Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
MAAMBUKIZI sugu ya njia ya mkojo (chronic urinary tract infections - UTIs) ni maambukizi kwenye njia ya mkojo ambayo hayatibiki kwa urahisi au yanajirudia mara kwa mara, Fikra Pevu inaripoti kwa kina.
Maambukizi haya yanaweza kuendelea kuathiri njia ya mkojo hata baada ya kupata matibabu sahihi au yanaweza kujirudia muda mfupi baada ya matibabu.
Njia ya mkojo huunda mfumo wa mkojo ukiwa na ogani mbalimbali kama figo, ureta (mirija inayobeba mkojo kutoka kwenye figo kwenda kwenye kibofu cha mkojo), kibofu cha mkojo na urethra (mirija inayobeba mkojo kutoka kwenye kibofu cha mkojo kutoa nje).
Soma zaidi hapa=> Nini Chanzo, Tiba & Kinga ya Maambukizi Sugu ya Njia ya Mkojo (Chronic UTI)? | Fikra Pevu