Nini hasa kilisababisha vurugu za Mwembechai mwaka 1998?

Pole sana... Kama Upanga ni bush mwembechai sijui panaitwaje.mi sioni tatizo la wao kuukana uungu wa Yesu. Suala ni kuwa kuna wahuni walidanganywa wakapata kipigo kibaya sana...hawajataka kurudia tena uhuni...si ndo mambo ya kibiti hayo unasahau? CCM ipo makini sana na wapuuzi kadhaa wanaotaka kutumika.sasa njoo na wewe na Jini mtaka damu uone serikali itafanyaje 😁😁😁😁
Sio walitest mitambo, walitaka Ruhusa ya kukana Uungu wa Yesu na wakapewa na Mahakama kuu, enzi hizo ulikuwa bush
 
Madhaifu ya serikali ilikuwa kuachia mihadhara ya kukashifu dini nyingine mwislamu kusemaYesu si Mungu sio kosa kwa imani yake ila linaweza kugeuka kosa kama atatoa kauli ileile kwa nia ya kukashifu kama ataitoa kwa nia ya kukashifu wakiristo
 
Pole sana... Kama Upanga ni bush mwembechai sijui panaitwaje.mi sioni tatizo la wao kuukana uungu wa Yesu. Suala ni kuwa kuna wahuni walidanganywa wakapata kipigo kibaya sana...hawajataka kurudia tena uhuni...si ndo mambo ya kibiti hayo unasahau? CCM ipo makini sana na wapuuzi kadhaa wanaotaka kutumika.sasa njoo na wewe na Jini mtaka damu uone serikali itafanyaje 😁😁😁😁

Nyinyi Makafiri mlifurahi sana waislamu waliopigania uhuru kuuawawa ndani ya nyumba yao ya ibada.
 
