Nini dawa ya vidonda vya koo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini dawa ya vidonda vya koo

Discussion in 'JF Doctor' started by ktman2, Jul 1, 2011.

 1. k

  ktman2 Member

  #1
  Jul 1, 2011
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninapokunywa soda ama bia baridi huwa nasuburiwa na vidondo vya koo, Wana JF nini dawa yake?
   
 2. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,714
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  usinywe soda na bia ya baridi
   
 3. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 27,696
  Likes Received: 2,784
  Trophy Points: 280
  Usile wala kunywa vitu vya baridi.
   
 4. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 10,355
  Likes Received: 1,304
  Trophy Points: 280
  usinywe soda na bia baridi... then observe kama tatizo bado litakuwepo..
   
 5. wende

  wende JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2011
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 683
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Achana na vitu nyote nya baridi yaani vyakula na vinywaji. Na kama hali hiyo ikielendelea kuwepo,basi tumia vidonge vya Ampicilin & VitaminB kwa pamoja.
  Mtalaam atakuelezea dosage yake.
   
 6. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,531
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Karibu jamvini.

  Kama itakupa moyo tuko na wengine wenye shida kama yako. Epuka hivyo vitu vya baridi.
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,003
  Likes Received: 3,609
  Trophy Points: 280
  Tiba ya vidonda vya koo

  chukua Vitunguu maji kiasi kumi au vinane, uviponde halafu Uchanganye na maji kiasi kikombe cha chai kimoja Ukoroge viziru Uvichuje halafu Unywe vijiko vitatu kila siku asubuhi, mchana na jioni vijiko vitatu.

  Au tumia Dawa hizi zitakusaidia
  Jinsi ya kutibu vidonda vya kooni:
  • Sukutua maji ya chumvi yaliyo vuguvugu
  • Mumunya dawa za koo, usiwape watoto inaweza kumnyonga akimeza kwa bahati mbaya.
  • Muulize mfamasia wako akuuzie kipulizo (spray) cha kutuliza uchungu kooni.
  • Ikiwa koo linawasha au limekauka, pumua mvuke wa maji moto itakusaidia.
  Please Give me your feedback.
   
 8. faszar

  faszar Member

  #8
  Feb 28, 2014
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Je matonsis dawa yake ni nini?
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2014
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,003
  Likes Received: 3,609
  Trophy Points: 280
  Tonsil husababishwa na sababu nyingi . Pia husababishwa na upungufu wa white blood cells katika mwili ambazo cells hizi ndio hupigana na vidudu vyote venye kuleta maradhi ndani ya mwili sasa vinaposhindwa kufanya kazi lymph zinavimba na husababisha Tonsils.

  Kila mtu na ukuwaji wake wa mwili, wapo ambao wanapata tonsils kwa kunywa maji ya baridi ambayo maji ya baridi huwa ni moja katika chanzo cha kupata tonsils, mavumbi huchangia vile vile pilipili na vitu vikali kama vile embe mbichi limau pia huwa ni sababu kuu ya kupata tonsil.

  Wakati unapokuwa na tonsils muhimu zaidi kuacha maji ya baridi na vitu vyote vikali, zaidi utumie maji ya moto.

  Dawa za tonsils ni : kama ni mtumiaji wa dawa za chemicals basi epincilin inasaidia sana kuondosha tonsils.

  Dawa nyengine ambayo mimi binafsi naipendelea hii zaidi kwani inafanya kazi mara moja : Kamua ndimu moja katika glass yako kisha tia maji ya Uvugvugu (warm water) na baadae tia vijiko vinne vidogo vya asali na kijiko robo cha chumvi kuroga uzuri na unywe pole pole

  Dawa nyingine ya tonsils ni
  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni.

  Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia.

  Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako.

  Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafanya kazi na mdomo uko wazi basi pia unaweza kuumwa na Tonsils.

  Vile vile kutoka nje kwenye joto kisha ukaingia pahala baridi huwa inasababisha Tonsils na maradhi mengine kama flu na kuumwa na kichwa..n.k
   
Loading...