Nini chaweza mfanya mtoto apende kula?

shamali

Senior Member
Jul 6, 2013
186
56
Habari zenu wapendwa?

Nna mtoto ana mwaka mmoja sasa, jamani ni mateso hataki hata kidogo kula nimetumia kila mbinu lakini nimekwama. Nimpe dawa gani ili awe anakubali kula?
 
Pole sana mama mwenzangu,natumaini wenye elimu watakuja kutupa darasa,juzi kuna dawa moja niliagiziwa famasi ya apetite jina limenitoka ila ina mtoto anapiga mpira wa blue hivi,unaweza ijaribu.

Hebu tupeane uzoefu mama mwenzangu,wewe wampa milo ipi?ana uzito gani?wa kikie au kiume?ameanza kutembea?ana meno?dah watoto wana mengi na hawafanani,all in all ni raha kuwahudumia
 
Pole sana mama mwenzangu,natumaini wenye elimu watakuja kutupa darasa,juzi kuna dawa moja niliagiziwa famasi ya apetite jina limenitoka ila ina mtoto anapiga mpira wa blue hivi,unaweza ijaribu.hebu tupeane uzoefu mama mwenzangu,wewe wampa milo ipi?ana uzito gani?wa kikie au kiume?ameanza kutembea?ana meno?dah watoto wana mengi na hawafanani,all in all ni raha kuwahudumia

Kwa kwel ana kg za kumtosheleza mana ana kg 11 na meno anayo mengi tu, meno 12. Kwa kuwa hapend kula sn nampa uji wa lishe, mtori na maziwa tu pamoja na kunyonya. Asante kwa ushaur ntaenda itafuta hiyo nijaribu
 
Msiwape watoto dawa kwa sababu ya chakula. Its not safe for children. Mpe mtoto dawa pale tu inapolazimu kwa sababu kila dawa ina side effects.

Watoto wanaoaxcha kunyonya na kuanza kula vyakula mchanganyiko hujenga tabia ya kukataa kula iwapo wataanzishiwa kula vyakula vitamu. Inashauriwa mtoto aanze na vyakula kama mboga za majani kabla ya kuanza kumpa vitu vyenye ladha ya sukari. Pia sio vizuri kumpa vyakula vya aina nyingi kwa muda mfupi. Inafaa umuanzishie chakula fulani several days halafu ndio unakuja kingine, akizoea unakuja kingine etc.

In your case. Jaribu kutokumlisha kwa ratiba maalum. Mpe ale pale anapohitaji na sio pale ratiba inavyohitaji, muda mwingi chakula chak kiwepo and now and then unajaribisha kumpa. Unaweza kucatch kipindi fulani anakula vizuri tu.

Saa ya kumlisha usiweke mazingira rasmi kama kumvalisha epron etc, mwache ale kama anacheza huku akiwa around vifaa vyake vya kuchezea.

Njia nyingine ni kumkutanisha na watoto wenzake na kuwalisha kwa pamoja kama mchezo.

Pia jifanyie analysis wewe mzazi. Wakati mwingine mtoto anakula kwa kawaida kiwango kinachomtosha, ila mzazi ndio anataka kumlisha zaidi ya mahitaji ya mtoto. Kumbuka kuwa familia nyingi zenye kipato cha kati na juu zinawalisha watoto kiasi kikubwa kuliko mahitaji yao, which is not good for child health.
 
usihangaike na madawa ndugu anza kukaangia mayai ya kienyeji marakwa mara yanaongeza apetite ya kula me wangu alikuwa anasumbua lakini saiv ni balaa unamuwekea sahani ya chakula kuiingia chumbani ukirud ameifuta!pia badiisha njia za kumlisha unamwacha anacheza unampa kidogo anaenda akirudi unampa tena hvyhvy mpk anamaliza.IMALASEKO WANAYO MAYAI YA KIENYEJI WANAUZA .
 
Msiwape watoto dawa kwa sababu ya chakula. Its not safe for children. Mpe mtoto dawa pale tu inapolazimu kwa sababu kila dawa ina side effects...

Du umetoa bonge la ushauli sina mtoto but hili tatizo huwa nawasikia kina mama wengi wanalalamika nikikutana na hii Case ntatumia ushauli wako.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Da! kweli watu tofauti mwanangu mie anakula mpaka anasema shiba! sa hivi ana mwaka mmoja na miezi nane(8) ana kilo 17 na bado ananyonya bado miezi 4 aache,na anakula hachagui chakula wala aina ya matunda liwe tango, chungwa, embe, papai twende,Kitu cha msingi kwako asiwe na ratiba ya peke yake tu ya kula wakati nyie watu wazima mnakula pia mnamjumuisha na yeye anakuwa na plate yake, na kwa umri wake huyo wako bado anatakiwa awe ananyonya!(jibu unalo).