Mauaji ya Mwembechai ni ya kidini.
Mapambano kati ya polisi na Waislamu:
Waliokufa sasa ni wawili
Ulinzi waimarishwa magerezani
Majira ya Jumapili Na. 1505 February 15
IDADI ya watu waliouawa kufuatia mapigano kati ya polisi na waumini wa dini ya Kiislamu katika msikiti wa Mwembe Chai jijini, imefikia wawili baada ya mtu mmoja aliyekuwa amelazwa hospitalini Muhimbili, kufariki dunia jana usiku.
Habari kutoka wodi namba tisa Kibasila ambako majeruhi wamelazwa zinasema mtu huyo ambaye jina lake halijafahamika mara moja alifariki jana usiku mara baada ya kufikishwa wodini hapo.
Wengine waliolazwa katika wodi hiyo ni pamoja na mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Kiislamu ya Al-Haramaini iliyopo Mtaa wa Lindi Ilala, Chuki Kipambano (17) ambaye alijeruhiwa kwa risasi mgongoni na kifuani.
Katika wodi hiyo pia kuna mtu mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Hassan Mtiani (32) mkazi wa mtaa wa Sikukuu Kariakoo jijini.
Bw. Mtiani ambaye pamoja na kujeruhiwa kwa risasi kwenye mguu wa kushoto, alikuwa akiendelea kuhubiri kitandani kwake. Hata hivyo, baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika wadi hiyo, walikuwa wakimbeza Bw. Mtiani kwa kumwita 'mtangaza dini'.
Habari zaidi kutoka Hospitalini hapo, zilisema kwamba jina la mtu aliyeuawa juzi na polisi limetambulika kuwa ni Saleh Issa (30) mkazi wa Tandale Jijini.
Katika tukio jingine Mwandishi Wetu Tumaini Mwaijenge anaripoti kuwa jeshi la Magereza limelazimika kuimarisha ulinzi wa magereza yake matatu yaliyopo jijini kufuatia tishio lililotolewa na Waislamu wenye msimamo mkali wa kutaka kuwatoa viongozi wao waliokamatwa kutokana na kashfa za kidini.
Gazeti hili lilishuhudia askari wa Kikosi Maalumu cha Kuzuia ghasia Magerezani (KMKGM), kikivinjari katika gereza la Keko, wilayani Temeke na askari wengine wakiwa kwenye Gereza Kuu la Ukonga na lile la Segerea.
"Hakikisheni hakuna mtu yeyote anayesogelea gereza bila ya kazi maalum. Jukumu la ulinzi liko mikononi mwenu", alisikika Kamishna Mkuu wa Jeshi hilo, Bw. Onel Malisa akiwaambia askari hao alipokuwa katika ukaguzi wa usalama wa magereza hayo, usiku wa kumkia jana.
Katika ziara hiyo ya Bw. Malisa, alikuwepo pia Mkuu mpya wa Magereza wa mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Ahmed Shangiri ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa mkuu wa chuo cha Magereza cha Ukonga.
Tukio jingine lililovuta hisia za askari katika gereza la Keko ni kuona watuhumiwa hao wa kike, wakiingia gerezani hapo bila kuwa na nguo za ndani walipopekuliwa.
Walipoulizwa ni kwa vipi wote hawajavaa nguo zao za ndani, walidai kuwa walilazimika kuzivua kutokana na kuwashwa na mabomu ya machozi yaliyovurumishwa na polisi katika jitihada za kuwatawanya kutoka katika msikiti huo wa Mwembe Chai.
Naye Nelly Mtema anaripoti, kwamba Bw. Christopher Mtikila anayejiita Mchungaji wa Taasisi ya Liberty Desk amepinga kitendo cha polisi kuwashambulia na kuwaua waumini wa Kiislamu wa Msikiti wa Mwembechai jijini na kusema kuwa kitendo hicho kinakiuka uhuru wa kuabudu.
"Kuwa na uhuru wa kuabudu, lazima kila kundi liwe na uvumilivu katika kuvumilia maneno ya wenzake na tulikubaliana hivyo pale Karimjee sasa nguvu ya dola imetoka wapi?" alihoji Mchungaji Mtikila.
Ni dhahiri kuwa mauaji ya Waislamu yamefanywa na serikali isiyo na dini lakini ikawa inatii kanisa.
Nukuu nyingine inayoonyesha kuwa mauaji yale ni ya kidini, kwa vile kanisa limeishinikiza serikali na kuwa mtandao mzima wa serikali una harufu ya kanisa zaidi kuliko taifa ni pale serikali na chama tawala kinyume na ubinadamu, Waziri mkuu ameripotiwa akisema Serikali sasa imeamua kwa dhati kupambana na watu wanaokashfu dini" (majira). CCM nayo imewapongeza polisi na kuelekeza J.W.T.Z. litumike kupambana na vurugu za kidini. ( Mtanzania Na 706 la Ijumaa Februari 20/1998 linatuelimisha zaidi.)
KUFUATIA VURUGU ZA MWEMBECHAI
JWTZ ruksa kutumia risasi kuzima ghasia zote za kidini
