Nini faida ya viwanja vya Mnazi Mmoja?

Nkungulume

JF-Expert Member
Nov 25, 2015
2,988
1,209
Wana jamvi habari za kushinda,

Nimejaribu kujiuliza sijapata jibu kuhusu uwepo wa viwanja vya mnazi mmoja. Nikikumbuka huko nyuma viwanja vya mnazi mmoja ilikuwa ni sehemu nzuri sana ya kupumuzikia kulikuwa na viti vya kukalia lakini vitu hivyo vyote viko wapi sasa.

Kulikuwa na kibwawa kidogo ambacho kilikuwa kinavutia kwa maji yaliyokuwemo katika bwawa hilo lililokuwepo mnazi mmoja na samaki wakicheza cheza.

Lakini ilikuwa ukienda kituo cha posta ya zamani upande wa bahari kulikuwa na eneo la kupumuzika huku ukiangalia vyombo vinavyopita baharini na huku ukiburudika na upepo wa bahari. Lakini kwa sasa maeneo yote hayo hayapo.

Wahusika shughulikieni mambo haya.
 
Hapa kazi tu... Hio ni Kazi ha makonda na mayor.. Makonda alitumi masaa matano kuongea na wanadarisalama na akaweka mikakati.. Hafi sasa hivi sijaona tofauti ya Makonda na Said Mek.
Haluna tofauti kabisa...
Naona tu maisha magumu sukari imepanda bei.. Brt ni ya JK .. Na kilichobadilika labda ni heading za magazeti wakiuza sura daily.
 
Bustani+ya+Mnazimmoja.jpg
 
Mbona eneo la forodhani Zanzibar lipo na linatumika vizuri tu mkuu
Wazenji ni wastaarabu sana. Forodhani pale na mji mkongwe pangekuwa ni hapa Dar ingekuwa balaa. Lakini watu wanaenda jioni, wanakula na kunywa then kesho ukija ni pasafi.
 
Unaweza ukailaumu manispaa lakini pia sisi wenyewe wananchi tupo mbali sana na msamiati unaoitwa ustaarabu.......yaani ilifikia kipindi mpaka watu wazima na akili zao wanajisaidia haja kubwa juu ya yale mabenchi......wengine usiku wanapageuza kuwa pahala pa kufanyia ufska na umalaya wa kila aina.......mtu anatoka na mfuko wa taka taka anakwenda kutupa pale...mpaka pakawa dampo lisilokuwa rasmi.........

Kiukweli sis wananchi tunashida sana....sijui tumekumbwa na nini...maana kuna baadhi ya mambo sio mpaka uende darasani ni wewe kutumia akili yako.....

Sasa mtu na akili yako unathubutu vipi kunya juu ya benchi ambalo asubuhi ya kesho yake unahitaji ukae hapo kwa mapumziko.......

Mimi nadhani ni bora wapafunge vile vile mpaka pale tutakapo elewa maana ya kuwa wastaarabu......
 
Pana stahili kufunguliwa na watu kuruhusiwa kupumzika waajiriwe watu wa kusafisha kila siku na pia wawepo walinzi kila siku.
Kweli kabisa wahusika wanatakiwa walifanyie kazi jambo hili
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Unaweza ukailaumu manispaa lakini pia sisi wenyewe wananchi tupo mbali sana na msamiati unaoitwa ustaarabu.......yaani ilifikia kipindi mpaka watu wazima na akili zao wanajisaidia haja kubwa juu ya yale mabenchi......wengine usiku wanapageuza kuwa pahala pa kufanyia ufska na umalaya wa kila aina.......mtu anatoka na mfuko wa taka taka anakwenda kutupa pale...mpaka pakawa dampo lisilokuwa rasmi.........

Kiukweli sis wananchi tunashida sana....sijui tumekumbwa na nini...maana kuna baadhi ya mambo sio mpaka uende darasani ni wewe kutumia akili yako.....

Sasa mtu na akili yako unathubutu vipi kunya juu ya benchi ambalo asubuhi ya kesho yake unahitaji ukae hapo kwa mapumziko.......

Mimi nadhani ni bora wapafunge vile vile mpaka pale tutakapo elewa maana ya kuwa wastaarabu......
Kama kutakuwa na ulinzi wa kutosha nadhani vitendo kama hivyo haviwezi kufanyika
 
Maisha ya dar es salaam hapo zamani yalikuwa waki ishi watu waungwana wenye nidhamu lkn sasa ohhh kila tabia za ajabu zipo , nenda ubongo kwenye daraja lile jipya kaone vituko pale vya uchafu na mikojo.inasikitisha sn
 
Back
Top Bottom