Ushauri wangu mpe uji wa lishe na viazi mviringo vya kulost,mboga za majani pia matunda pia ktk muda wa chakula watu wazima nae pia anawekewa sahani yake anakula mwenyewe huku pia ukimsaidia kumlisha.
 
Watu wazima mnapokula na mtoto mle nae, mwaweza mpatia chakula chake katika sahani yake. Ila ukimuwekea ratiba ya peke yake anakataa.
 
Mie wa kwangu ana miaka 6 anasumbua kula huyo, chakula anachokijua ni chips na soseji. Siku akizinduka atakwambia anataka pilau yaani kazi kweli vyakula vingine hana habari kabisa!
 
Habari zenu wapendwa?!
Nna mtoto ana mwaka mmoja sasa, jamani ni mateso hataki hata kidogo kula nimetumia kila mbinu lakini nimekwama. Nimpe dawa gani ili awe anakubali kula?

dada
mwanangu na miezi tisa, alikua hataki kula,akila vijiko viwili tu anabana mdomo,nikimlazimisha kula anatapika mpaka alivyovila juzi, nimpeleka kwa maspecialist wooote wa watoto amepimwa kila kitu,wamesema hana tatizo lolote,nilianzia kwa dk massawe,nikaenda kwa dk hameer,nikaenda hindu mandar,nikaenda tmj,nimemaliza pesa kwa madaktari jamani hadi na mimi nikaanza kukonda,mtoto alizidi kupoteza uzito mpaka akabaki kilo tano just imagine mtoto wa miezi tisa ana kilo tano. sasa mama mkwe wangu akaniambia nimpeleke kwa wachina, nikampeleka wachina wakampima vipimo vyoooote jibu likawa hilo hilo(HANA TATIZO LOLOTE) NILICHANGANYIKIWA.

mama akaniambia nimpeleke tianjin(pale msasani mwisho kwa wachina) nikampeleka nikawaelezea wakaniambia mtoto anatakiwa apate calcium(vitamin D3) tena wakaniambia ni tatizo la watoto wengi sana now days, wao wanatengeneza calcium powder yani ni kama lishe tu inauzwa 45,000/= nikanunua namkorogea mtoto kwenye maji kila siku nampa,its only a week tangu nimeanza kumpa mtoto hiyo calcium ila anamabadiliko makubwa analilia chakua yani anakula mpaka nafurahi. tena hata kama huna hela ya kumnunulia calcium walinishauri nikaushe mifupa ya samaki niisage halafu nihakikishe kila siku asubuhi anakunywya kijiko cha chai kimoja cha unga wa mifupa ya samaki ulichangwanywa na maji au maziwa.

pili mama aliniletea dawa fulani insuch ni multvitamin inaitwa ELYDAC SYRAP, ina vitamin D3 nayo nampa kila siku kijiko kimoja na inapatikana phamarcy.hii nayo inamsaidia kupata apetite maana ina calcium ndani.
if its useful niPM nikupe more details maana mwanangu sasa hata uzito unongezeka
 
Hiyo ELYDAC SYRAP bei gani?
 
Mie wa kwangu ana miaka 6 anasumbua kula huyo, chakula anachokijua ni chips na soseji. Siku akizinduka atakwambia anataka pilau yaani kazi kweli vyakula vingine hana habari kabisa!

Usizoee kumpa mtoto vyakula vilivyosindikwa kama hizo soseji,ni hatari sana kwa Afya,niliwahi kusoma makala moja inasema kuwa vyakula vya aina hiyo vinachochea sana vimelea vya magonjwa ya kansa,moyo pamoja na kisukari
 
kama bado mtoto anambua licha ya ushauri uliopata we anza kummiksia chull sauce na tomato sauce atakula tu
 
dada mwanangu na miezi tisa, alikua hataki kula,akila vijiko viwili tu anabana mdomo,nikimlazimisha kula anatapika mpaka alivyovila juzi, nimpeleka kwa maspecialist wooote wa watoto amepimwa kila kitu,wamesema hana tatizo lolote,nilianzia kwa dk massawe,nikaenda kwa dk hameer,nikaenda hindu mandar,nikaenda tmj,nimemaliza pesa kwa madaktari jamani hadi na mimi nikaanza kukonda,mtoto alizidi kupoteza uzito mpaka akabaki kilo tano just imagine mtoto wa miezi tisa ana kilo tano. sasa mama mkwe wangu akaniambia nimpeleke kwa wachina, nikampeleka wachina wakampima vipimo vyoooote jibu likawa hilo hilo(HANA TATIZO LOLOTE) NILICHANGANYIKIWA....
Nisadie naelezo na mimi hiyo ELYDAC SYRAP nina mdogo wangu ana mtoto ana mwaka na mwez moja ila anasumbua kula sana na pia mtoto hatembei hawa hajaanza kutembea tumetembea hospitar sana huku mkoan ila wanasema hana ugonjwa kinachomfanya kutotembea ni uzito mdogo sio sir inasikitisha sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom