Nini chanzo cha wizi bongo!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini chanzo cha wizi bongo!?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by lugamba2001, Sep 6, 2009.

 1. l

  lugamba2001 Member

  #1
  Sep 6, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wana jamii forums! hoja yangu, ni nyepesi kuisoma lakini ukiiangalia kwa undani ni nzito! najua kila mtu aweza kutoa jibu lake kwa haraka haraka, lakini mimi napenda tufikirie na tutafiti kwa umakini mkubwa na pengine waliokwishafanya utafiti watuambie, labda tunaweza kuioko jamii yetu!

  Mojawapo ya mambo yaliyonishangaza toka nifike India miezi kadhaa iliyopita, ni kukosekana kwa matukio ya wizi! Licha ya umaskini uliokithiri miongoni mwa vijana wengi katika nchi hii, ikiwa ni pamoja na tatizo la ombaomba na wazee na watoto wa mitaani! Kila ukipita katika majiji makubwa ya nchi hii utakuta watu wengi sana wakifanya biashara za "kimachinga", vibarua na wakilala pembezoni mwa majengo makubwa au kwenye vibanda, kama vile vya kulindia nyani wasile mahindi kule Kasulu vijijini. lakini hawa wanaishi kwenye majiji, kuna magari, pikipiki na baiskeli zisizo na idadi... l

  Jambo moja tofauti na Bongo ni kuwa, hawatakukaba na kukuibia simu, wala hawatakuchomoa pochi yako mfukoni au kukuuzia simu feki achilia mbali roba ya ubao wakikutana nawe gizani au penye kichaka! Mashirika ya umma ndiyo yanafanya biashara zote muhimu za nchi wala hayajafirisika hata wakati mmoja. Sasa swali kwa nini bongo? ukiuliza watakuambia hali ngumu ya maisha? yaani umaskini! ni kweli? mbona wahindi wana hali ngumu? naweza kusema, hata zaidi na bado hawaibi? kuna nini nyuma ya wizi wa Bongo? jamani nisaidieni!
   
 2. M

  Malila JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Kama uliwahi kuwa na jamaa yako aliyekuwa mwajiriwa ktk shirika la serikali au serikali yenyewe na akawa mwaminifu sana kazini nenda ukamuulize au watafute watoto wake uwaulize hivi, does it pay to be honest?

  Nipe feedback ya jibu utakalopewa ndo tuanze mjadala.
   
 3. P

  Preacher JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2009
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uhalifu wote unatoka kwa SHETANI - katika mikakati yake huyu Ibilisi - amewapata hao wahindi kwa mambo mengine - mfano kuabudu ng'ombe, kuabudu masanamu, kufunga ndoa na viumbe (e.g. chura, nyoka etc) eti kuondoa mikosi - hivyo maeneo mengine ya ulimwengu kama Bongo - shetani ametuma mapemo ya wizi mengiiiiii - ndio maana hata wasio na shida kihivyo (mafisadi) bado ni wezi, wakandamizaji - wote ni vyombo vya Ibilisi - matapeli wa kila aina etc. THIS IS WITH REGARD TO SPIRITUAL REALM - yaani mtazamo wa KIROHO - unaweza kupata majibu mengine kwa kupitia mitazamo mingine pia -fanya utafiti au tembea maeneo mengine ya ulimwengu utaona kila mahali kuna tofauti zake za uhalifu - yaani zinazidiana au kutofautiana.
  Ukiingia rohoni utapata majibu ya mambo mengi kiurahisi.
  I submit
   
 4. l

  lugamba2001 Member

  #4
  Sep 18, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli yaonyesha uchovu ni mwingi miongoni mwetu! Ukiwa uwezo wako ni kuona karibu sana, kioo kitafaa kukuonyesha uso wako! Utahisi siku zote we wang'ara, kumbe mwili wako si uso pekee! Na ukishaona umeng'ara sana usoni, ongeza kioo cha pili ili uone na kisogo pia! Je chan'gara pia? Maana binadamu si uso pekee! Ipo siku utazomewa kwa kudhani unang'ara kumbe kioo chakudanya! Wizi utang'arisha usoni, lakini iko siku utakikimbia hata kivuli chako!
   
 5. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  wizi upo kila sehemu Duniani siyo bongo tu
   
 6. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  hakuna sehemu ambayo haina wezi sema tu inategemea na aina ya wizi
   
 7. G

  Gofu Zulu Member

  #7
  Sep 21, 2009
  Joined: Sep 15, 2009
  Messages: 23
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naungana na Malila kama alivyoliweka swali lake lakini twende mbele kidogo ya hapo, hebu tukutane na akina Spika Sita, Mwakyembe, Kilango na wengine wa jinsi hiyo nadhani mwawatambua tujaribu kuwauliza je ukiwa mkweli na muwazi ndani ya chama chetu tawala CCM (Siifahamu tafsiri yake) je kunakalika au utadumu? Wakati tunawauliza swali hilo pia tuwe na kumbukumbu ya watu kama Sokoine, Kibona(Marehemu kwa sasa lakini aliwahi kuwa waziri wa fedha), Horace Kolimba, na wale Wabunge walopewa jina la G20, wako wapi????????

  Gofu
   
 8. G

  Gofu Zulu Member

  #8
  Sep 21, 2009
  Joined: Sep 15, 2009
  Messages: 23
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Preacher nakubaliana nawe kuwa tukienda kiroho basi hayo uloyaeleza ni sahihi kabisa. Hebu tuache wizi huu wa Vibaka ambao twajua hawana chakula yaani mkate wao wa kila siku ndo maana wanaomba wengine wakikosa inabidi watumie mtaji wa Maskini---yaani nguvu zao wenyewe (Walishanichukulia site mirror za gari yangu pale Ubungo nikabaki nawaangalia tu...MUNGU awasamehe sana).Tuwaangalie hawa wanaoiba Billions of money za serikali chanzo chake ni nini hasa???Nadhani muuliza swali ailtaka kupewa majibu kwenye hiyo nyanja.

  Ni kweli wizi ni wizi lakini tunapotoa majibu hatuwezi kuyatoa kiujumla jumla namna hiyo.Preacher naomba utueleze hawa wakwapuaji wa Majisenti haya chanzo chake nini??
   
Loading...