JoJiPoJi
JF-Expert Member
- Aug 8, 2009
- 2,907
- 3,261
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza aaga dunia.
===
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza (55) amefariki dunia. Taarifa ya serikali imeeleza kuwa alikuwa hospitali akisumbuliwa na tatizo la moyo.
Serikali ya Burundi imetangaza kifo cha Rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunziza (55). Mshtuko wa moyo umetajwa kuwa chanzo cha kifo chake.
Imeelezwa alilazwa Hospitali Jumamosi na alikuwa anaendelea vizuri hadi Jumatatu ambapo hali yake ilibadilika ghafla na jitihada za madaktari kuokoa maisha yake hazikufanikiwa.
Rais Nkurunziza alizaliwa Desemba 18, 1964 na ameongoza nchi hiyo kuanzia mwaka 2005 (takribani miaka 15) hadi mauti ilipomfika.
Serikali imesema kutakuwa na kipindi cha maombolezo ya kitaifa kwa siku saba na bendera zitapepea nusu mlingoti.