Nini dawa ya jirani mkorofi

pilau

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
1,593
443
:bange:Umepakana na jirani ambaye kwa macho tu anaonekana ni mwenye majvuno na visenti vyake uchwara....mnaishi uswahilini...... hafungui kioo cha gari yake tinted akirudi.... akitoka yale yale, watoto wake amewakataza kusalimia watu na hata kucheza na watoto wenzake... ni jirani asiyependa mawasiliano ya aina yoyote........ nini dawa yake:israel:
 
Hapo sasa sioni ukorofi wake nini, unataka akuchekee uanzishe uhusiano wa kumkopa??

sasa hapo anakupunguzia nini na kabla hajamia ulikau unapata nini ambacho huyo amekichukua hapo wewe ndio MKOROFI umezoea majungu ndio maana unapata shida sana juu yake acha KERO sio za maendeleo pole
 
Ndiyo maisha aliyojichagulia usilazimishe kumzoea ikiwa hakuna unachohitaji kwake zaidi ya ujirani na urafiki sioni kama kuna sababu yeyote ya kuona ama kuhisi vibaya ,maadam majirani wengine waliokuzunguka wapo angalia mwingine anayekubali na kupenda urafiki uwe naye karibu
 
Watu hatufanani kila mtu ana tabia yake na unaweza ukamwona mtu yuko hivyo ndivyo alivyo lelewa we uwe mpole.
 
Huyu mleta mada anapenda umbea na bla bla !! Watanzania tunasomeka katika ramani ya dunia kama watu wapenda Blaa blaa ndio watu kama wewe mnaojenga Hoja Hiyo kimataifa!!
 
1.kwa macho tu anaonekana ni mwenye majvuno, 2.visenti vyake uchwara, 3.hafungui kioo cha gari yake tinted, 3.watoto wake amewakataza kusalimia watu na hata kucheza na watoto wenzake, 4.ni jirani asiyependa mawasiliano ya aina yoyote

Mkuu Pilau, mbona sioni kosa lolote alilokukosea?
 
Ngoja nikupe mf.kuna jirani yangu kama 600m kutoka kwangu alikuwa anadharau majirani zake kisa ana vijicent hawasalimii akavamiwa na majambazi mara ya 1,na 2 anapiga yowe hamna anayetoka wala kumsaidia akauwawa mtu humo ndani hakujifunza mara ya 3 alianza mwenyewe kwenda kwa majirani nakuwasakimia bila kujigamba akavamiwa mara ya 4 watu wakamsaidia kwa makelele hakuibiwa.sasa pilau mwache akifiwa akipata tatizo atakuja kwa magoti huwezi kuzika mwenyewe ati
 
Last edited by a moderator:
endelea na shughuli zako, na wala usimwombee mabaya, na hata akifikwa na mabaya fanya tu yakupasayo na atajifunza saana!
 
endelea kumuombea ili afanikiwe zaidi ahame na mtaa aende kwa wenye hela wenzake hapo ndo utakuwa mwisho wa matatizo

ule msemo wa mpende jirani yako kama nafsi yako ndo majaribu yake hayo
 
Kama mnaishi uswahilini lazima ajichanganye!! Otherwise watu wa uswazi wanajua namna ya kudeal naye!!
 
Dawa ya bishoo ni kuwa bishoo zaidi yake..!!
Sasa unaweza ukawa huna VIWALO vya kumzidia ubishoo!

Neylu

Ha! ha! ha! .... umenikumbusha kitu hapa

Kuna polisi walimkamata mhalifu ... polisi akajigamba akamwambia jamaa "Si unajifanya f.ala sio! ... sasa mimi ni f.ala zaidi yako"

N.B:

MODS Neno f.ala sio tusi ... hata kwenye kamusi ya TUKI lipo

f.ala nm [a-/wa-] (si rasmi) imbecile, unwise, unreasoning, witless,
 
:bange:Umepakana na jirani ambaye kwa macho tu anaonekana ni mwenye majvuno na visenti vyake uchwara....mnaishi uswahilini...... hafungui kioo cha gari yake tinted akirudi.... akitoka yale yale, watoto wake amewakataza kusalimia watu na hata kucheza na watoto wenzake... ni jirani asiyependa mawasiliano ya aina yoyote........ nini dawa yake:israel:

Mnunulie creti la bia Zambezi uone uwezo wa bia kumaliza migogoro mkuu....
 
:bange:Umepakana na jirani ambaye kwa macho tu anaonekana ni mwenye majvuno na visenti vyake uchwara....mnaishi uswahilini...... hafungui kioo cha gari yake tinted akirudi.... akitoka yale yale, watoto wake amewakataza kusalimia watu na hata kucheza na watoto wenzake... ni jirani asiyependa mawasiliano ya aina yoyote........ nini dawa yake:israel:

Hayakuhusu. Chukua time yako.
 
Sasa unaweza ukawa huna VIWALO vya kumzidia ubishoo!

Neylu

Ha! ha! ha! .... umenikumbusha kitu hapa

Kuna polisi walimkamata mhalifu ... polisi akajigamba akamwambia jamaa "Si unajifanya f.ala sio! ... sasa mimi ni f.ala zaidi yako"

N.B:

MODS Neno f.ala sio tusi ... hata kwenye kamusi ya TUKI lipo

f.ala nm [a-/wa-] (si rasmi) imbecile, unwise, unreasoning, witless,

Unaogopa ban balaa. Sasa kama neno la kawaida si ungeandika "****" badala ya kuweka vidoti!
BTW nimecheka
 
Watu wanapenda sana ujuamaa!!! wewe huna shughuli zako ? siyo kila mtu ni rafiki au jamaa yako, achana naye na wewe fanya mambo yako.
Mleta maada unataka urafiki sababu mnakaa jirani? hiyo siyo sababu!!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom