ingekuwa salama, hapana, hata kama Marekani isingekuwepo bado kungetokea tu taifa lingine ambalo lingei-Control Dunia. Nothing Changes!
 
Ummayed

Ummayed

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2019
Messages
3,952
Points
2,000
Ummayed

Ummayed

JF-Expert Member
Joined May 21, 2019
3,952 2,000
Hahahaha naomba kukujibu mkuu!

North Korea wana tengeneza silaha za Nuclear ili kupiga taifa la Marekani.
Iran anatengeneza silaha za nuclear ili kupiga Marekani na washirika wake.

Israel alitengeneza hizo silaha ili kujilinda dhidi ya maadui zake.
Pakistan alitengeneza kujilinda dhidi ya India ambaye ni adui yake.
India alitengeneza kujilinda dhidi ya Pakistan.

Utaona tofauti hapo juu kuna nchi zilitengeneza na zinazoendelea kutengeneza, hakuna ushahidi wa wazi hata wasiri wakuthibitisha kuwa India na Pakistan wana hizi silaha za hatari kabisa ila kuna propaganda.

Iran huwa hawezi kumshambulia Israel kwa sababu hiyo.
BTW silaha za nuclear zinauwezo wa kukuathiri hata wewe uliyeko mbwinde huko usishabikie uundwaji wake wala kuwepo kwake
Nyie jamaa vipi kuhusu china mbona anatengeneza naye mpango wake haram au?!
 
Ummayed

Ummayed

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2019
Messages
3,952
Points
2,000
Ummayed

Ummayed

JF-Expert Member
Joined May 21, 2019
3,952 2,000
Kumekuwa na mijadala mingi mitandaoni watu wakiongelea ubabe wa Marekani katika sakata zima la kupelekea kudunguliwa kwa Drone ya Marekani kwenye mlango bahari wa hormuz,wengi hawaelewi ni kwa nini Marekani na Iran zineingia kwenye mgogoro mkubwa kiasi cha kuanza kutunishiana misuli.

Pamoja na mambo mengine ugomvi huo unasababishwa na Irani kutaka kuufunga ,lango bahari wa Hormuz baada ya kuona inazidiwa na vikwazo ilivyowekewa tanazo hilo lilitolewa na Rais Hassan Rouhan alitoa tangazo hilo July 3,2018 kwa wasafishaji wa mafuta wote wa eneo hilo baada ya Marekani kudai kuzuia usafirishaji wa mafuta yote ya Iran wakati huo huo mafuta ya nchi zingine yatakuwa yanaendelea kupitia katika mlango bahari wa Hormuz unaomilikiwa na Iran kitendo hicho ndicho hasa kilichopelekea Iran itoe tishio la kuufunga mlango bahari wa Hormuz.

Kwa upande wa Marekani wao wanashawishi Iraniwekewe vikwazo vya kiuchumi zaidi maana inahusika na vurugu nyingi zinazoendelea huko Mashariki ya kati na Marekani inategemea vikwazo hivyo vitauzorotesha uchumi wa Iran hivyo kusababisha kubadili misimamo yao dhidi ya maslahi ya Marekani katika eneo hilo.

KWA NINI MAREKANI NA IRAN WANATISHIANA KILA MMOJA?

Mwanzoni mwa November 2017 Marekani ilirudisha vikwazo vya kusafirisha mafuta vilivyokuwa vimewekwa na JONT COMPREHESIVE PLAN OF ACTION(JCPOA)ambavyo hapo nyuma vilikuwa vimeondolewa baada ya makubaliano ambayo Marekani ilijiondoa katika mpango huo na iliwaagiza washirika wake waache kununua wala kusafirisha mafuta kutoka Iran na wakati huo huo Marekani ikiwahamasisha washirika wake wa Ghuba ya uajem wazalishe mafuta kwa wingi ili kuzipa pengo la mafuta kutoka Iran na Libya hivyo kuikosesha mapato na kodi Iran.Ndiyo maana Iran ikatoa tishio la kuufunga mlango bahari wa Hormuz.

KWA NINI WANAHUSISHA STRAIT OF HORMUZ??

Mlango bahari wa Hormuz ni njia nyembamba inayopita kwenye Ghuba ya uajemi kati ya Oman na nchi ya Iran njia inayowezesha kupita 30% mpaka 40% ya mafuta karibu mapipa Million 17 yanasafirishwa kupitia Mlango bahari wa Hormuz kila siku na meli zote za mafuta lazima zipite hapo hii ni pamoja na usafirishaji wa mafuta kutoka katika kati bandari za Iraq,Kuwait,Bahrain na Qatar na Bandari ambazo ziko kwenye Falme za Emirates pia na bandari mhimza Saudi arabia.Kwa hiyo ukitishia Mlango bahari wa Hormuz utakuwa umetishia usafirishaji wa mafuta ulimwenguni na wasafirishaji wote wa mafuta ikiwemo Marekani ambayo inategemea usafirishwaji wa mafuta salama kupitia Mlango bahari wa HormuzJE IRAN HAPO NYUMA ILISHAWEKA TISHIO LA KUFUNGA STRAIT OF HORMUZ?

Ni kweli kabisa 2012 Iran iliwahi kutishia kuufunga mlango bahari wa Hormuz baada ya kuona uchumi wake unazidi kudorora kwa vikwazo ilivyowekewa na Marekani na washirika wake jumuia ya Ulaya kutokana na mpango wake haramu wa kutengeneza mabomu ya Nuclear.Mkuu wa vikosi vya wanamaji wa Iran alisema ni kitu kidogo sana kufunga mlango bahari wa Hormuz ambao hawataruhusu hata tone moja la mafuta kupita hapo kama nchi yao Iran itaendelea kubanwa na vikwazo visivyoisha vya Marekani cha ajabu vikwazo viliendelea na Iran haikuweza kufunga Mlango bahari wa Hormuz.

Tofauti kubwa iliyopo kati yao ni kuwa Iran inataka mazungumzo na Marekani lakini utawala ulioko sasa madarakani hautaki kabisa mazungumzo na Iran badala yake unafanya mazungumzo na kuimarisha mahusiano na washirika wake wakiwemo Israel na Saudi Arabia ambao wanaiona Iran kama adui yao mkubwa.

JE NI KWELI KWA SASA IRAN INAWEZA KUTIMIZA AZMA YAKE YA KUFUNGA STRAIT OF HORMUZ?.

Mbali ya misimamo mikali iliyo nayo Iran kuufunga mlango bahari wa Hormuz itakuwa imefanya maamuzi yanayoweza kuibua hisia kali kwanza kutoka kwa majirani zake wanaotumia mlango bahari wa Hormuz.Pia kufunnga mlango bahari wa Hormuz kutapelekea vita vya moja kwa moja na Marekani na jumuia ya nchi za Ghuba ambazo kwa pamoja zinataka mlango bahari huo uwe huru kutumiwa na nchi zote zilizoko eneo hilo maana zinauona mlango bahari wa Hormuzi kama Moyo au mshipa wa fahamu wa eneo hilo.Hata uchumi wa Iran unategemea meli zinazopita eneo hilo hivyo kuufunga mlango bahari wa Hormuz itakuwa sana kuutia kitanzi uchumi wa Iran.na kutaharibu sna usafirishaji wa mafuta duniani ambako hata Iran yenyewe itapata hasara kubwa.

JE SASA NINI KITATOKEA?

Mlango bahari wa Hormuz ni mhimu sana kwa mataifa yote kwa maoni yangu Iran haiwezi kuufunga mlango bahari wa hormuz hata kama itabanwa na vikwazo vipi Iran inaweza tu kulipiza kisasi kwa njia nyingine inazojua yenyewe au ku-Harass meli za mafuta zinazopita hapo kama walivyofanya na wanavyofanya kwa meli za mataifa mbalimbali kushambuliwa wakiwa katika eneo hilo na mashambulizi kama hayo ni kawaida sana kufanywa na Jeshi la wanamaji wa Iran IRGC ambalo limedhibiti eneo lote la Ghuba ya Uajemi baada ya vikwazo hivyo kuwekwa 2017
Itaendelea.................
Americans ni ma a**holes.
Asa mbona yeye anaunda hzo atomic bombs na kuzuia wenzake?!
Mbona mataifa ya Ulaya yanaunda atomic bombs au nazo zao ni halal hawana haram?!
Hawa majamaa nawachukia wallahi wanabahati sikulelewa usomalini ningejiunga na kina Faridad kuwatia mboko
 
Forum statistics

Threads 1,315,687
Members 505,368
Posts 31,867,125
Top