Nini Hasa huwa kinakukera kwa mwanamke/mwanaume je hutumia mbinu zipi kumrekebisa Bila kumfanya ajisikie vibaya? ?

KAKADO

JF-Expert Member
Nov 8, 2012
230
336
Habari wanajamvi na Heri ya pasaka,wakati dunia inaendelea na mapambano dhidi ya Covid-19 sio vibaya tukaendelea kuchukua taadhari ikiwemo kutokuwa na mitoko isiyoyalazima,tutumie muda mwingi nyumbani kama ambavyo tumekuwa tukishauriwa na Wataalam wa afya.

Wanajamvi kukaa huku nyumbani kumenipa tafakuru hasa kutaka kufahamu ni jambo gani hasa huwa ni kero kutoka kwa mwenza/mpenzi wako na je huwa unatumia mbinu zipi kumrekebisha? ??
Binafsi nilikuwa na kero zifuatazo kutoka kwa wifi/shemeji yenu.

1.Kupigwa mzinga.wadada wa siku hizi unamtongoza leo tayari anakuamishia matatizo ya ukoo mzima,hili huwa linakera sana unagundua hapo hakuna mapenzi ni ushenzi,njia pekee ninayotumia bila kuwaudhi ni kula ganzi yani najizima data kama sio mimi mdogo mdogo namuachia manyoya na kamwe hatafutwi maisha.

2.Alikuwa muongeaji na mropokaji.hili jambo lilikuwa ni kero kwangu yani ilikuwa tukiwa kwenye mtoko wa jumuiya ya watu wengi yeye ilikuwa lazima afanye namna uwepo wake uonekane,anakuwa muongeaji sana sana.

Nilimrekebisa kwa kumtania nilimuita tarumbeta ya kijiji kila ninapoona dalili zakuanza kupitiliza kuongea nilitumia code ambayo mimi na yeye pekee tulikuwa tunaelewana nilifanya hivi kumtunzia heshima bila kumzalilisha.

3.kuzidisha chumvi kwa mboga..asee hili lilikuwa tatizo kipindi cha mwanzo wa ndoa yetu,sikuelewa tatizo ilikuwa nini nilipata tabu kumuelewesha Kwa useriously nikaamua kutumia mzaa, ilikuwa ikifika muda wa chakula namtania umefika muda wa kula chumvi hahahaha utani ulizaa matunda mwisho wa siku chumvi ikapungua.
4.Pale Kati kuwa gogo....hii ilikuwa changamoto mtoto wakichaga alikuwa ajui mambo kabisa kwa sababu nilimtoa UZI sikushangaa,nilikuwa naleta utani kumtania na kumfundisha taratibu we sasa hivi naomba poo wacha nisiseme sana mambo yachumbani haya mabaharia hamkawii kuiba:D:D:D:D

Wanajamvi tuambie kipi hasa nichangamoto kutoka kwa mwanamke/mwanaume au mchepuko wako? Ni njia ipi hasa huwa unaitumia bila kumuudhi? ?
 
Ha ha ha ha Tarumbeta la kijiji, Nawaza ulikua unamuita hvyo kabisa ama kwa namna tofaut na hyo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha nilikuwa natumia password tulikuwa tunaelewana wawili tu,ila chumbani nilikuwa namchana live naona leo tarumbeta ya kijiji limepigwa vyakutosha,anacheka ila ujumbe ulikuwa unafika hahaah
 
Back
Top Bottom