Na Mwandishi wetu
VIKOSI vya ulinzi na usalama vimeelekezwa kutumia risasi za moto kuzima ghasia za kidini iwapo kufanya hivyo, itakuwa ndiyo njia pekee ya kulinda amani ya walio wengi, imefahamika.
Habari zilizopatikana serikalini, zimeeleza kuwa hayo, yalikuwa maazimio ya mkutano wa kamati ya Ulinzi na usalama pamoja na Kamati Kuu ya CCM iliyokutana mjini dodoma na kujadili matukio yaliyosababishwa na Waislamu wenye imani kali wa Msikiti wa Mwembe Chai, Dar es Salaam wiki iliyopita.
Kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM amesema kuwa hiyo imekuja kufuatia wasiwasi wa serikali kwamba lipo kundi la vijana wa Kitanzania waliopewa mafunzo rasmi ya kuleta na kuendeleza ghasia za kidini.
Alisema pia kuwa serikali ina wasiwasi kwamba vurugu zilizotokea katika msikiti wa Mwembe Chai zinachochewa na mataifa ya nje na zinaweza kukua iwapo serikali haitachukua hatua madhubuti.
"Risasi za moto zitatumika tu. Kwa sababu hekima iko wapi kama utaona vurugu hizo zinaweza kusababisha vifo vya watu 200, ukaacha kumpiga mmoja kusalimisha wengi?" alidadisi kiongozi huyo aliyetaka jina lake lisiandikwe gazetini.
Hata hivyo, alisema kuwa risasi hizo hazitawalenga watu wote, bali wale viongozi watakaoonekana kuwa mbele katika vurugu hizo.
Kiongozi huyo, alisema kuwa yeye binafsi anapingana na kauli ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alfred Gewe aliyoitoa hivi karibuni kwamba polisi waliwapiga risasi kwa bahati mbaya wale waliofariki.
Alieleza kuwa polisi hawakuwa na njia yoyote ya kufanya isipokuwa kuwapiga risasi za moto viongozi wa vurugu hizo kwa sababu bila hivyo vurugu hizo zisingekoma. Alisema hata misahafu inasema kuwa ukimpiga mchungaji kondoo watatawanyika.
Aidha, kiongozi huyo alisema kuwa nchi nne za Mashariki ya Kati zinashukiwa kuhusika katika ghasia na mihadhara ya dini ambayo imesababisha maafa na uharibifu katika eneo la Mwembe Chai.
Majira la Jumamosi Aprili 4, 1998, inasema:
...CCM yaunga mkono polisi
Na Rachel Lugoe
KAMATI Kuu ya Chama cha Mapunduzi (CCM) imeipongeza serikali kwa uamuzi wake wa kufunga kwa muda Msikiti wa Mwembe Chai jijini na kuweka ulinzi mkali wa Polisi na Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) katika eneo hilo.
Tamko la kamati hiyo kuhusu tukio la Mwembechai la Machi 29, mwaka huu, iliyotolewa jijini jana na Idara ya Uenezi ya chama hicho, limesema hatua kama hizo pia zichukuliwe kwa misikiti mingine yote inayoeneza vurugu na uchochezi nchini.
Uamuzi wa kuunga mkono hatua za Serikali ulitolewa baada ya kikao cha Kamati hiyo iliyokaa Aprili mosi mwaka huu kilichoongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Benjamin Mkapa ambapo pamoja na mambo mengine, vurugu za Msikiti wa Mwembechai zilijadiliwa.
Kuhusu CCM kuelekeza kutumia JWTZ, gazeti la Rai Na. 225, Alhamisi Februari 19-Februari 24/1998 linaripoti hivi:
BAADA YA POLISI, FFU KUPATA TAABU MWEMBECHAI
Jeshi sasa kupambana na wanaofanya vurugu
Laanza mazoezi kujiandaa
Ni uamuzi wa CCM
Na Mwandishi Wetu
MAFUNZO maalum ya kukabiliana na vurugu nchini, yameanza ndani ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na habari za uhakika zinaeleza kuwa mafunzo hayo yanafuatia vurugu zilizozuka katika msikiti wa Mwembe chai Alhamisi iliyopita.
Habari za kuaminika kutoka Chama cha Mapinduzi CCM na serikalini, zimethibitisha kuwa uamuzi wa kulitaka jeshi kuanza kujiandaa kupambana na ghasia za namna hiyo ulifikiwa katika vikao vya wiki iliyopita vya CCM vilivyofanyika Dodoma.
Vikao hivyo ni vya Kamati Kuu pamoja na Kamati ya Ulinzi na Uslama ya chama hicho. Vikao hivyo vyote vilifanyika chini ya mwenyekiti wa kamati hizo mbili, Rais Benjamin Mkapa ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM.
Habari hizi baadae zilikanushwa vikai na serikali.
Habari hizi za kukanusha kutumia jeshi nazo zimeripotiwa na magazeti kadhaa. Kujikanganya kwa serikali na chama kunatia mashaka makubwa juu ya kauli ya kuitegemea.'




My take:Kila kitu kina mwisho wake na utajibu ulichotenda uwekwe panapostahili!
Bora uue mbu ili wengine wasipate malaria
 
Kwangu uonevu mkubwa wamefanyiwa waislam ni kutokusikilizwa hata humu ndani watu hawataki kusikiliza upande wa waislam wana hoja gani,ni kulaumiwa tu
Sababu kuna uhusiano wa karibu kati ya uislamu na ugaidi ,na uislamu ni janga sana hapa duniani...ndo maana sehem ambapo kuna uislam mwingi basi ujue kuna matukio ya kigaidi mengi
 
Unaposema waislam kuskilizwa unamaanisha nini?

Wakatholic nao wakitaka waskilizwe?
Waprotestant nao wakitaka kusikilizwa?
Waislam nao wanataka waskilizwe
Wasabato nao wanataka kusikilizwa
Wapagani nao wanataka kusikilizwa

Nchi itakalika hii?

Hii nchi haina dini ila wananchi wake wana dini

Dini inaishia kwenye nyumba yako ya ibada ukitoka hapo wewe ni mtanzania
Waislam wanapenda kulia lia sana,afu wanajikutaga speeeshooo sana
 
Mauaji ya mwembechai yalikuwa ni kilele cha kilio cha waislamu juu ya ubaguzi dhidi yao wa siri na dhahiri katika nyanja nyingi hususan elimu na ajira serikalini, Serikali ya Mwalimu haikufanya vya kutosha kubridge gap kati ya Wakiristo waliokuwa na advantage kielimu toka wakati wa mkoloni. Hata shule za Kanisa ambazo Nyerere alitaifisha kwa hoja kwamba Watanzania wote wasome haikusaidia kwa sababu gepu la kielimu liliendelea. Na badala ya Nyerere kujenga shule mpya nyingi yeye alitaifisha zilizokuwepo ambazo bado ziliendelea kuwa chache na ndiyo maana watoto walikuwa wakifaulu primary school hawachaguliwi kutokana na uhaba wa shule za Sekondari.

Viwango na idadi ya waislamu chuo kikuu ilikuwa ni ndogo sana na serikali ya Nyerere na ya Mwinyi ambayo iliendelea kuwa under watch kali ya Nyerere kama Mwenyekiti wa CCM hadi mwaka 1990 haikuweza kuaddress tatizo hili.

Mkapa alivyoingia madarakani alikuta tatizo hili limefikia peak, mihadhara ilikuwa ni sehemu mojawapo tu ya waislamu kufikisha grievences zao kwa serikali.
Mkapa akaona atoe kile chuo cga TANESCO morogoro kuwapa waislamu ili kupunguza gepu na kilio hiki cga waislamu kuwa marginalized kwenye elimu.

Alipoingia JK akafanya kazi nzuri sana ya kujenga shule za kata kila nchi, kwa hiyo waislamu wakaweza nao kuaoma kwa wingi na pia JK akapandisha hadhi vyuo vya advanced diploma na kuvifanya vitoe digrii kwa hiyo katika mazingira haya huwezi kuwabagua tena waislamu.
Katika ishu ya teuzi, Kikwete alijirahidi kuteua teua na waislamu kwa wingi kidogo ijapokuwa wakiristo overall waliendelea kuwa wengi.

Alipoingia Magufuli, amejaribu kurudisga nyuma mafanikio haya ya kubalance demography za taifa katika utumishi wa serikali.Teuzi za Magufuli zinanuka Udini.
Proportiaonally ukiangalia idadi ya ma RAS, MaDAS, Wakuu wa wilaya, Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Mashirika ya Umma, Mawaziri, Manaibu Waziri, Wenyeviti wa Bodi Waislamu ni wachache mno kulinganisha na proprtion yao katika hii nchi.
Kitila mkumbo kabla hajaenda CCM aliandika makala juu ya hili akasema ni muhimu kwa kiongozi kubalance demography za kitaifa ktk utumishi wa serikali.
Magufuli aishukuru sana BAKWATA na Sheikh mkuu, hawa wamekuwa kama nguzo yake kuu katika kutuliza munkari wa waislamu, lakini kiukweli lazima ukweli usemwe Teuzi za serikali y awamu ya tano zinanuka udini.

