Nini hasa kinafichwa bunge letu kutoonyeshwa live? Kama ni muda wa kazi, basi Tv zote ziwe hewani kuanzia saa 9:30 alasiri

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,791
3,360
Ninaenda kwenye uchaguzi Mkuu 2020 bila kujua mchango wa Mbunge wangu bungeni.

Bunge live lilisaidia wengi kutathmini japo sio kwa asilimia zote uimara wa Wabunge wetu kifikra.

Awali, aliyekuwa Waziri wa Habari alitoa tamko kuwa Bunge Live muda wa kazi linafanya watu waache kufanya kazi za ujenzi wa Taifa.

Hoja hii haina mashiko ya kutosha kwani Tv zinarusha matangazo mengineyo muda wa kazi!

Hapa ni nani anadhibiti kuona watazamaji hawaangalii na wanafanya kazi za kujenga Taifa?

Kwanini iwe kwa Bunge tu huku Isidingo ikirushwa saa tatu au saa tano asubuhi?
 
Mkuu unataka kuwaona wabunge live, kwani wabunge sasa hivi wanapatikana bowa njia ya kura? Au Magufuli ndiyo anaamua nani atangazwe mshindi au apite bila kupingwa? Mkuu sisi tuombe tu wazungu waendelee kukata misaada na mikopo yao ili kuichosa hii serikali dhalimu.
 
Back
Top Bottom