Pole sana mama mwenzangu,natumaini wenye elimu watakuja kutupa darasa,juzi kuna dawa moja niliagiziwa famasi ya apetite jina limenitoka ila ina mtoto anapiga mpira wa blue hivi,unaweza ijaribu.hebu tupeane uzoefu mama mwenzangu,wewe wampa milo ipi?ana uzito gani?wa kikie au kiume?ameanza kutembea?ana meno?dah watoto wana mengi na hawafanani,all in all ni raha kuwahudumia
Msiwape watoto dawa kwa sababu ya chakula. Its not safe for children. Mpe mtoto dawa pale tu inapolazimu kwa sababu kila dawa ina side effects...
Jaribu kumpa unga wa maini uliosagwa.
Ila chonde chonde mwanao atakula sana mpaka wazazi mtamshangaa.
Ukiwa tayari ni Pm nikuelekeze jinsi ya kuandaa.
Habari zenu wapendwa?!
Nna mtoto ana mwaka mmoja sasa, jamani ni mateso hataki hata kidogo kula nimetumia kila mbinu lakini nimekwama. Nimpe dawa gani ili awe anakubali kula?
dada
mwanangu na miezi tisa, alikua hataki kula,akila vijiko viwili tu anabana mdomo,nikimlazimisha kula anatapika mpaka alivyovila juzi, nimpeleka kwa maspecialist wooote wa watoto amepimwa kila kitu,wamesema hana tatizo lolote,nilianzia kwa dk massawe,nikaenda kwa dk hameer,nikaenda hindu mandar,nikaenda tmj,nimemaliza pesa kwa madaktari jamani hadi na mimi nikaanza kukonda,mtoto alizidi kupoteza uzito mpaka akabaki kilo tano just imagine mtoto wa miezi tisa ana kilo tano. sasa mama mkwe wangu akaniambia nimpeleke kwa wachina, nikampeleka wachina wakampima vipimo vyoooote jibu likawa hilo hilo(HANA TATIZO LOLOTE) NILICHANGANYIKIWA.
mama akaniambia nimpeleke tianjin(pale msasani mwisho kwa wachina) nikampeleka nikawaelezea wakaniambia mtoto anatakiwa apate calcium(vitamin D3) tena wakaniambia ni tatizo la watoto wengi sana now days, wao wanatengeneza calcium powder yani ni kama lishe tu inauzwa 45,000/= nikanunua namkorogea mtoto kwenye maji kila siku nampa,its only a week tangu nimeanza kumpa mtoto hiyo calcium ila anamabadiliko makubwa analilia chakua yani anakula mpaka nafurahi. tena hata kama huna hela ya kumnunulia calcium walinishauri nikaushe mifupa ya samaki niisage halafu nihakikishe kila siku asubuhi anakunywya kijiko cha chai kimoja cha unga wa mifupa ya samaki ulichangwanywa na maji au maziwa.
pili mama aliniletea dawa fulani insuch ni multvitamin inaitwa ELYDAC SYRAP, ina vitamin D3 nayo nampa kila siku kijiko kimoja na inapatikana phamarcy.hii nayo inamsaidia kupata apetite maana ina calcium ndani.
if its useful niPM nikupe more details maana mwanangu sasa hata uzito unongezeka
Mie wa kwangu ana miaka 6 anasumbua kula huyo, chakula anachokijua ni chips na soseji. Siku akizinduka atakwambia anataka pilau yaani kazi kweli vyakula vingine hana habari kabisa!
Nisadie naelezo na mimi hiyo ELYDAC SYRAP nina mdogo wangu ana mtoto ana mwaka na mwez moja ila anasumbua kula sana na pia mtoto hatembei hawa hajaanza kutembea tumetembea hospitar sana huku mkoan ila wanasema hana ugonjwa kinachomfanya kutotembea ni uzito mdogo sio sir inasikitisha sanadada mwanangu na miezi tisa, alikua hataki kula,akila vijiko viwili tu anabana mdomo,nikimlazimisha kula anatapika mpaka alivyovila juzi, nimpeleka kwa maspecialist wooote wa watoto amepimwa kila kitu,wamesema hana tatizo lolote,nilianzia kwa dk massawe,nikaenda kwa dk hameer,nikaenda hindu mandar,nikaenda tmj,nimemaliza pesa kwa madaktari jamani hadi na mimi nikaanza kukonda,mtoto alizidi kupoteza uzito mpaka akabaki kilo tano just imagine mtoto wa miezi tisa ana kilo tano. sasa mama mkwe wangu akaniambia nimpeleke kwa wachina, nikampeleka wachina wakampima vipimo vyoooote jibu likawa hilo hilo(HANA TATIZO LOLOTE) NILICHANGANYIKIWA....