Na kama akishinda uchaguzi ujao akaendeleza teuzi za hivi basi ajue matatizo mengi ya utawala wake kupigwa vita sababu mojawapo ni yeye kushindwa kubalance force za demography kwenye watu wa kumsaidia kazi. Akimarginalize watu ajue pindi anapohitaji force za kumuunga mkono anaweza asizipate na kibaya zaidi inajenga chuki kali kwa wananchi ambao wanahisi wanatengwa
Sasa kama waislam wengi wamekimbia umande wanashindia elimu akhera watapataje uteuzi kwa ratio sawa na wakristo ambao wamesoma sana,labda wapate teuzi za kwenye dini yao
 
Nina alama kubwa kichwani kwa vurugu zile nusu nife,hadi leo sijui ule ujasiri niliutoa wapi,kwa ile hali nilioiona kipindi kile uonevu ukizidi ipo siku nchi hatakalika,nakumbuka kuna mtu alianguka miguuni kwangu,tulimsogeza huku anavuja damu tukaanza kupiga manati huku tunavuja damu,tulikamatwa kufikishwa kituoni hospital hawatupelek tuliuwasha moto mpaka tukaanza kufungwa dawa mlemle ndani,binafsi nimewasamehe ila kila nikikumbuka lile tukio huwa nachoka sana,nilikuwa nipo form two Azania,jion nakuwa madrasa kwimba street na kujichanganya mwembechai
 
Sio tuu nilikuwa nafanyia kazi DTV, I was the reporter in a line of fire. Kwa vile Mkuu Maalim Mohammed Said yeye ameandika hii kitu kwa urefu, tumtumie yeye.
P
Mkuu Paskali nakumbumbuka vema nilikushuhudia nyuma ya camera by the time nilikua nasoma shule moja maeneo ya Ubungo na nikiishi Upanga nakumbuka siku hiyo shella beach lilipitia Mwenge kutokea Kimara kuelekea kivukoni maana pale mwembe chai palikua hapapitiki
 
Mkuu Paskali nakumbumbuka vema nilikushuhudia nyuma ya camera by the time nilikua nasoma shule moja maeneo ya Ubungo na nikiishi Upanga nakumbuka siku hiyo shella beach lilipitia Mwenge kutokea Kimara kuelekea kivukoni maana pale mwembe chai palikua hapapitiki
Shella beach ndio lile liliandikwa Acapulco ?
 
Nina alama kubwa kichwani kwa vurugu zile nusu nife,hadi leo sijui ule ujasiri niliutoa wapi,kwa ile hali nilioiona kipindi kile uonevu ukizidi ipo siku nchi hatakalika,nakumbuka kuna mtu alianguka miguuni kwangu,tulimsogeza huku anavuja damu tukaanza kupiga manati huku tunavuja damu,tulikamatwa kufikishwa kituoni hospital hawatupelek tuliuwasha moto mpaka tukaanza kufungwa dawa mlemle ndani,binafsi nimewasamehe ila kila nikikumbuka lile tukio huwa nachoka sana,nilikuwa nipo form two Azania,jion nakuwa madrasa kwimba street na kujichanganya mwembechai
Duuuuuuh poleeeh sana Jah akusaidie na akuweke maisha marefu, nimeumia mnoooh
 
Pinda ana kauli yake kua wapigwe tu maana hamna namna.. haiwezekani nchi bdo maskin watu kutwa nzima kubishana mambo ya dini yalioletwa na wageni toka mataifa ya mbali
 
Back
Top Bottom