Nini faida ya kuremba kwa gharama kubwa makaburi ya wapendwa wetu?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Kuyaremba ninakomaanisha hapa ni kuyaweka nakshi nakshi za kila aina, Mbwembwe nyingi, kuyapiga Picha na Kuwaringishia Watu Mitandaoni mpaka kutaka hata kuyawekea Taa na AC ndani yake.

Na kinachonishangaza na kuniachia Maswali mengi ni pale ninapoona Msiba fulani Kaburi linafanyiwa Mbwembwe zote hizi ambazo zinatumia Gharama Kubwa na Marehemu akishazikwa tu Dhiki inaanza Kuiandama Familia yake.

Kama kuna tofauti ya Marehemu anayezikwa Kikawaida tu na Yule anayezikwa kwa Mbwembwe katika Makaburi yao tofauti naomba nijulishwe / nielimishwe kwani huenda hawa ambao Makaburi yao yanajengwa kwa Mbwembwe ndiyo Mwenyezi Mungu huwahi kuwapokea na Kuwasamehe upesi Dhambi zao walizozifanya wakiwa Hai duniani.
 
Ayubu 14:21
Wanawe hufikilia heshima, wala yeye hajui; Kisha wao huaibishwa, lakini yeye hana habari zao.
 
Sometimes it might be a manifestation of guilt.

Unakuta kuna mtu alikuwa hayupo in good terms na marehemu mpaka anafariki.

Sasa ile guilt ya kutomuona tena, inamfanya afanye jambo ambalo litamsaidia ku expiate hayo maumivu au majuto aliyokuwa nayo.kwa marehemu kwa kuamini atapata amani kutokana na kitendo hicho.

Other times, God knows best... unakuta ni udhaifu wetu tu wa kibinaadamu na kukosa upeo. Inaweza kuwa ni show off, inaweza kuwa ni zawadi ya wanafamilia kwa marehemu....
 
Back
Top Bottom